Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Nilitegemea ungekuja kuonesha upotovu kwa yale yanayofanya watu waamini mungu.
 
.
Hapa wewe ndio unamtaja mungu maana unaogopa hata kivuli chake.
Narudia tena kukuuliza swali. Haya maumbile unayoyaona na pia yapo mengi tu usiyoyaona asili yake ni nini?
Lete jibu kwanza ndo tuendelee
 
.
Hapa wewe ndio unamtaja mungu maana unaogopa hata kivuli chake.
Narudia tena kukuuliza swali. Haya maumbile unayoyaona na pia yapo mengi tu usiyoyaona asili yake ni nini?
Lete jibu kwanza ndo tuendelee
Mimi shida yangu kuthibitishiwa Mungu yupo au hayupo.

Nikikwambia sijui jibu la swali lako, wewe unaweza kuthibitisha kwamba Mungu ndiye chanzo?
 
Hiyo akili yako ingewezaje kujua kuwa haya ni mazuri? Utajuaje mwanga bila Giza?
.
Hawezi jibu hili.
Ndo maana nilimuuliza kile anachokiita ni upendo alijua je kua huo ndio upedo, huruma, uwezo, mamlaka nk?
 
Nilitegemea ungekuja kuonesha upotovu kwa yale yanayofanya watu waamini mungu.
Umeelewa hata nilichoandika ni nini?

Unafahamu contradiction ni nini?

Ukisema, Mungu ana uwezo wote, ana ujuzi wote ana upendo wote.

Halafu kaumba ulimwengu ambao njaa, matetemeko ya ardhi, mioto, mafuriko vinaweza kuua mamilioni ya watoto wasio na hatia, kila mwaka, wakati alikuwa na uwezo wakuumba ulimwengu ambayo mabaya hayo yote hayawezekani kufanyika na wala hayajulikani kabisa, habari yako ya kuwepo kwa huyo Mungu inajipinga yenyewe kabla mimi sijaipinga.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya haya kuwepo ni kujipinga yeye mwenyewe.

Mungu huyo hayupo.

Hawezikuwepo.

Kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Ni kama bachelor wa ndoa aliyeoa, au pembetatu duara katika Euclidean geometry.

By definition, pembetatu si duara na bachelor hajaoa, huwezikuwa na bachelor aliyeoa, huwezi kuwa na pembetatu duara.

Ni vitu vinavyojipinga kabla ya kupingwa.
 
Mimi shida yangu kuthibitishiwa Mungu yupo au hayupo.

Nikikwambia sijui jibu la swali lako, wewe unaweza kuthibitisha kwamba Mungu ndiye chanzo?
.
Kutokujua jibu la swali langu hakuondoshi ukweli kwamba maumbile yana asili yake.
Majubu ya swali hili ni mwanzo mzuri wa swali lako la msingi. Kma hujui jibu basi utapewa jibu. Jihadhari kubisha kitu ambacho hujui.
 
Hiyo akili yako ingewezaje kujua kuwa haya ni mazuri? Utajuaje mwanga bila Giza?
Mungu angeshindwa kunifanya nijue mwanga bila giza?

Mbona muda unaenda mbele tu, haurudi nyuma, lakini hilo halinizuii kuujua muda?
 
.
Kutokujua jibu la swali langu hakuondoshi ukweli kwamba maumbile yana asili yake.
Majubu ya swali hili ni mwanzo mzuri wa swali lako la msingi. Kma hujui jibu basi utapewa jibu. Jihadhari kubisha kitu ambacho hujui.
Maumbile yana asili yake, hilo si jambo lenye ubishi.

Lenye ubishi ni, kwa nini asili yake ni lazima iwe Mungu na si kingine chochote?
 
Maumbile yana asili yake, hilo si jambo lenye ubishi.

Lenye ubishi ni, kwa nini asili yake ni lazima iwe Mungu na si kingine chochote?
.
Hivyo basi wewe unasema asili ya maumbile ni nini?
 
.
Hivyo basi wewe unasema asili ya maumbile ni nini?
Mbona nishakujibu hapo juu, unafuatiliamjadala au unauliza tu?

Mbona nishakujibu kwamba sijui,na mimi sipokatika kundila kusema najua kitu ambachosijui, kama sijui natafuta uthibitisho na ushahidi.

Unaweza kuthibitisha asili ya maumbile ni Mungu?
 
Mbona nishakujibu hapo juu, unafuatiliamjadala au unauliza tu?

Mbona nishakujibu kwamba sijui,na mimi sipokatika kundila kusema najua kitu ambachosijui, kama sijui natafuta uthibitisho na ushahidi.

Unaweza kuthibitisha asili ya maumbile ni Mungu?
.
Wewe ndio unayaita "mungu" maana yake kitu cha kuabudiwa.
Mimi sijayaita hivyo.
Kama unakubali maumbile yana asili basi sijali itatajwa je hiyo asili kulingana na mitazamo ya watu. Shauku yangu ni kutaka kusikia kutoka kwako ama ulivyopokea, unaiita je? Usikwepwe swali tafadhali.
 
.
Wewe ndio unayaita "mungu" maana yake kitu cha kuabudiwa.

Nayaita Mungu wapi? Kivipi? Unajuamtu akiuliza hajasemawala kuita?

Mimi sijayaita hivyo.

Hujayaita nini hivyo?

Kama unakubali maumbile yana asili basi sijali itatajwa je hiyo asili kulingana na mitazamo ya watu. Shauku yangu ni kutaka kusikia kutoka kwako ama ulivyopokea, unaiita je? Usikwepwe swali tafadhali.

Nimeshakwambia sijui,utasemajenikikwambia sijui nakwepa swali?

Unataka nikudanganye najua kitu ambacho sijui?

Wewe maumbile chanzo chake ni nini na una uthibitisho gani kwamba ni hicho na ni hicho tu si kingine chochote asilani.
 
mbona mnamsemea sana Yesu ? unaijua ' red letter bible?' maelezo yote hayo lakin yeye Yesu ingetokea akaulizwa hajui hata moja!!!
 
Ndugu yangu usiimbe mafundisho ya kanisa au maneno ya mchungaj/padr wako, sikiliza Yesu mwenyewe anasema nini hapa chini:


Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.

Yohana 12.49-50



Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.

Yohana 5.30



Fakhari kubwa ya Yesu ilikuwa kwamba kila alisemalo na alitendalo ni kufuata mapenzi ya Mungu na kutii maamrisho yake.


Katika hadithi ya muujiza wa kufufuliwa Lazaro tunasoma kama ilivyo katika Injili ya Yohana:

Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.

Yohana 11.38-42

Kutokana na kisa hichi tunajifunza nini? Mambo matatu hapa yanatudhihirikia wazi:

1. Yesu anamwambia Martha, dada wa maiti, kuwa "ataona utukufu wa Mungu" si utukufu wa Yesu, kwani muujiza ni wa Mwenyezi Mungu, si wa Yesu, Mwana wa Adamu. Mfufuaji ni Mwenyezi Mungu, mwenye uwezo wa kila kitu. Yesu "hawezi kufanya neno mwenyewe".

2. Yesu anamwomba Mungu na anamshukuru Mungu kwa kumwitikia na kuyasikia maombi yake.

3. Yeye Yesu anajua kuwa Mungu siku zote anamwitikia maombi yake, lakini alifanya yale hadharani ili athibitishe kwa wale waliohudhuria kuwa kweli yeye Yesu ametumwa na Mungu, yaani yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kamaalivyosema mwenyewe:"ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma." Yesu pia anathibitisha kuwa ayatendayo ni mapenzi na amri ya Mungu.

Hayo ndiyo, lakini yeye mwenyewe Yesu kafufuka kutoka wafu. Huo si muujiza wa kuonyesha kuwa yeye ni Mungu? Hebu tuitazame Biblia inasema nini juu ya tukio hili. Kila tusomapo kitabu hichi kitakatifu tunaona kuwa ni Mungu ndiye aliyemfufua Yesu.


Hatuoni kuwa Yesu kajifufua mwenyewe. Vile vile tunasoma humo humo kuwa si yeye peke yake aliyesimuliwa na kuaminiwa kuwa kafufuliwa kutoka wafu. Twasoma katika 2 Wafalme:4.32-37 vipi Nabii Elisha (Al Yasaa) alivyomfufua mtoto aliyekwisha kufa. Kisa kingine kama hicho kinasimuliwa katika 1 Wafalme 17.22. Biblia pia inawataja watu wengine wasiokuwa Yesu waliopaa wakenda mbinguni. Katika 2 Wafalme tunasoma:



Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili (Elisha na Eliya, yaani Al Yasaa na Ilyas); naye Eliya (Ilyas) akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.

2 Wafalme 2.11



"Kisulisuli" ni upepo wa chamchera au kimbunga. Hadithi kama hizo za watu watukufu kupaa mbinguni na kufufuka zilikuwa zimeenea sana katika zama za Yesu.

Josefas akiandika katika kitabu Antiquities (Ya Kale) anasimulia khabari ya Musa: "Kwa ghafla kiwingu kilisimama mbele yake, naye akapotea katika bonde fulani, ijapokuwa ameandika katika vitabu vitakatifu ya kuwa alikufa. Hayo yalifanywa kwa kuogopa wasije kusema kuwa kwa sababu ya uchamngu wake uliopita kiasi, alikwenda kwa Mwenyezi Mungu." Josefas pia ametaja kuwa baadhi ya watu walifikiri kuwa "Musa ameingizwa katika ungu."


Na J. Jeremias katika Moyses amesema:


"Watatu wamepaa mbinguni nao wahai: Enoko, Musa na Eliya".

Almuradi tunaona kwa uthibitisho wa maandiko matakatifu ya Kikristo kwamba si Yesu peke yake aliyeitwa "Mwana wa Mungu, au Mungu", wala si yeye peke yake aliyefufua wafu, wala si yeye peke yake aliyefufuka na kupaa mbinguni.
 
Rafiki yangu umepewa maandiko ambayo Yesu anasema yeye sio Mungu sasa wewe unampinga Yesu?
 
Mungu tayar alishaumba ulimwengu huo, na wakaz wake walikuwa malaika hakukua na baya maan malaika hawakupewa hiar ya kufanya mabaya , amebadili creation na kuumba wanadamu ambao amewapa hiar ya kufanya mazuri au mabaya, nahuo ndio mtihani ambao mwanadamu akiushinda atapata pepo ya juu kuliko ya malaika na akiushindwa ataingia moton
 
Kwa nini huu ulimwengu unakufanya ufikiri kuwepo kwa aliyeuumba?

Kwa nini ukufanye ufikiri "aliyeuumba" na si "kilichouumba" ?

Na kwa nini aliyeuumba ni lazima awe Mungu tu, na si kingine chochote?
Tuanzie hapa, je unaamini kwamba kuna nguvu za utendaji beyond ubinadamu wetu?
 
Kwa nini Mungu ampe mtihani mtu?

Hajui majibu mpaka kwa msaada wa mtihani?

Kama Mungu anajua kila kitu, mtihani wa kazi gani?
 
Kwa nini Mungu ampe mtihani mtu?

Hajui majibu mpaka kwa msaada wa mtihani?

Kama Mungu anajua kila kitu, mtihani wa kazi gani?
unashangaa Allah kuifanya dunia kama Mtihani? yeye ni mjuzi wa kila kitu na anafanya anachokusudia..siwezi kuhoji uadilifu wake lakini logically mtihan ni kwa sababu kila mtu apate anavyostahili baada ya maisha ya dunia, yule aliyefaulu afuzu kuingia pepon na aliyefel aadhibiwe na kuingia mtoni.

wewe mwenyewe sasa hivi umeanza ku fail exam maana unashindwa hata kitambua uwepo wake.

Jifikirie kama hii Dunia isingekuwa kama mtihan, watu wangefanya kufuru sana kwa sababu mwisho wa siku hakuna wa kusahihisha na kujua nani anastahili sawa na alivyoishi, huwezi kwa mfano kuua watu bila sababu za kisheria hapa dunian halafu uwe sawa na mtu aliyeishi kiungwana!

umepewa hiyar, ukifanya mabaya unafeli mtihani ukifanya mazur unafaulu! Lengo ni kutoa haki ambayo inaweza isipatikan hapa dunian kwenye mahakama zetu kutokana na limitation za kibinaadam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…