Robo Fainali CAFCL: Simba Sc kukutana na Kaizer Chiefs

Robo Fainali CAFCL: Simba Sc kukutana na Kaizer Chiefs

Ni mechi moja tu mara ya mwisho kua match mbili ilikua kati ya Wydad na Esperance 1st league Esperance alibebwa sana kiasi kwamba Wydad alishindwa kuvumilia hakumaliza mechi na kutoka uwanjani.

CAF wakampa ubingwa Esperance na Fainali ikaanza kua moja nakumbuka ni kama miaka minne kutokea hili tukio
2018-2019 mkuu.
 
Naona kama tunafika Nusu fainali kirahis tu but tuwe makin tu huko ugenini tupate hata droo tu
 
Wewe sio shabiki wa Simba.
Wewe no utopolo.Shabiki wa Simba hawezi toa kauli kama hiyo.
Huu mwaka tutawafurahisha sana

Ushabiki wa timu siyo mali binafsi.

Endelea kujipa asilimia 100% ya ushindi, tunaojua mpira tunaujua umuhimu wa kutomdharau mpinzani.
 
Kaizer chief mashabiki wao wameanza kushangilia maana siku zote dua yao ilikua wanataka kukutana na Simba.
Kwa mujibu wao bora derby kuliko kukutana na wekundu wa msimbazi
Screenshot_2021-05-01_124736.jpg
 
Abdoulaye Traore alipigwa kanzu moja matata na Hussein Marsha, akaona ni fedheha akampiga ngumi, kadi nyekundu ikafuata
Mechi gani hiyo kwani huyu Abdoulaye Traore nakumbuka kwenye ngazi ya vilabu alikuwa akicheza Professional Football Ufaransa.
 
Nasubiri kumuona fundi khama billiat akipambana na kina kahata pale kwenye kiungo.
 
Hawa ndo mnakutana nao
Kaizer hao hao wa 9 kwenye msimamo wa ligi? Ni haohao waliofunga magoli 24 kwenye mechi 25 na kufungwa magoli 28?
Ni hao hao waliocheza mechi 9 za Mabingwa na kufunga magoli 5 tu huku wakifungwa 4?
Yaani hawa watakuwa futari.
 

Attachments

  • VID-20210502-WA0020.mp4
    3 MB
Mechi gani hiyo kwani huyu Abdoulaye Traore nakumbuka kwenye ngazi ya vilabu alikuwa akicheza Professional Football Ufaransa.
Alicheza Ufaransa ni kweli, lakini pia alimalizia mpira kwao Ivory Coast.
NB: Yupo pia mchezaji mwingine mwenye jina kama hilo Abdoulaye Traore, ila ni raia wa Burkina Faso

1619989707268.png
 
Nakumhusha kwa kiwango cha kaizer hana hata uwezo wa kumfunga Yanga hivo nusu fainali ni Simba na Mc Alger/Wydad Casablanca
 
Back
Top Bottom