G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Baada ya gwiji la sheria la kimataifa ndugu Robert Amsterdam kufanikiwa kuishawishi idara ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya kuijadili Tanzania dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hatimaye kusubiri hatua rasmi za kinidhamu kuchukuliwa, sasa Robert amethibitisha rasmi kuwa jumatatu anaenda ICC kufungua mashitaka dhidi ya uhalifu wa binadamu nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa kanuni za ICC, endapo mashitaka yatafunguliwa basi Tanzania itahitajika kupeleka utetezi wake na kisha pande zote mbili kujadiliwa kwa kina.
Sasa mataifa mbalimbali yanaendelea kuchukua hatua dhidi ya Tanzania baada ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhuru kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.