Road Trip yangu ya Kukumbukwa mwaka 2018

smarte_r Ukiangalia kwa ukaribu wengi nchi yetu hatuijui kabisa. kila mtu anapambana kwenye kona yake na anakotoka. Kama wewe kwenu ni Songea basi ni basi moja kwa moja au private car Dar-Songea. Kama wa Kigoma, basi ni hivo hivo. Kuna watu wa Lindi, hawajawahi kuvuka Chalinze kwenda Morogoro. Mfano natokea kanda ya ziwa, na maisha yangu yote, sijawahi vuka Mbagala kwenda kusini! yaani kila opportunity ya likizo nafikiria kuwasha gari na kuelekea kwetu. In fact, nadhani kuhamia Dodoma, imesaidia wengi kupita barabara ya Dar-Moro-Dodoma.

Nimeamua kubadilisha hii tabia. Naanza na trip next year, ya kutembelea mikoa ya kusini. Lindi-Mtwara-Masasi-Tunduru nk.

WaTanzania tumebarikiwa na nchi nzuri sana. Lets make the most of it!
 
Eeeh
 
Tanzania ni tamu Sana kwakifupi kila sehemu utaenda utafutahia mazingira yake na Hali ya hewa tamu.
Mimi sio MTU wa kanda ya ziwa huwa napenda Sana kufanya safari za Huko nikifika mwanza huwa moyo wangu unachangamka mno kutokana na mandhari yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…