Roho inaniuma nimetimiza miaka 35 sina mtoto wala maisha

Daa mkuu umemaliza kila kitu yani.
 
Maisha utasema huna ukiwa kaburini kwa sasa hata hyo pumzi mshukuru Mungu
 
Pole sana Kama post yangu imekuumiza kwa niaba ya muhusika!

Hata hivyo ukweli unatakiwa usemwe bila kupepesa macho. Sikufikiri Kama nimeandika "michambo" (hata sijui michambo ni vitu gani)

Mimi naamini ndani ya maelezo yangu endapo muhusika atayosoma kwa kutuliza akili hatakosa cha kujifunza

Usitegemee kila siku kupewa ushauri 'soft' huenda usikusaidie sana. Wakati mwingine unatakiwa uambiwe vitu katika uhalisia wake ili ujitafakari

Na mwisho kabisa, inabidi uelewa kwamba anayekusaidia kimawazo si lazima kupamba pamba maneno ili kukufurahisha ndo ujue anakutia moyo!

Wakati mwingine maneno magumu yanaweza kukusaidia zaidi kuliko maneno mepesi mepesi.
 
Gender...?
 
Brather usikate tamaa wanaume hatuzeeki piga kazi IPO siku mwanga utauona
 
Asante Mkuu, nimejifunza kitu.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Dah! nina 27 tu lakin naona nipo nyuma sana mpaka inafika mahali nawaonea wivu walifeli sekondari, Ila nashukuru Mungu amenijalia mtoto mmoja japo napata taabu sana kutunza lakin kwakweli ndo anayenifanya nione raha ya maisha

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Daah miaka 35 huna mtoto [emoji2960] ebu tupige hesabu ndogo hapa labda tuseme mwaka ujao unapata mtoto unakuwa upo na miaka 36 , mwanao anakuwa hadi anafika miaka 6 anaanza darasa la kwanza wewe unakuwa upo 42, anasoma hadi darasa la 7 wewe unakuwa upo na 49 mwanao anakuwa yupo na miaka 13....haya amefaulu kwenda shule ya sekondary ya kata anasoma hadi kidato cha nne, wewe unakuwa upo na miaka 53 wakat mwanao yupo na miaka 17 [emoji2960][emoji2960][emoji2960][emoji2960]...............daah itaendelea
 
Wakati wewe unalalamika hivyo, kuna mwenzako ana 35 na ana watoto kadhaa ila hana uwezo wa kuwahudumia na kuwapa mahitaji ya msingi.

Anawatazama wakiangamia na kuwa na dalili ya future mbaya. Hakuna kitu kina fedhehesha kama uwe na watoto ushindwe wapa malezi bora......

Anyways nikutoe hofu, mwanamke ndie anatakiwa kuvurugwa umri huo ukifika hana Ramani wala familia , kwa mwanaume umri huo ni saa moja asubuhi, bado mapema sana. Ila kwa mwanamke ni saa kumi na mbili jioni jua limezama kiza kimeingia.

Wewe hapo ndani ya huo umri wa miaka 35 unaweza chapa mimba wanawake hata 20 na wakakufanya baba wa watoto 20 ukiwa umri wa miaka 36 ila mwanamke hiyo haiwezekani hata kwa muujiza.

Mwanamke akifika 35 kwanza ana nafasi ndogo sana ya kupata zaidi ya watoto wawili. Ila ni impossible kuwa na watoto zaidi ya hao sababu ya complications mbali mbali za kiuzazi.

Imagine abebe ujauzito miezi 9, alee hadi miaka miwili tu hapo, tayari miaka mitatu hiyo. Miaka 3 jumlisha kwenye miaka 35 ana 38 akijiacha akae sawa baadae miaka 39 au 40 ndio mtoto wa pili..... So unaona namna inavyokuwa tofauti kwa mwanaume.

So nadhani unajitisha tu. Na mwanaume akishafika 35 mapenzi ya kisekondari huo muda hatakiwi kuwa nao.... Yeye ni kutafuta tu pesa.....
 
Usikate tamaa bado hujachelewa! Life starts at 40.. Usijilinganishe na waliowahi.. Kila mmojawetu ana fungu lake na saa yake ya kupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…