Uchaguzi 2020 Robert Amsterdam na Sheikh Ponda ndio watakaomuangusha Lissu

are u Muslim? Nani kaisikia hiyo
YEHODAYA, Jamaa hapo juu kakuhoji swali lenye mantiki kabisa - labda niongezee kidogo kwa kukusaidia: Fanya tafiti kuhusu dini ya kiislaam na Jumuhia zake wakati wa koloni pamoja na umoja wao na ujasiri walio kuwa nao katika kupinga udhalimu wa kikoloni bila woga - ndio waanzilishi wa chama kupigania Uhuru wa Tanganyika lakini for some strange reasons hilo huwa alisemwi , likisemwa ni kijuu juu tu as if Muslims contribution katika harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika was insignificant!!

Nguvu na umoja wa Waislaam uliteteleka baada ya kuundwa kwa BAKWATA kutokana na shinikizo la kutaka kuwa-contain nguvu za kiislaam Nchini, hayo nilisimuliwa na ndugu yangu wa karibu aliye kuwa kwenye harakati hizo kuanzia kwenye 1940s mpaka 1967 - majority hawakuunga mkono kuvunjwa kwa jumuhia yao na kuanzishwa kwa BAKWATA, ninacho taka kusema hapa MTU kama Sheikh Ponda sio wa kuchukulia POA hata kidogo, wengi wanao jaribu kumponda na kumukejeri ni wanafiki tu na kutaka kujipendekeza lakini deep down wanajua ushawishi alio nao Ponda.
 
Yes. Kama angesimama yeye kama Lisu lakini siyo kama Amsterdam
Msimlaumu Lissu kwenda kumuajiri Amsterdam kama wakili wake, kwani kuna nguvu kubwa ambayo iliyotaka kumuondoa uhai wake. Na Amsterdam yupo kisheria, anayoyafanya ni kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na wanadamu kufuatwa, kama hafuati sheria basi kwani Tanzania hakuna mwanasheria mkuu?

Basi awashitaki huyo Amsterdam na mteja wake kwa mambo wanayoyafanya, lakini leo Lissu anagombea nafasi kubwa kabisa katika nchi hii na mpaka sasa anasubiri kupigiwa kura na wanaomkubali kwa mujibu wa sera za chama chake. Nina uhakika Magufuli asingewabana wapinzani na baadhi ya wanachama wake basi uchaguzi huu asingepata tabu kabisa. Uchaguzi ukiwa wa haki na huru basi tutegemee chama kikubwa cha upinzani kitakuwa CCM.
 
Wewe huna taaluma za kisiasa na uongozi.Kaa uangalie mambo yaendevyo.
Lisu na Chadema na ACT na hata Ponda ni wataalamu sana wa siasa.Act wameona ukweli baada kujua mgombea wao ni kupoteza muda na nguvu bure.Chadema wamejuwa waislamu ni kundi kubwa la wapiga kura.Muda huu ni kutafuta ushindi kwanza. Kama hapo baadaae watamgeuka Ponda na wafuasi wake kama watangulizi wao walivyofanya ni kitu kingine.

sheikh Ponda naye baada ukweli kuuona kwa tawala zote zilizotangulia kila moja inampita mwenzake katika kuwakandamiza na kuwabagua waislamu,hana makosa kabisa kumfuata Lissu kwa tamaa huenda ikawa nafuu kuliko wenzake.
Sijui nini kimekuudhi kwa Lissu kuwa karibu na waislamu wakati wa haja.Mbinu hii aliitumia sana hayati Nyerere raisi wa mwanzo wa Tanzania.
 
Yupo kisheria za kwake siyo za tz
 
Wewe hujui siasa za tz,! Ndio maana ccm itaendelea kutawala.

Lisu sijui hana washauri, kaenda Zanzibar alafu anatamka eti sisi chadema hatuna maslahi na Zanzibar. Kiufupi Lisu hajui siasa ya tz ili uungwe mkono wakupe urais unapaswa kuwaje.
Wewe unadhani ili ukubaliwe na wahafidhina wa Tz lazima utunishe misuli na uoneshe ubabe kuhusu Muungano.Hii sio siasa safi.Afadhali ukubali haki itendeke kila eneo ili amani itawale na nchi iwe salama.Waiengereza na Wamarekani na Warusi wangekuwa na akili kama za Tanzania basi nchi zao zingeingia matatizoni zamani na zisingekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi na kiteknolojia.
 
Sawa Ponda kawaambia waislamu mfanye hivyo na Lisu atashinda sehemu yenye waislamu wengi kwa mujibu wako!

Likini umeshajiuliza ni vipi Wakristo nao maamuzi yao baada ya taarifa za Ponda?
Mimi ni mkiristu lakini kura kwa Lisu tu
 
Tanu ilianzishwa msikiti gani? ndani ya msikiti upi? WAanzilishi wa Tanu walikuwa nchi nzima hawakuwa watu wa Dar es salaam tu!!! unachotaka kutuaminisha wewe ni kuwa wanachama wa mwanzo wa Tanu walikuwa watu wa DAr es salaam tu mikoani walikuwa hawapo

Kila mkoa ulikuwa na watu wake walioanzisha tawi la TANU kwenye mikoa yao ukienda kila mkoa wako kibao walitoa hadi nyumba zao kuwa ofisi za TANU lakini hata huko mikoani japo sehemu zingine wote ni wakristo lakini TANU haikuanzia kanisani kama ambavyo TANU dar es salaam haikuanzia msikitini MPAKA IITWE ILIANZISHWA NA WAISLAMU
 
Sawa Ponda kawaambia waislamu mfanye hivyo na Lisu atashinda sehemu yenye waislamu wengi kwa mujibu wako!

Likini umeshajiuliza ni vipi Wakristo nao maamuzi yao baada ya taarifa za Ponda?
Nasubiri nione kura kutoka maeneo yenye waislamu wengi
 
Sawa Ponda kawaambia waislamu mfanye hivyo na Lisu atashinda sehemu yenye waislamu wengi kwa mujibu wako!

Likini umeshajiuliza ni vipi Wakristo nao maamuzi yao baada ya taarifa za Ponda?
hata ss wakristo tunasema Niyeye#
 
Kuna watu hawasemwi ila walitoa mchango mkubwa wakati Tanu inaanzishwa na pale Nyerere alipotakiwa kwenda ulaya lakini walikuwa wakiristo.

Kama mtu anafikiri ataingia ikulu kwa nguvu ya dini anajidanganya hakuna mtanzania anayetaka kuharibu nchi yake kwa ushabiki wa dini
 
Tulieni tuli legezeni masaburi yenu ili sindano iwaingie vizuri.
 
Ingawa ni kosa kuingilia, lkn ukitembea uchi....mhmmm!
 
Hao viongozi wabakwata wapo hapo kwa lengo lakuinufaisha ccm, lkn waislamu tulio wengi tunawafahamu ndio maana tunamsikiliza shekhe Ponda, amejipambanua kama mtu anaepigania maslahi ya waislamu, kwahio sisi tutamfuata kwa sababu nikiongozi wetu, kwalilie analosema maana tunaona ukweli wake.

Hao bakwata wanajua kabisa uma wa waislamu walio wengi hawaikubali bakwata.
 
Lisu ni mwana harakati hajui siasa,

Angekuwa anajua asingempandisha Ponda majukwani,
Pia asingeenda zanzibar na kuropoka kwamba chadema haina maslahi na zanzibar
 
Sheria za TZ ni urithi wa sheria za kikoloni na za hao tunaowaita mabeberu, hivyo ni tabu sana kuweza kufanya maamuzi yetu kama nchi kwa kiburi.
Chini ya Chadema hii ya lisu haiwezekani ila chini ya ccm ya magu tz inaweza kujiamlia mambo yake kwa sheria zake yenyewe
 
Tundu lisu hamjui ponda, ponda hatalidhika na uongozi wa Lisu hata siku moja, na baada ya kuitoa CCM ponda ataanza kumtoa Lisu na nduo atajuta kumjua ponda na ajenda zake.
Sema kilaza wewe wa Lumumbaendo hutampigia kura. Watanzania wengi kwa mamilioni tunampigia kura za kishindo Tundu Antiphas Lissu na kuzilinda
Mtazilinda ila mtazikimbia baada ya kutotosha,
Kila mtu atapita njia yake bila kumwambia mwenzake.😁😁😁😁
 
NAWAPENDA SANA WATANZANIA KWA UMOJA WAO LINAPOKUJA SWALA LA KITAIFA, TUNAAMINI WATAFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KUHAKIKISHA #MAGUFULI ANASHINDA KWA KISHINDO KATIKA UCHAGUZI HUU WA TAREHE 28
 
Magufuli atapigiwa kura na MAGENGE YAKE YA WASIOJULIKANA, wapenda HAKI wote hawawezi kupoteza muda naye.
 
Siku hazigandi mkuu, zinakimbia sana. Miaka 8 hadi 10 nyuma nani alitatarajia Chadema wangewahi kuja kutumia mpaka udini kutafuta madaraka. Upinzani Tz umekuwa wa hovyo kuliko kipindi kingine chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…