Roho inaniuma mpenzi wangu anataka tuachane kwa sababu hayaelewi maisha yangu

Roho inaniuma mpenzi wangu anataka tuachane kwa sababu hayaelewi maisha yangu

Waziiii! Mi naona mama atembee tu japo inauma moyo...ila itakuwa chachu ya msela kujitafuta. Niliwahi pitia hio situation. It hit me really hard ila nilipata nafasi ya kukua.
Hamna namna kwa kweli, aache tu wenye visu vikali waendelee kula nyama kwa sababu kwa miaka na dahari, always you must have something in order to handle a woman!!

Hata hizo enzi tunazoambiwa eti kulikuwa na mapenzi ya kweli unakuta waliokuwa wanapata mademu utasikia ama ni wapiga ngoma maarufu kijijini, wawindaji au wapiga jembe wa ukweli shamban and all that; seuze hivi sasa!
 
Kipindi nina mgogoro na mpenzi wangu niliomba ushauri humu JF kutokana na tabia za mpenzi wangu wengi walinishauri nijaribu kukaa naye chini na kuzungumza nae kiupole hatimaye nimefanikiwa na tumezungumza .

Katika mazungumzo aliniambia kiustarabu anaona bora tuachane au tuvunje uhusiano kwa sababu zifuatazo

1. Haoni future nzuli na Mimi hivyo anaona kama nampotezea muda

2. Maisha yangu hayaeleweki nimekuwa mtu wa kubangaiza ninaishi maisha ya kubahatisha hivyo bado sijasimama

3. Amejitahidi kuvumilia hali yangu ya maisha lakini uvimilivu unamshinda kwani Miaka yote haoni mabadiliko kila siku niko vile vile haoni hatua yoyote nilioipiga Katika maisha haya.

4. Finally akaniambia amenipa muda anataka kuona maisha yangu yanabadilika anataka kuona natoboa Katika maisha haya

Ila alichoniambia Kikubwa tuvunje uhusiano kama sitoweza kutimiza Yale anayoyataka yeye nimuache aendelee na maisha yake
Mkuu pole sana,,nakuhusia usilazimishe mapenzi,,
Mapenzi ni kama maji ,,yanafata mkondo,,
Kama hakuelewi na maisha yako wewe wachana nae na utapata wa size yako,,
Wapo wanaume wengi magerezani na wengine tumeshawazika na kuwasahau ktk ulimwengu huu,,sababu ya kulazimisha kumridhisha mwanamke,,,
Kingine cha kukushauri ,,
Njoo pm nipe no za huyo mpnz wako nizungumze nae nimuweke sawa mkuu ,,amini atatulia...
 
Mjomba mjomba mjomba mjomba ukiona mwanamke anataka kuachana na akakupa facts kwanini anaona mvunje mahusiano tambua ya kwamba

Huyo mtu ameshakupima ameshaona hamuendani hata ufanye kitu gani tambua ya kwamba ameshakuona hamuendani hivyo hawezi kukuvumilia hivyo anajipanga kujitoa ili asionekane yeye ndo Ana tatizo

Ninachokushauli kwa hivi sasa kaa mbali na huyo mwanamke punguza mawasiliano punguza shobo siku ukimisi mtafute msalimie cha tatu fanyia kazi mapungufu yako mapema ujiweke sawa ili siku atayosema nataka kutoka awe anajiuliza Mara mbili mbili kweli nitapata mwingine kama huyu
 
Swali la kwanza..
Wewe mwenyewe maisha yako unayaelewa mbaka hapo ulipo?

Maisha yangu mpka hivi sasa kwa

Kwa kweli tangu nimalize chuo mwaka 2016 sijabahatika kupata ajira

Maisha yangu sasa hivi nayaendesha kupitia biashara ya dagaa Nyanya na pilipili hoho ndo vinanisaidia kulipia chumba na hela ya kula
 
huyo dem ana akili sana sema tuu wewe hujasoma. Kuliko uje kulia kwamba umesalitiwa kaamua akuchane live kabisa kua maisha yako na wewe yanamshawishi kusaliti ila anashindwa sababu anakupenda hatimaye uzalendo unkaribia mwisho kama hutabadilika. Pili wanawake miili yao hua inadeteriorate kwa speed ya 5G so kaona anazeeka huku haoni future. Amekuambia A HARD TO SWALLOW, UGLY TRUTH.
 
Vipi huyo mpenzi wako na yeye katoboa au anakulaumu tu, chakukushauri achana na mahusiano kwa Sasa maana ndio yanayokurudisha nyuma, maana mda mwingi unayawaza kuliko maendeleo, na huyo mwanamke achana naye ana ngundu badala akutie moyo yeye anakuongezea negative energy tu.
 
Mkuu tafuta pesa uishi kwa furaha na starehe hakuna maisha tofauti na aya ..sio lazima kuoa unaweza chagua kuwa na watoto watakao pata mgao wa mali au ukaacha watu wagombanie jasho lako.
 
Achana nae na upambane, japo utapitia kipindi kigumu hamna namna, huyo kashakuonyesha alivyo ko hata ukifanikiwa uamuzi wa kumuacha au kurudiana naye utakuwa juu yako.
 
Back
Top Bottom