Robert Kiyosaki amenibadili leo, Nakuwa bilionea

ze jj

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2012
Posts
497
Reaction score
592
Nmesoma rich dad poor dad na cashflow quadrant. Huyu jamaa hataree. Shida ni kwenye kupata mtaji wa mwanzo ili kuapply knowledge kuwa bilionea. Anafundisha kuajiri na Sio kujiajiri au kuajiriwa. Kumbe kujiajiri Sio utajiri. Kuwafanya watu na pesa wakufanyie kazi ndio utajiri. Aiseee kumbe kuwa daktari, engineer, pilot, mchezaji Sio kitu.
 
Nmesoma rich dad poor dad na cashflow quadrant. Huyu jamaa hataree. Shida ni kwenye kupata mtaji Wa mwanzo ili kuapply knowledge kuwa billionea. Anafundisha kuajiri na Sio kujiajiri au kuajiriwa. Kumbe kujiajiri Sio utajiri. Kuwafanya watu na pesa wakufanyie kazi ndio utajiri. Aiseee kumbe kuwa daktari, engineer, pilot, mchezaji Sio kitu.
Only if you make that theory practically
 
... Aiseee kumbe kuwa daktari, engineer, pilot, mchezaji Sio kitu.

Sasa mkubwa, kama hao sio kitu utakapougua, utakapotaka kujenga, utakapohitaji burudani utapata wapi endapo hao wote sio kitu?

Mie niliambiwa kuheshimu kanuni za fedha, weka akiba, jiufunze kutuna na kutumia pesa yako vizuri, wekeza, ilinde pesa yako. Kisha tumia kipaji au kile unachopenda kukifanya kikuingizie pesa, iwe utabibu, uhandisi, kufundisha n.k
 
Anamaanisha ujiajiri kupitia kipaji au taaluma yako kama wewe in engineer fungua biashara yako eg saichiro Honda
 
Uzuri Robert Kiyosaki haadvocate watu waache kazi zao. Unaweza kuwa umeajiriwa lakini na wewe pia uka"mind your own business", yaani ukawa na shughuli yako ya pembeni inayokuingizia pesa. Taabu sasa ni pale ambapo mwajiri wako hakupi nafasi ya kumind your business (working 7.30am to 5pm, 6 days a week etc) na ndio maana anasema ni ngumu kutoboa ukiendelea kung'ang'ania kuajiriwa tu.
 
Hao waliowarithisha hao 98% wao pia walirithi kutoka kwa watu wengine? Kuna watu wameanzia zero kabisa mpaka kuufikia ubilionea
ni kweli wapo walio anzia zero! unaweza jiuliza kwa nini sasa hv wanaoanzia zero wawe wachache sana jibu ni kuwa mazingira ya kipindi hicho cha zamani yaliwawezesha kufanya hivyo tofauti na karne za 19,20, na 21
 
Uzuri Robert Kiyosaki haadvocate watu waache kazi zao. Unaweza kuwa umeajiriwa lakini na wewe pia uka"mind your own business", yaani ukawa na shughuli yako ya pembeni inayokuingizia pesa. Taabu sasa ni pale ambapo mwajiri wako hakupi nafasi ya kumind your business (working 7.30am to 5pm, 6 days a week etc) na ndio maana anasema ni ngumu kutoboa ukiendelea kung'ang'ania kuajiriwa tu.
utajiri maana yake ni Muda ndio maana hamna tajiri aliyeajiriwa na uwezi fanya vitu viwili vyote kwa wakati mmoja hukutakuwa na ufanisi hata siku 1 kiufupi huwezi kuwa wa moto na ubaridi kwa wakati 1
 
Anamaanisha ujiajiri kupitia kipaji au taaluma yako kama wewe in engineer fungua biashara yako eg saichiro Honda

Hicho ndio nilichomaanisha kwenye post yangu, nilikua napingana na hoja ya kuzarau tasnia au fani zingine kama mleta mada alivyoleta mkuu. Soma vizuri post yake ya mwanzo, anasisitiza kuajiri wengine na pesa ikutumikie.
 
Poa nimekupata sasa
 
Robert Kiyosaki ni great writer amespend maisha yake kupractice anacho kijua na kufundisha watu.

Umesoma vitabu vyake viwil unasema unaenda kuwa billionaire
REALLY
Wealth is the mind set is all about what going on in your mind
Kuna vitu vingi sana vya kukonsida kuwa billionaire.

Nakushauri endelea kusoma sana vitabu
 
Nmesoma rich dad poor dad na cashflow quadrant. Huyu jamaa hataree. Shida ni kwenye kupata mtaji Wa mwanzo ili kuapply knowledge kuwa billionea. Anafundisha kuajiri na Sio kujiajiri au kuajiriwa. Kumbe kujiajiri Sio utajiri. Kuwafanya watu na pesa wakufanyie kazi ndio utajiri. Aiseee kumbe kuwa daktari, engineer, pilot, mchezaji Sio kitu.
Yeye mwenyewe pamoja na kuandika vitabu vyote lakini sio bilionea
 
Mwenye PDF ya hicho kitabu msaada tafadhali
Tafuta thread moja yenye kichwa kama "kitabu kilichobadirisha maisha yako" kama sijakosea. Utakipata pamoja na vingine vingi vizuri. Ningekuwekea kama ningekuwa nacho kwenye simu. Unaweza kugoogle pia.
 
"Kama bado hujafanikiwa kimaisha usitafute kisingizio chochote, bali tafuta njia ya kuweza kukufanikisha"

Zanzibar-ASP
 
Back
Top Bottom