Road Trip yangu ya Kukumbukwa mwaka 2018

safi sana
 
Hahaha, inakua safi sanaaa..kinywaji murua kimenogesha story kabisa..nikajua wanasafiri hamna drinks, ingekua safari mbovuu haina haja ya uzi.
 
Sijawahi kuielewa supu ya samaki, huwa naona kama unakunywa maji yenye shombo hivi...
pole sana ndg yangu.
mwaka juzi nyumbani kwangu tuliwahi kuwa na dada wa kazi kutoka mkoa fulani.

alikuwa ni mchapakazi hodari, shida yake ilikuwa ni ulaji wa nyama ya kuku.

ukileta nyama ya kuku nyumbani, atapika na kuiunga vizuri, ila ikija mezani hali. cha ajabu mayai yake alikuwa anakula.

siku moja wife akamuuliza kwanini hali nyama ya kuku, akajibu ni sharti la huko kwao alikotoka, bibi yake alimwambia siku akila kuku ataugua ghafla homa kali.

basi tukawa tunaishinae kwa style hiyo.
View attachment 2401047
 
Hahaha, inakua safi sanaaa..kinywaji murua kimenogesha story kabisa..nikajua wanasafiri hamna drinks, ingekua safari mbovuu haina haja ya uzi.
hahaha
 
Ujue kuna pombe ukinywa huoti ndoto mbaya, katandike hizi za bukubuku uone koo linavoanza kuwasha, kichwa kinakua kizito kama ulibeba matofari basi tu dunia haina usawa
hii comment imenivunja mbavu sana. haya weekend ndio hii imeshaanza.
 
Huu uzi hauja utendea haki.
Nilitarajiwa kuona V8 ikikata mbuga/lami Ila umeweka video ya miti na ziwa
 
Nilitarajiwa kuona V8 ikikata mbuga/lami Ila umeweka video ya miti na ziwa
niwie radhi ndg.
front view video ya hii roadtrip ipo, ila file ni kama limekuwa damaged maana ni siku nyingi sana(2018).kila nikijaribu ku transfer kutoka kwenye flash disk kuja kwenye simu, inakataa

badala yake nakuwekea hii. hapa ni 2020, nikiwa na jamaa zangu tuki drive toka singida kuelekea arusha. sikumbuki ni eneo gani nilirekodi hii video maana siko familia sana na barabara ya singida-arusha. ila ninachokumbuka tulikuwa tunaitafuta katesh.

ilikuwa ni miezi ya masika, bila shaka utaenjoy kutazama front view ikionyesha barabara, landscape na uoto wa asili.

NB:
ilikuwa ni trip ya kikazi, gari tuliyotumia ni toyota hiace wagon grand cabin, mali ya taasisi fulani.enjoy.
Your browser is not able to display this video.
 
R I p
 
Sijawahi kuielewa supu ya samaki, huwa naona kama unakunywa maji yenye shombo hivi...

Jiandae, nakuandalia trip ya kwenda kula samaki wa maziwa ya Tabora.

Samaki wanachemshwa supu kisha wanapakwa asali na kubanikwa....

Ukitengewa unapewa supu pembeni na samaki aliyebanikwa na asali....

Usijesema Tabora kuna ulozi, ni Mahaba na ukarimu tu kwa wageni...😊😊
 
nilikuwa tabora december 2021 na hiyo ndio ilikuwa trip yangu ya kwanza kufika mkoa huo.

sijui kwanini sikuulizia kuhusu hao samaki wanaopakwa asali.
 
nilikuwa tabora december 2021 na hiyo ndio ilikuwa trip yangu ya kwanza kufika mkoa huo.

sijui kwanini sikuulizia kuhusu hao samaki wanaopakwa asali.

Wanapatikana kwa oda, Bi. Kalunde ndo mtaalamu wa kuwaandaa.

Hutojutia ukifika wakati mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…