Robert Amsterdam athibitisha kufungua mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa Tanzania ndani ya ICC jumatatu

NaSupport kwa 100% wahalifu walioharibu Uchaguzi wafunguliwe mashtaka lakini SiSupport vikwazo vya kiuchumi kwa Tanzania!
 
Baada ya gwiji la sheria la kimataifa ndugu Robert Amsterdam kufanikiwa kuishawishi idara ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya kuijadili Tanzania dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hatimaye kusubiri hatua rasmi za kinidhamu kuchukuliwa, sasa Robert amethibitisha rasmi kuwa jumatatu anaenda ICC kufungua mashitaka dhidi ya uhalifu wa binadamu nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa kanuni za ICC, endapo mashitaka yatafunguliwa basi Tanzania itahitajika kupeleka utetezi wake na kisha pande zote mbili kujadiliwa kwa kina.

Sasa mataifa mbalimbali yanaendelea kuchukua hatua dhidi ya Tanzania baada ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhuru kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Kwa hiyo unafurahi sana? Huu ni upumbavu usio kifani
 
Mmeshindwa kupambania freedom hapa Tanzania kwa maandamano aliyoitisha Lissu wenu ,mkamsaliti !.Leo hii mnaona wazungu wakombozi wenu! Mpo kama Nyumbu hivi! Mnashindwa kujisaidia Alafu mnataka msaidiwe,!.
Tugawane silaha nusu kwa nusu alafu tupigane..si zimenunuliwa kwa kodi zetu...mnaonaje MaCCM
 
Maria Sarungi si alishatushtaki kama Taifa? Au mashtaka mawili tofauti?
Maria Sarungi alishashitaki
ACT walishashitaki
Bob Amsterdam atashitaki
Kuna coalition ya sisi civil servants Tz nasi pia tuna jambo letu pale ICC.

Lazima mtu awekwe kati dadeki..... left right and centre!
 
Baada ya gwiji la sheria la kimataifa ndugu Robert Amsterdam kufanikiwa kuishawishi idara ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya kuijadili Tanzania dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu na hatimaye kusubiri hatua rasmi za kinidhamu kuchukuliwa, sasa Robert amethibitisha rasmi kuwa jumatatu anaenda ICC kufungua mashitaka dhidi ya uhalifu wa binadamu nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa kanuni za ICC, endapo mashitaka yatafunguliwa basi Tanzania itahitajika kupeleka utetezi wake na kisha pande zote mbili kujadiliwa kwa kina.

Sasa mataifa mbalimbali yanaendelea kuchukua hatua dhidi ya Tanzania baada ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhuru kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Zitto huyo katika ubora wake, dogo una hasira sana na nchi yetu. Sikia dogo, ukiona vipi we hama tu nchi nenda katafute raha huko Yemen, Somalia, Sudan, ama Afghanstan.
 
Hamna kitu hapo,wazungu wanaangalia interest zao kwanza,,itakua dana dana hadi mnashitukia mwaka 3000 huu hapa,,
Badili mbinu,,UkAwA tuliwambia kosa la kususia bunge la katiba litawacost miaka 100.
 
Mungu wabariki Wazungu, kwa kweli huyu rafiki yetu ndio pekee anayeweza kumnyima usingizi huyu dikteta wetu kwa sasa.
 
Hamna kitu hapo,wazungu wanaangalia interest zao kwanza,,itakua dana dana hadi mnashitukia mwaka 3000 huu hapa,,
Badili mbinu,,UkAwA tuliwambia kosa la kususia bunge la katiba litawacost miaka 100.
Sasa jiandaeni kuwasindikiza watu wenu Icc
 
Kuwa dikteta kwenye Dunia ya sasa inahitajika uwe na roho ya mwendawazimu

Hebu cheki Russia pamoja na ubabe wake wote bado akipigwa vikwazo vya kutokutumia $$$ anayumba kama mlevi

Ndio maana kumbe watu wenye akili kama JK ,Mkapa& Mwinyi walichukua $$$ za kutosha halafu wakakabidhi vijiti
 
Dikteta pekee anayefahamika na kila mtu ni huyu Mr Mzungu anayedai huduma za afya, maji na elimu eti siyo maendeleo. Anawalazimisha chama kisiwe na uwakilishi wa wabunge. Labda na huyu Mr Hai ambaye chama hatimaye kimemparaganyikia mikononi mwake.
 
Si mlimtamtafuta mbunge aliye ingia bungeni kwa hisani ya mtu wa Chato, Halima Mdee mlisema analysis vikao anachelewesha maendeleo. Sasa mnamtaja wa nini tena?
Huyo aliyeshinda kwenye jimbo lake,kikao cha chama gani kilimpitisha,kwani aligombea ili ashindwe? Au kwa vile hakushinda majimbo ya kaskazini ndo mnamnyanyapaa...
 
Hata mwenyewe hajui alishindaje kwakweli. Inawezekena akawa afisa kipenyo
 
Back
Top Bottom