Robo Fainali Klabu Bingwa Africa: TP Mazembe 4 - 1 Simba SC

Wakuu hii kikosi inayoanza mnaonaje bila chama na kagere.
#CAFCL Kikosi cha kwanza cha Simba dhidi ya TP Mazembe, kwenye mchezo unaopigwa Congo DR, saa 10:00 jioni.

1. Manula
2. Coulibaly
3. Mo Hussein
4. Nyoni
5. Juuko
6. Kotei
7. Mzamiru
8. Mkude
9. Bocco
10. Niyonzima
11. Okwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kocha kazingua unamuanzisha vipi bocco kagere unamuweka nje,,?? Striker butu vilee,, kama alikosa magoli Yale atafunga yapii kocha anazinguaa,,,
 
TV yangu inasema Super Sport 4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyie Yanga mbona mna kimbembele na mechi za Simba kwanini usituachie Simba yetu na nyie mpambane na hali yenu
 
Kocha kazingua unamuanzisha vipi bocco kagere unamuweka nje,,?? Striker butu vilee,, kama alikosa magoli Yale atafunga yapii kocha anazinguaa,,,
Hapana hajazingua Kumbuka tunaenda kujilinda na Bocco anatoa vitu vingi Sana kwa Timu pindi haina Mpira, Bocco huwa anashuka kukaba,Bocco Ni mzuri kutengeneza assist, Bocco mipira ya just yote huwa anaicheza na kumdondoshea mtu ikipigwa na kipa, Bocco akiruka juu inabidi akabwe na beki zaidi ya mmoja Bocco timu pinzani ikiwa inapiga Kona anasaidia kukaba forward wa adui,kagere mzuri tuu kwenye kumalizia na kucheza kwa moyo bila kuchoka ambacho icho kitu siku hizi kwa bocci kipo,ukiangalia vizuri kwenye icho kikosi mvivu kukaba ni Niyonzima tuu hao wengine wote wanakimbia uwanja mzima...tusubiri tuone ila matokeo ya Leo 1-1 Mpira tutachelewesha sana tutaucheza kwa dakika 75

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo na Laptop je ni youtube gani inayoonyesha hii game
 
Aliijua sana na ndo maana alipiga kwa kuipania. Matokeo yake ikawa patupu.
Tuache utani simba kazi mnayo kubwa sana.
Nguvu ya mamba iko kwenye maji
simba wakitulia tp mazembe hana ukali wa kusema anatisha
 
Mahesabu ya kocha ni kuwa na sub yenye nguvu iliyosoma mchezo. Lakini pia hii mechi inaweza kwenda dk 120, ni vizuri kujiandaa mapema kwa lolote.
Lakini pia Akili ya TP Mazembe iko kwa Kagere!! Kutokuanza kwa Kagere kutawachanganya TP Mazembe kisaikologia!!!!
 
simba wakitulia tp mazembe hana ukali wa kusema anatisha
Nakubaliana na wewe mkuu.
Simba wanapata tabu sana kupata goli ugenini, achilia ushindi.
Je, TP Mazembe watakuwa wazembe kiasi cha kuwaachia Simba wajipatie sare ya magoli au ushindi?

Time will tell.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…