Road Trip yangu ya Kukumbukwa mwaka 2018

Road Trip yangu ya Kukumbukwa mwaka 2018

smarte_r Ukiangalia kwa ukaribu wengi nchi yetu hatuijui kabisa. kila mtu anapambana kwenye kona yake na anakotoka. Kama wewe kwenu ni Songea basi ni basi moja kwa moja au private car Dar-Songea. Kama wa Kigoma, basi ni hivo hivo. Kuna watu wa Lindi, hawajawahi kuvuka Chalinze kwenda Morogoro. Mfano natokea kanda ya ziwa, na maisha yangu yote, sijawahi vuka Mbagala kwenda kusini! yaani kila opportunity ya likizo nafikiria kuwasha gari na kuelekea kwetu. In fact, nadhani kuhamia Dodoma, imesaidia wengi kupita barabara ya Dar-Moro-Dodoma.

Nimeamua kubadilisha hii tabia. Naanza na trip next year, ya kutembelea mikoa ya kusini. Lindi-Mtwara-Masasi-Tunduru nk.

WaTanzania tumebarikiwa na nchi nzuri sana. Lets make the most of it!
 
Naandika article hii baaada ya kupata inspiration kupitia uzi wa rrondo Wazee wa ‘road trip’ mpo?. Mimi ni subscriber wa uzi huu.

Ilikuwa december 2018 nikiwa na jamaa zangu watano wa idara fulani.Katika hao watano mmoja alikuwa dereva.

Gari tuliyotumia ni off-road toyota land cruiser 4.5 v8 dlx 2013. Mimi sio mtaalamu wa magari, watu wa magari mnajua speed yake na namna inavyoweza kuhimili mikimikiki ya safari ndefu.

Trip ilianzia dar mpaka musoma. We stayed at musoma for six days. Then we left for another roadtrip to Bukoba.

Tuliondoka Musoma saa 11 asubuhi. Around saa nne asubuhi tukafika kivuko cha Kigongo-Busisi Mwanza. Tukavuka na kuanza safari ya kuitafuta Geita Town.

Tulifika Geita na kupumzika kwa nusu saa. baada ya mapumziko tukaanza safari ya kuitafuta Chato.

Tulipita Buzirayombo, Itari then Chato. Tulisimama kidogo kwenye makazi ya marehemu Magufuli. Tukapiga story kidogo na jamaa zetu tuliowakuta pale nje kwenye Mgahawa wake. Sina hakika kama ule mgahawa bado unaendelea kutoa huduma au lah.

Wale jamaa zetu wakatukaribisha supu ya samaki Sato. Hatukulaza damu, supu ilikuwa tamu sana. Wale sato walikuwa ndio kwanza wametoka kuvuliwa ziwani, si unajua tena kanda ya ziwa.

Mwaka 2018 Magufuli alikuwa wa moto sana, he was in his prime time kiasi kwamba kama ulikuwa safarini na gari ukatize Chato jirani na makazi yake, unajikuta tu unakatiza kwa heshima na adabu(nimechomekea tu, hili sio jukwaa la siasa[emoji1787]).

Basi tukaamsha zetu kuitafuta Nyamirembe, Katemwa, pori la Biharamuro, Nyakabongo, Kyamyorwa, Muleba na hatimaye around saa tatu usiku tukaingia zetu Bukoba town.

Tulikuwa hatuna haraka, mwendo wetu ulikuwa very reasonable kama watalii vile. Tulisimama mara kwa mara njiani kupiga picha na simu zetu.

Kwangu hii ni trip ya kukumbukwa sana, ilijaa matukio mengi ya furaha, utani, vicheko na story za hapa na pale.

Kipande cha kutoka Geita kuitafuta Chato tulichangamka sana, kwasababu tukiwa Geita tulinunua chupa mbili kubwa za Jameson. Mimi na wenzangu wanne ndio tulikuwa tunazinywa.

Dereva wetu ni kijana wa kipemba, ustaadh fulani mjanja mjanja. Yeye na mambo ya ulevi tofauti. Starehe yake kubwa ni watoto wa kike[emoji1787].

Naambatanisha kipande cha video nilicho record siku hiyo. Ila sikumbuki exactly ni aneo lipi. Nadhani ni Nyamirembe au Nyakabongo. Nawaachia assignment wakali wa location.

NB: Mmoja kati ya jamaa yangu niliyekuwanae kwenye hii road trip ameshatangulia mbele ya haki miezi mitatu iliyopita. I dedicate this thread to him. May his soul continues to rest in peace. We are dust and to dust we shall return.
Eeeh
 
smarte_r Ukiangalia kwa ukaribu wengi nchi yetu hatuijui kabisa. kila mtu anapambana kwenye kona yake na anakotoka. Kama wewe kwenu ni Songea basi ni basi moja kwa moja au private car Dar-Songea. Kama wa Kigoma, basi ni hivo hivo. Kuna watu wa Lindi, hawajawahi kuvuka Chalinze kwenda Morogoro. Mfano natokea kanda ya ziwa, na maisha yangu yote, sijawahi vuka Mbagala kwenda kusini! yaani kila opportunity ya likizo nafikiria kuwasha gari na kuelekea kwetu. In fact, nadhani kuhamia Dodoma, imesaidia wengi kupita barabara ya Dar-Moro-Dodoma.

Nimeamua kubadilisha hii tabia. Naanza na trip next year, ya kutembelea mikoa ya kusini. Lindi-Mtwara-Masasi-Tunduru nk.

WaTanzania tumebarikiwa na nchi nzuri sana. Lets make the most of it!
Tanzania ni tamu Sana kwakifupi kila sehemu utaenda utafutahia mazingira yake na Hali ya hewa tamu.
Mimi sio MTU wa kanda ya ziwa huwa napenda Sana kufanya safari za Huko nikifika mwanza huwa moyo wangu unachangamka mno kutokana na mandhari yake
 
Back
Top Bottom