WALA ROHO WAKO MTAKATIFU USINIONDOLEE
Kuna maneno ya Zaburi yanayonipa tafakari sana.
Mzaburi anamwambia hivi Mungu:
_Usinitenge na uso wako, Wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee _ (Zaburi 51:11 )
Hivi kumbe kuna uwezekano wa kuondolewa Roho Mtakatifu?
Mimi nilidhani tukiisha kumpokea Roho Mtakatifu basi anabakia kwetu HATA KAMA TUKIENDA kinyume na maagano yetu na Mungu.
Lakini niliposoma katika Maandiko, nikagundua yakuwa, MAFARISAYO nao walikuwa WAKIDHANI HIVYO HIVYO, na kuringa kuwa wao ni wa UZAO wa Abrahamu hivyo watabakia hivyohivyo *Hata wafanye maovu kiasi gani. *
Lakini Yohana Mbatizaji aliwaambia ukweli kwa kusema;
_Msifikiri na kujisemea, Baba yetu ni Abrahamu. _
Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu (Mathayo 3:1-17)
Maana yake, kumbe wangeweza kuupoteza ule urithi wa kuzaliwa akapewa mwingine.
Tena Yohana aliwathibitishia yakuwa, wala sio *vigumu kwani hata mawe yangeliweza kuinuliwa mahali pao. *
Mchungaji mmoja aliwahi kuniambia eti;
Yeye alikuwa AMEPAKWA MAFUTA, hivyo, hata AKIFANYA Matendo maovu, lakini akisimama madhabahuni kuhubiri, pale anamwakilisha Yesu na sio yeye na Yesu NI lazima anakuwepo akisimama nae. Yeye anaendelea kutumiwa tu kama chombo.
Nilibaki nikiduwaa na kushangaa.
NIKAJIULIZA! HIVI Yesu HANA NAMNA BALI ANALAZIMIKA hata KWA njia NAJISI ili AWEZE kuwafikia watu ?
Nilichogundua ni kuwa mchungaji huyu, alikuwa na KIBURI cha KUHALALISHA Uovu wake, akidhani, anastahili hata katika UOVU wake.
Nami nikadhani eti, NIKISHABATIZWA na Kumpokea Roho Mtakatifu, Basi, *hatoki kwangu. *
Kumbe nikagundua SIO KWELI.
_Mungu hakai na au hatendi ndani ya chombo kilicho najisi. _
Ni dhahiri kuwa tunapoenda kinyume na AHADI ZETU, Roho Mtakatifu ANAWEZA kutuacha.
Haya yalimtokea Mfalme Sauli aliyekuwa MASIHI (Mpakwa Mafuta) wa Bwana.
Alipoenda kinyume na Mpango wa Mungu, Ufalme uliondolewa kwake na Alipoteza nafasi iliyoendana na kupakwa Mafuta kwake.
Samweli alimwambia hivi;
Uasi ni sawa na dhambi ya KUPIGA RAMLI, na KIBURI ni sawa na uovu na kuabudu VINYAGO.
Kwa sababu umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme (1 Samueli 15:23)
Mzaburi anamwomba Mungu kuwa ASIMWONDOLEE ROHO WAKE MTAKATIFU kwa sababu alijua ya kuwa bila ya yeye, HAWEZI KUFANYA LOLOTE.
Tuliona mfano wa Samsoni Mnadhiri wa Mungu.
Mara zote alikuwa akitenda kwa njia ya ROHO WA BWANA.
Alipoenda KINYUME na mpango wa Mungu, Roho Mtakatifu ALIMWACHA.
Samsoni hakuelewa hilo.
_*Yeye alibaki AKIENDELEA na MAZOEA. * _
Maandiko yanasema; (Samson) Akaamka katika usingizi wake, akasema, NITAKWENDA NJE KAMA SIKU NYINGINE, na kujinyoosha.
Lakini *hakujua ya kuwa Bwana Amemwacha *(Waamuzi 16:20)
Ni mara nyingi sisi nasi tunadhani tunaandamana na Roho wa Mungu lakini kumbe alikwisha KUTUACHA kutokana na KIBURI na UASI wetu.
SAMSONI hakujua hilo.
Aliendelea ma mazoea yake akidhani atawashinda Wafilisti.
Lakini akajikuta ni mdhaifu, akakamatwa na kutobolewa macho.
Mara nyingi na kwa hiari yetu wenyewe tunaweka makubaliano yetu na Mungu ili yeye ATENDE NASI kwa njia ya *Roho wake Mtakatifu. *
Kwa kufanya hivyo, Mungu ANATUPA Roho wa Kufanya yale yaendanayo na makubaliano yale.
Lakini tunapoenda kinyume, Roho wa Mungu ANAWEZA kutuacha. Tena, anaweza kutuacha MAZIMA kama SAULI
Mara kwa Mara, tunayarudia maagano yetu ya Ubatizo, kwamba:
Tunamkataa shetani na mambo yake yote…
Ni wazi kuwa, sisi ni dhaifu, na kukosea ni ubinadamu wetu.
Lakini tunapokuwa na Kiburi cha Uzima na KUASI kwa makusudi huku tukidhani Roho wa Mungu anaendelea kutenda nasi, tutakuwa tunajidanganya.
_Nilimjibu yule mchungaji hivi; _
Ni afadhali kutokuweka makubaliano fulani na Mungu kuliko kuyaweka na kuyavunja ukidhani Eti umepewa UPENDELEO. Huko ni kujidanganya kwa KIBURI cha UZIMA.
Ni Muhimu kukumbuka pia yakuwa ROHO Mtakatifu anapo mwacha mtu, *nafasi yake huchukuliwa na roho mchafu. *
Katika mazingira hayo, mtu anakuwa akiongozwa vibaya na roho aliye kinyume na Mungu, ndipo mtu anaanza kuwa na sifa au TUNDA la ROHO MCHAFU ambalo ni *Macho ya Kiburi; Ulimi wa Uongo; Mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uzaao mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo na asemaye uongo; Apandaye mbegu za fitna kati ya ndugu * (Mithali 6:15-19).
Hili ni kinyume na TUNDA LA ROHO MTAKATIFU ambalo ni Upendo; Furaha; Amani; Uvumilivu; Utu wema; Fadhili; Uaminifu; Upole; Kiasi (Wagalatia 5:22-23)
*TUSIMZIMISHE Roho Mtakatifu * (1 Thesalonike 5:19) na *kumkaribisha roho mchafu * kwamaana *MUNGU HAWEZI KUTENDA KATIKA CHOMBO KICHAFU. *
Tudumu katika maagano yetu kwa unyenyekevu na uthabiti ili Roho wa Mungu APATE *kuimarika na kutenda ndani yetu. *
Basi Ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, TAKATIFU, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana ...(Warumi 12:1)
Tumsifu Yesu Kristo
©️ Professor Innocentus Alhamis