Si kila sehemu lazima uwe fundi kujua. Ulichofanya hapa ni ufundi kujua.
Mtu ana shida, anahitaji msaada na wewe unaleta ngonjera zisizokuwa na kichwa wala miguu.
Ndivyo ulivyofundishwa kwenu, mtu akiwa na matatizo suluhu ni kumchamba. Nimeshangaa sana mwanaume unachamba.
Kama ulikuwa huna cha kusema kumsaidia, akheri ungekaa kimya, wala usingepungukiwa chochote.
Inakuaje unaandika barua yote hii kumuharibia mtu siku, kumtonesha kidonda, kuongeza mzigo juu ya mzigo, kuongeza msiba juu ya msiba.
Wewe binadamu gani unaona fasheni kutokuwa na huruma dhidi ya binadamu mwenzio. Unasaidia watu kweli wewe?
Huenda husaidii, sio kwa kuibua huko dhana usiyo na uhakika nayo kama ina uhusiano na mtoa mada basi tu upenyeze mipasho! Halafu unamshauri afanye maamuzi asilie.
Seriously kuna mwanadamu hafanyi maamuzi! Tatizo la mtoa mada sio kutofanya maamuzi bali anafanya maamuzi yasiyo muongezea thamani anayoitaka. Ulipaswa umshauri afanyeje hayo maamuzi baada ya kuacha kulia.
Halafu Baba, Mtoa mada kasema anapambana na maisha na wewe unaibuka na ushauri wa "pambana watu wakupe hongera wanapoona mafanikio". Inaleta tofauti gani? Nicheke [emoji1787].
Mkuu C kama hutojali nicheki PM tushirikishane mawazo. Usimsikilize huyu fundi kujua ambaye kaokota kapoint huko anadhani kanaapply kila mahali. Lipo tumaini kumpata C unayemtaka. Kama hutoboi maana yake kuna mahali unazingua. So you need to take good care of it.
Nisamehewe mimi[emoji120], nimetuma kama nilivyopokea.