Roho Mtakatifu na Mwamini

Roho Mtakatifu na Mwamini

Hakuna jipya ni abracadabra zilezile tu,za Mungu kushuka duniani Kisha kudundwa na jakobo akitaka ambariki, Mungu akapakachuliwa Paja akambariki yakobo, Mungu kwenye biblia katukanwa na kuzushiwa sana
Unamtukana Muhammad kuiba jina la Israel na kupachika kwenye Koran , unataka kutuaminisha alikuwa hajui maana ya jina Israel 😂🤣🤣😂
 
Mwanzo 32:28
Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Muhammad Ali copy jina Israel hakujua maana yake akaliweka kwenye kipeperushi chake Koran 🤣😂😂😂
 
Roho Mtakatifu ndio kipind chake sasa,kama kanisa tunatakiwa jua hlo kama mtoa maana ulivosema..bila yy Kwa sasa mamb hayaendi kabisa..

Ushuhuda,, before sijamjua nilikua nakula sana loss ktk biashara yangu ya mikopo na ilifika kipind nataka rudisha lesen na kufunga ofisi sabb watu wanakopa ndio ila ulipaji ni wa kusumbuana sana..

Baadae ya kufatilia maandiko nikapata neema ya kumjua uyu Roho Mtakatifu aiseeee mamb yamebadilika jumla,, before Mtu sijamwidhinishia mkopo naenda kumuuliza nimpe au nisimpe..ananipa majibu yupi apewe mkopo na yupi asipewe..since then sijawah sumbuliwa kurejeshewa na sijawah dhulumiwa tena..afu wateja kama wote..wapinzan wananifatilia wanazan nimepata mganga amenisaidia hawajui nachojua mm nipo nawazooom tuu na sitowaambia Siri!!!
Waambie ili nao wamjue Mungu wa kweli waachane na ushirikina!
 
Roho Mtakatifu ndio kipind chake sasa,kama kanisa tunatakiwa jua hlo kama mtoa maana ulivosema..bila yy Kwa sasa mamb hayaendi kabisa..

Ushuhuda,, before sijamjua nilikua nakula sana loss ktk biashara yangu ya mikopo na ilifika kipind nataka rudisha lesen na kufunga ofisi sabb watu wanakopa ndio ila ulipaji ni wa kusumbuana sana..

Baadae ya kufatilia maandiko nikapata neema ya kumjua uyu Roho Mtakatifu aiseeee mamb yamebadilika jumla,, before Mtu sijamwidhinishia mkopo naenda kumuuliza nimpe au nisimpe..ananipa majibu yupi apewe mkopo na yupi asipewe..since then sijawah sumbuliwa kurejeshewa na sijawah dhulumiwa tena..afu wateja kama wote..wapinzan wananifatilia wanazan nimepata mganga amenisaidia hawajui nachojua mm nipo nawazooom tuu na sitowaambia Siri!!!
Kwamba hutowaambia hao siri hiyo!
MaanaYesu anasema; enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili,
ila wewe unadai hutowaambia mtu siri ya Yule anayekufanikisha!
Je, huyo uliyenaye; ni Roho Mtakatifu wa Mungu, au roho mtakavitu vya mzungu.
 
Hiki watu wengi hawajakijua. Hakuna miungu mitatu kwenye Biblia ila kuna Mungu mmoja anayejifunza katika nafsi 3 kwa kulingana anataka fanya nini (Mission gani). Aliposema Baba inamaanisha Elohim alipojifunua kama (Muumbaji) aliposema Mwana ina maana Yeheshua (Mkombozi) au Neno katika uumbaji na alipojifunua kama Roho Mtakatifu(Hapa akimaanisha ukamilishaji wa misioni husika) kwenye uumbaji na ukombozi.
Mathayo 28:18-20 aliposema Mtawabatiza kwa Jina la Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu akimaanisha Mungu kujifunua katika nafsi tatu kwa kulingana na misioni. Hii ni sawa na Maji. Maji yakiwa kwenye Liquid state ni Maji. Yakiwa kwenye Gas state ni Mvuke na solid state ni Barafu ila yote ni Maji mkuu.
Haya ni Maarifa Makubwa.

Mungu Baba

Mungu Mwana

Mungu Roho MTAKATIFU.

Kila Mwanadamu aliyezaliwa na Mwanamke anaye Roho MTAKATIFU.

Suala ni UNAISIKIA SAUTI YAKE?

NI MPOLE NA ASIYECHOKA KUKULETEA UJUMBE NA AU KUKUSAIDIA KUISHI KILE ULICHOUMBWA KWA AJILI YAKE...KARAMA AU KIPAJI.

KIPAJI ndicho kitu pekee ambacho kinamtofautisha Mwanadamu mmoja na Mwingine...na hiyo ndiyo Sababu ya KUWEPO KWA WAKATI HUO..A PURPOSE OF YOUR LIFE...(Mh Benjamin Mkapa aliandika kitabu kikielezea PURPOSE YA YEYE KUWEPO HAPA DUNIANI)

Karama au KIPAJI kinatafsiriwa na Roho MTAKATIFU...ndiye msaada mkubwa wa kukusaidia kujitafsiri...kwa Sababu kila anayezaliwa tayari anayo Master Plan ya Maisha yake yote...Compus anayo Roho MTAKATIFU....

Sasa kwa Sababu Tafsiri ya kila kitu hupitia kwenye UBONGO wa Mwanadamu kasoro insanza kutokea hapo kwa Sababu UBONGO hauwezi kuchuja vizuri.. matokeo yake unaweza kupata majawabu yasiyofaa. . Na hapo ndipo unaingia kwenye Mgogoro kati ya majawabu ya UBONGO na Majibu sahihi ya Mwenye DIRA AU MCHORO SAHIHI AMBAYE NI ROHO MTAKATIFU....!

BAADA YA YESU KUPAA MBINGUNI NDIPO IKAWEPO PENTEKOSTE.....NDIPO ROHO MTAKATIFU AKAACHILIWA KWA KILA MMOJA WETU.. MUNGU NA RAFIKI WA WAKATI WOTE...

ROHO MTAKATIFU ANAZUNGUMZA KABISA...mnaweza hata kujoke...He is the Best Friend ever!

Yako mafundisho mengine yanawafanya watu wafikiri kwamba Roho MTAKATIFU anaweza kukuacha kwa kuwa umetenda Dhambi...au anaweza asitake kukusikiliza baada ya wewe kutenda Dhambi...HAPANA..

NI MTU PEKE YAKE ndiye anayejipoteza kwa kufuata AKILI YAKE BADALA YA KUMSIKILIZA ROHO MTAKATIFU...AJAPORUDI TU KWENYE MSTARI NA AKAMUITA ROHO MTAKATIFU WA MUNGU anakutana naye bila kujali hali aliyoko nayo!

Ni ELIMU KUBWA.

NI FURAHA KUBWA KUJITAMBUA NA KUTAMBUA ZAWADI TULIYOKO NAYO..yaani Mungu Roho MTAKATIFU!

Mungu na Rafiki wa Maisha yetu wa wakati wote!
 
Kwamba hutowaambia hao siri hiyo!
MaanaYesu anasema; enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili,
ila wewe unadai hutowaambia mtu siri ya Yule anayekufanikisha!
Je, huyo uliyenaye; ni Roho Mtakatifu wa Mungu, au roho mtakavitu vya mzungu.
ni Roho mtakatifu nilie nae,.. siwez waambie sabb tupo ktk tasnia Moja ni wapinzan wangu kibiashara ila sio maadui ni washindani..

Na kanuni mojawapo ktk biashara ni kuficha Siri Yako ya mafanikio.wao ndio watafute hyo Siri..coz hata wao Wana nguvu wanazitumia toka sehem mbalimbal mara wanavaa mapete,mara mikufu nk na Kuna vitu wanakuja fanya Kwa kificho ktk biashara yangu ili tu waniwin...thus why nikisema sitowaambia mkuuu..
 
Waambie ili nao wamjue Mungu wa kweli waachane na ushirikina!
wameshaambiwa sana uko makanisani mwao na wachungaji wao,wahubiri wao,wainjilisti wao Sina hakika kama wamewasikiliza..

Asa mm sio muhubiri hawatanisikiliza kabisa!!nadhan ni suala la Mungu kumpa mtu tu neema ajue mamb yanavyokwenda.. kumweleza mtu asiye na hyo neema ni kupoteza MDA.
 
Kwa jina la baba, na la mwana na la roho mtakatifu.

Tuombe:

Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu
Roho zetu kwa mwangao

Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji
Uje mwanga wa mioyo

Ee Mfariji mwema sana, ee rafiki mwanana
Ewe raha mustarehe

Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto, burudiko
U mfutaji wa machozi

Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waamini
Neema yako mioyoni

Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu
Kwake yote yana kosa

Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu
Na kuponya majeraha

Ulegeze ukaidi, washa moto wa uadili
Nyoosha upotevu wote

Wape waumini wako, wenye tumaini kwako
Paji zako zote saba

Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila
Wape heri ya milele

Amina aleluya, amina aleluya,
Amina aleluya
Amina.
 
WALA ROHO WAKO MTAKATIFU USINIONDOLEE

Kuna maneno ya Zaburi yanayonipa tafakari sana.

Mzaburi anamwambia hivi Mungu:

_Usinitenge na uso wako, Wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee _ (Zab‬uri 51:11‬ )

Hivi kumbe kuna uwezekano wa kuondolewa Roho Mtakatifu?

Mimi nilidhani tukiisha kumpokea Roho Mtakatifu basi anabakia kwetu HATA KAMA TUKIENDA kinyume na maagano yetu na Mungu.

Lakini niliposoma katika Maandiko, nikagundua yakuwa, MAFARISAYO nao walikuwa WAKIDHANI HIVYO HIVYO, na kuringa kuwa wao ni wa UZAO wa Abrahamu hivyo watabakia hivyohivyo *Hata wafanye maovu kiasi gani. *

Lakini Yohana Mbatizaji aliwaambia ukweli kwa kusema;

_Msifikiri na kujisemea, Baba yetu ni Abrahamu. _

Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu (Mathayo 3:1-17)

Maana yake, kumbe wangeweza kuupoteza ule urithi wa kuzaliwa akapewa mwingine.

Tena Yohana aliwathibitishia yakuwa, wala sio *vigumu kwani hata mawe yangeliweza kuinuliwa mahali pao. *

Mchungaji mmoja aliwahi kuniambia eti;

Yeye alikuwa AMEPAKWA MAFUTA, hivyo, hata AKIFANYA Matendo maovu, lakini akisimama madhabahuni kuhubiri, pale anamwakilisha Yesu na sio yeye na Yesu NI lazima anakuwepo akisimama nae. Yeye anaendelea kutumiwa tu kama chombo.

Nilibaki nikiduwaa na kushangaa.

NIKAJIULIZA! HIVI Yesu HANA NAMNA BALI ANALAZIMIKA hata KWA njia NAJISI ili AWEZE kuwafikia watu ?

Nilichogundua ni kuwa mchungaji huyu, alikuwa na KIBURI cha KUHALALISHA Uovu wake, akidhani, anastahili hata katika UOVU wake.

Nami nikadhani eti, NIKISHABATIZWA na Kumpokea Roho Mtakatifu, Basi, *hatoki kwangu. *

Kumbe nikagundua SIO KWELI.

_Mungu hakai na au hatendi ndani ya chombo kilicho najisi. _

Ni dhahiri kuwa tunapoenda kinyume na AHADI ZETU, Roho Mtakatifu ANAWEZA kutuacha.

Haya yalimtokea Mfalme Sauli aliyekuwa MASIHI (Mpakwa Mafuta) wa Bwana.

Alipoenda kinyume na Mpango wa Mungu, Ufalme uliondolewa kwake na Alipoteza nafasi iliyoendana na kupakwa Mafuta kwake.

Samweli alimwambia hivi;

Uasi ni sawa na dhambi ya KUPIGA RAMLI, na KIBURI ni sawa na uovu na kuabudu VINYAGO.

Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme (1 Samueli‬ ‭15:23‬)

Mzaburi anamwomba Mungu kuwa ASIMWONDOLEE ROHO WAKE MTAKATIFU kwa sababu alijua ya kuwa bila ya yeye, HAWEZI KUFANYA LOLOTE.

Tuliona mfano wa Samsoni Mnadhiri wa Mungu.

Mara zote alikuwa akitenda kwa njia ya ROHO WA BWANA.

Alipoenda KINYUME na mpango wa Mungu, Roho Mtakatifu ALIMWACHA.

Samsoni hakuelewa hilo.

_*Yeye alibaki AKIENDELEA na MAZOEA. * _

Maandiko yanasema; (Samson) Akaamka katika usingizi wake, akasema, NITAKWENDA NJE KAMA SIKU NYINGINE, na kujinyoosha.

Lakini *hakujua ya kuwa Bwana Amemwacha *(Waamuzi 16:20)

Ni mara nyingi sisi nasi tunadhani tunaandamana na Roho wa Mungu lakini kumbe alikwisha KUTUACHA kutokana na KIBURI na UASI wetu.

SAMSONI hakujua hilo.

Aliendelea ma mazoea yake akidhani atawashinda Wafilisti.

Lakini akajikuta ni mdhaifu, akakamatwa na kutobolewa macho.

Mara nyingi na kwa hiari yetu wenyewe tunaweka makubaliano yetu na Mungu ili yeye ATENDE NASI kwa njia ya *Roho wake Mtakatifu. *

Kwa kufanya hivyo, Mungu ANATUPA Roho wa Kufanya yale yaendanayo na makubaliano yale.

Lakini tunapoenda kinyume, Roho wa Mungu ANAWEZA kutuacha. Tena, anaweza kutuacha MAZIMA kama SAULI

Mara kwa Mara, tunayarudia maagano yetu ya Ubatizo, kwamba:

Tunamkataa shetani na mambo yake yote…

Ni wazi kuwa, sisi ni dhaifu, na kukosea ni ubinadamu wetu.

Lakini tunapokuwa na Kiburi cha Uzima na KUASI kwa makusudi huku tukidhani Roho wa Mungu anaendelea kutenda nasi, tutakuwa tunajidanganya.

_Nilimjibu yule mchungaji hivi; _

Ni afadhali kutokuweka makubaliano fulani na Mungu kuliko kuyaweka na kuyavunja ukidhani Eti umepewa UPENDELEO. Huko ni kujidanganya kwa KIBURI cha UZIMA.

Ni Muhimu kukumbuka pia yakuwa ROHO Mtakatifu anapo mwacha mtu, *nafasi yake huchukuliwa na roho mchafu. *

Katika mazingira hayo, mtu anakuwa akiongozwa vibaya na roho aliye kinyume na Mungu, ndipo mtu anaanza kuwa na sifa au TUNDA la ROHO MCHAFU ambalo ni *Macho ya Kiburi; Ulimi wa Uongo; Mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uzaao mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo na asemaye uongo; Apandaye mbegu za fitna kati ya ndugu * (Mithali 6:15-19).

Hili ni kinyume na TUNDA LA ROHO MTAKATIFU ambalo ni Upendo; Furaha; Amani; Uvumilivu; Utu wema; Fadhili; Uaminifu; Upole; Kiasi (Wagalatia 5:22-23)

*TUSIMZIMISHE Roho Mtakatifu * (1 Thesalonike 5:19) na *kumkaribisha roho mchafu * kwamaana *MUNGU HAWEZI KUTENDA KATIKA CHOMBO KICHAFU. *

Tudumu katika maagano yetu kwa unyenyekevu na uthabiti ili Roho wa Mungu APATE *kuimarika na kutenda ndani yetu. *

Basi Ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, TAKATIFU, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana ...(Warumi 12:1)

Tumsifu Yesu Kristo

©️ Professor Innocentus Alhamis
 
QURAN IMEANDIKWA NA SHETANI MPINGA KRISTO NA NABII WA UONGO.

QURAN 2:97 - Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

ADUI WA MALAIKA WA MUNGU NDIE ALIYEITEREMSHA QURAN

1.JE ADUI WA MALAIKA WA MUNGU ATAKUWA NANI?????

2. JE ADUI WA MUNGU NI NANI????

JIBU NI SHETANI.

SITAMANI WAKRISTO JIJIFANANISHE NA HILO SHIMO LA KUZIMU UFUNUO 9.
Hiyo ayah Mbona Inafafanuliwa Mara Nyingi Lakin Bado Mnaendelea Nayo,
Qur'an Haiwezi Jikanyaga Kama bible Hata siku Moja

Sitaki Elezea sana kwani Nishaeleza kwenye Nyuzi Nyingi tu.Lakini Adui wa Jibril Ni Watu Wa israel.Allah Anawaambia huyo Adui Yenu Jibril Yeye Ndo kaiteremsha Qur'an Kwa hyo Uadui wenu Na Jibril Usiwafanye Muache Kuamini Qur'an kwani quran Ni maneno ya Allah na sio ya Jibril wala muhammad(S.A.W)
Wao Ni Madaraja Kufika Kwa wahusika.

Kwa nini Uadui wa Jibril na wa israel? Nishaeleza sana tu
 
Kuelewa fumbo la utatu mtakatifu ( Holy Trinity) kwa akili za kibinadamu ni sawa na kuhamisha maji ya bahari kwa kutumia kikombe/bakuli
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Hiyo ayah Mbona Inafafanuliwa Mara Nyingi Lakin Bado Mnaendelea Nayo,
Qur'an Haiwezi Jikanyaga Kama bible Hata siku Moja

Sitaki Elezea sana kwani Nishaeleza kwenye Nyuzi Nyingi tu.Lakini Adui wa Jibril Ni Watu Wa israel.Allah Anawaambia huyo Adui Yenu Jibril Yeye Ndo kaiteremsha Qur'an Kwa hyo Uadui wenu Na Jibril Usiwafanye Muache Kuamini Qur'an kwani quran Ni maneno ya Allah na sio ya Jibril wala muhammad(S.A.W)
Wao Ni Madaraja Kufika Kwa wahusika.

Kwa nini Uadui wa Jibril na wa israel? Nishaeleza sana tu
Jibril ndie au Gabriel au ?
 
Sijasoma vizuri mada, ila kama Wakristo wanavyo mtaja na kumtegemea Roho Mtakatifu.

Wenzetu wana yataja na kuyategemea Majini.
Wale watoto wadogo wanaozaliwa huku wakiijua Qurani na lugha mbalimbali huwa wanapandwa na Majini ya ukoo wa Sharifu.

Ndio maana wanaitwa Masharifu, na pamoja na akili zao zote zile na kuijua kwao Qurani wanaishia kuwa Waganga wa Kienyeji, Wapiga Ramli na Warozi.
Mfano. Sharifu Majini.
Waislamu Roho Mtakatifu wao ni Majini.
Wakipagawa na Majini Sharifu ndio wanakuwa Waalimu Mahili wa Dini ya Kiislamu.

Surah Al-Djini : Ayah 14

وَأَنَّا مِنَّا ٱلۡمُسۡلِمُونَ وَمِنَّا ٱلۡقَٰسِطُونَۖ فَمَنۡ أَسۡلَمَ فَأُوْلَٰٓئِكَ تَحَرَّوۡاْ رَشَدٗا
Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.
..............

Kwenye Kitabu chao Kitukufu Wameyatukuza sana Majini hadi wakayapa Sura nzima,
Sura ya Majini.
Huko misikitini kumejaa makundi ya Majini yaki mswalia Allah.

Eti Majini ndio Waislamu wenzao wazuri.
Yalaaaah..... Rabi.

[emoji23]Daah! Sijui Wakristo akili Ndo Hamna au Hamtaki Kuelewa tu Au Ubishi

Waislamu Hatutegemei majini Tunategemea Mungu Mmoja.

Pia Jini Ni Kiumbe Kama Ulivyo wewe,Mbuzi,Kuku
Hakuna sehemu Katika Quran Imemtukaza jini Ila Allah Ndo ametukuzwa,Pia katika hayo Majini Kuna mema Na majini Mabaya.
 
[emoji23]Daah! Sijui Wakristo akili Ndo Hamna au Hamtaki Kuelewa tu Au Ubishi

Waislamu Hatutegemei majini Tunategemea Mungu Mmoja.

Pia Jini Ni Kiumbe Kama Ulivyo wewe,Mbuzi,Kuku
Hakuna sehemu Katika Quran Imemtukaza jini Ila Allah Ndo ametukuzwa,Pia katika hayo Majini Kuna mema Na majini Mabaya.
Soma 😂😂 waislamu mnalindwa na shetani na Kuna wakristo kitabu Chao kimesema ulinzi wao ni Malaika

Soma
Wakristo wanalindwa na Malaika
Psalm 91:11”For He will give His angels charge concerning you, to guard you in all your ways.

Waislamu wanalindwa na mapepo
Allah anasema
, “Each one of you has a devil-companion from the jinn over him.” saḥīḥ Muslim 2814
 
Injili ya nabii issa naipataje?
Ipo Kwenye Qur'an Kwani Vitabu

Al Imran 3:3
Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili

An Nisaa 4:46
Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake
 
Soma [emoji23][emoji23] waislamu mnalindwa na shetani na Kuna wakristo kitabu Chao kimesema ulinzi wao ni Malaika

Soma
Wakristo wanalindwa na Malaika
Psalm 91:11”For He will give His angels charge concerning you, to guard you in all your ways.

Waislamu wanalindwa na mapepo
Allah anasema
, “Each one of you has a devil-companion from the jinn over him.” saḥīḥ Muslim 2814
Sijui Ni Lugha Ya Kiingereza Imekuchanganya

, “Each one of you has a devil-companion from the jinn over him.” saḥīḥ Muslim 2814

Each One Of You And Not Each Muslim,Je Kama Each One Of you Wanaambiwa Wasio Waislamu.
 
Kuelewa fumbo la utatu mtakatifu ( Holy Trinity) kwa akili za kibinadamu ni sawa na kuhamisha maji ya bahari kwa kutumia kikombe/bakuli
Kwa hiyo Mungu Analeta Dini Ngumu Kuielewa Ili Atuchome Moto?

Kwenye Uislamu Vitu Ni rahisi Kuelewa Na viko Very Straight.
Mungu Mmoja Hafafani Na chochote Na Ndo Maana Tunamuabudu,Kitu cha Tofauti Na sisi,Hiyo Ndo Sifa ya Mungu Tofauti Na Hapo Huyo sio Mungu
 
An Nisaa 4:46
Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake
Huu ni ujinga wa Allah au ni waislamu walibadilisha verse

Koran 5:3 .......Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu,.....

Surah ya tano kakamilisha Uislamu na Kuna surah zaidi ya 100 mbele ?

Ni ujinga wa Allah au ni waislamu wamebadili ?
 
Back
Top Bottom