Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mshindi wa Ligi Kuu ya Uingereza na Euro, Rodri, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa kiume duniani kwa mwaka 2024, akiwa kiungo mkabaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo.
Kiungo wa Manchester City, Rodri, ametunukiwa tuzo ya Ballon d’Or baada ya msimu bora uliomletea mafanikio katika ngazi ya klabu na timu ya taifa. Alisaidia klabu yake kushinda taji la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Uingereza mwezi Mei, akionesha kiwango bora baada ya msimu mzuri wa 2022/23.
Aidha, alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya UEFA EURO 2024 kutokana na uchezaji wake mzuri wakati Uhispania iliposhinda taji hilo nchini Ujerumani.
Rodri alikabidhiwa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika Paris siku ya Jumatatu, Oktoba 28 iliyoandaliwa na jarida la Ufaransa la France Football kwa ushirikiano na UEFA.
Soma, Pia:
• Majina ya Vinicius Jr na Jude Bellingham yaondolewa kwenye Viti vyao katika Hafla ya Ballon d’Or usiku huu
• Rodri atua na magongo ndani ya Paris kupokea Ballon d'Or aliyoporwa Vinicius Jr