Wamefanya utoto mkubwa sana, sikutegemea kabisa. Timu yao imekuwa ikitoa mshindi wa ballon d'or karibia kila baada ya miaka 2, ina washindi wa ballon d'or zaidi ya 10, leo unasusa kwasababu unaamini mchezaji wenu alistahili zaidi ya wachezaji wengine.Mimi binafsi sijawahi kuwa shabiki wa tuzo hizi, naamini mpira ni team hauchezwi kama Tennis hakuna mchezaji mmoja akawa bora anaweza kuwa ni special kuliko wenzake lakini ni team ndio mafanikio yanakuja ni kama music awards kama ni band bora inachaguliwa group bora hakuna mwanamziki bora atachaguliwa kutoka kwenye kundi hata kama yeye ni star wa Band. Mpira ndio hivyo bila wenzako 10 nyuma yako hata uwe na mabawa utakabika tu. Ila Madrid utoto mwingi unazira team nzima sababu hamjashinda?