Rodgers aiponda BBS na Madam Ritha.

Rodgers aiponda BBS na Madam Ritha.

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
1,255
Reaction score
77
Msanii Rodgers aliyewahi kushiriki mashindano ya Bongo Star Search ameyaponda mashindano hayo kuwa hakuna haki na yanaendeshwa kwa interest za Madam Ritha. Amesema hajutii kukosa nafasi ya kwanza licha ya kushiriki mara mbili.

Amefika mbali kwa kusema Ritha anadhulumu haki za wasanii hao kwa kutengeneza pesa ndefu wakati washiriki ambao ndio wanaofanya mashindano hayo yawepo wanakufa masikini.

Akiongea kwa uchungu Rogers amesema Madam Ritha ndo anapanga nani awe mshindi hata kama hana kipaji. Hali hii inakatisha tamaa na kuwafanya wasanii wachukie aina ya mashindano kama BSS.

SOURCE: TBC (The Avenue program).
 
Siku zoye shukurani ya punda ni mateke.
Heri ufuge mbwa kuliko binadamu

Anadai madam Ritha alianzisha BSS ili kutengeneza hela na si kuinua vipaji vya wasaniih ndio maana baada ya mashindano anakua hana story na mshiriki yeyote kujua anaendeleaje. Amefunguka zaidi na kusema BSS its just a tv show like any other na haina maslahi yoyote kwa msanii.
 
Anadai madam Ritha alianzisha BSS ili kutengeneza hela na si kuinua vipaji vya wasaniih ndio maana baada ya mashindano anakua hana story na mshiriki yeyote kujua anaendeleaje.

Kuna msemo huu huwa naupenda, "MOST LOOSERS END UP HATERS" ndo kinachomkuta huyo Rogers.Kama kweli ana kipaji tungeendelea kumsikia kama anavyosikika KALA JEREMIA pamoja na kubaniwa,kwani alitaka Madam Rita amfanyie nini baada ya hapo wakati mashindano yameisha?Anataka kubebwa ee
 
huyu dogo siku zote alikuwa wp kuya sema haya? Aache unafiki wake....
 
m2 ukikosa elimu bwana mimi ningemjuaje huyo roja kama sio bss sasa unataka ubebejwe wakati kuna wasani wanafanyaga show bure ili wajulikane ila hujui kama wale walikutangaza dah kweli usimpe m2 samaki bali mfundishe kuvua samaki yaani kabebwa kidogo yeye anataka milele
 
Khah, mjini kuna mambo.
Athari ya mibangi hiyo.
 
BSS ni mradi wa mtu sidhani kama wanania kweli ya kuendeleza wasanii
 
Viroja vya bwana rodger hivi!anataka madame amfanyie nini?kwani kuna mkataba wa kibiashar wa muda mrefu pale?
 
Mbona naye alibebwa sana!Kweli shukrani ya punda mateke!Hata kama madame Rita anatengeneza mkwanja inahusu?Si ni project yake kabuni mwenyewe kijasiria mali?Watanzania tuwe na moyo wa shukrani pale tunapooneshwa njia tutembee kwa miguu yetu na siyo kulaumu tu na kusubiri kubebwa siku zote!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
haya ni maneno ya mkosaji! hivi kweli madam alipanga wale vijana wa mbeya na mwanza washinde kweli au ni uwezo wao uliwabeba
 
ki ukweli siielewagi kabisa hii show ya BSS!!wasanii wabovu bovu ndo wanashinda..wa ukweli kabisa chali,mimi hapana elewa kabsa!

ila pia dogo alipaswa kujua namna ya kueleza matatizo yake bana!(anyways..........labda hajui hata namna ya kufanya interview......huwa hawafundishwi kule!!).
kuhusu kupewa mbunye labda ni kweli ila nadhani cha msingi ambacho alipaswa kufanya ni kuutathmini muziki wake ajue namna gani abdilike ili kuendana na soko la ndani.(sina tatizo na kiwango cha rodgers kimuziki.....ila sasa....aina ya muziki wake hapa unauza!!!?
 
We uliyeleta mada kweli unapotosha nimeangalia kipindi lakini sikumsikia hayo maneno uliyomnuukuu. jamani muwe mnaleteta vitu vyene ukweli hivi vitu ndio vinavyochonganisha wakati mwingine. Roger kuna mengi ameongea lakini in general. Ingawa Mimi namuona Roger kama kaisha kisanii. Ingawa anajiona ana kipaji.

Nitarudi.
 
Mfa maji haachi kutapatapa..utaanzisha mradi usio kupa faida?ungeshinda ungeyasema hayo..?namuunga mkono aliyesema heri kufuga mbwa kuliko binadam..lol
 
hii dunia tupo ni ya capitalism and the aim of it is just maximization of profit Rodgers asifikirie kua madam ritha alikua na nia ya kuibua vipaji kwani nia yake ni kumake more money and not otherwise.ila ata hivyo rodgers lazima umshukuru mungu kwani ulipotoka ndo mbali fanya kazi kwa bidii na pia ujiendeleze kimasomo na kufanya biashara ndogo ndogo

"a journey of hundreds miles begins with a single mile"
 
Madam Ritha ofcoz ana interest zake na ndio maana washindi wa BSS hawana lolote angalia Jumanne Iddi cjui kafia wapi
 
Back
Top Bottom