Sheikh wangu,,,hayo yote ulioandika sio kwamba siyajui au kuyaelewa ila ndio sababu nilianza kukupa hadhari kwamba wewe kuna mtazamo unauona ni sahihi juu ya Yesu lakini na mimi nina mtazamo wangu dhidi ya Yesu tena ninaouona sahihi mno,,na usioweza kubadilika kama sheria ya mmedi na muajemi,,hata sekunde moja...Wewe umekuwa na imani kwamba Yesu ni nabii Isa jambo ambalo halijawahi,,halitawahi wala halitakaaliwahi kuniingia akilini asilan...Equation ya kumuequate Yesu na Issa haiwezekani hata katika Irreversible reaction.Kamwe....
Unaweza kuwa unayajua lakin hujatafakari, ukitafakari baada ya kusoma utaelewa na haitakuwa ngumu kufuata njia ya ukweli na haki, Yesu mwenyewe anakwambia utafute ukweli sio uegemee tu mafundisho ya sunday school had sasa umekuwa na unaweza kutafakari mwenyewe!!!!!
angalia hapa chini Mwandishi mmoja amechambua hoja yako ya Muujiza wa kuzaliwa Yesu na ambavyo unakufanya umuelewe yesu kama Mungu wako!!!!! katika Biblia na Quran.
KUZALIWA BILA YA BABA
Labda katika miujiza yote ya kumthibitishia Yesu ungu ni kule kuzaliwa kwake na bikra bila ya baba. Wengi wanaona hayo ndiyo yanayoonyesha kwa nguvu zaidi kuwa yeye ni Mungu au Mwana wa Mungu. Mtaalamu mkubwa wa Kikristo, Maurice Wiles, Professor of Divinity and Canon of Christ Church Oxford, na Mwenyekiti wa Tume ya Imani ya Kanisa la Kiingereza, ameeleza vipi ilivyokuwa ni muhimu kabisa kuamini kuzaliwa na bikra kwa mwenye kutaka kuamini kwamba Yesu ni Mungu. Professor Wiles akiandika katika kitabu The Myth of God Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu) amesema:
"Mwanzoni mwa karne hii (ya ishirini) zilipokuwa shaka shaka zinatamkwa kuwa ati ni kweli hakika Yesu alichukuliwa mimba na bikra, maneno hayo ya kuonyesha shaka yalionekana mara nyingi kuwa ni mashambulio khasa juu ya imani ya kuwa Mungu kawa mtu. Ilionekana kwamba imani ya kuzaliwa na bikra na kwamba Mungu amekuwa mtu ni kama pacha wasiobandukana, ama zitasimama pamoja au zianguke pamoja."
Biblia yasemaje juu ya jambo hili? Kwa hakika si kitu cha kawaida mtu kuzaliwa na mwanamke bikra asiyeingiliwa. Ni kweli huo ni muujiza. Lakini ndio ndivyo kuamini kuwa chenye kuzaliwa kwa muujiza ni Mungu? Au hata ndio ndivyo kuona tukio kama hilo ni dalili mojawapo ya kuzidisha ushahidi ya kuwa huyo mtoto ni Mungu au Mwana wa Mungu, kwa maana wanavyotaka wakuu wa makanisa wafwasi wao waamini?
Biblia inayotwambia kuwa Yesu kazaliwa bila ya mama yake kuingiliwa na mwanaadamu (Injili ya Mathayo 1.18) vile vile inatuambia ya kuwa Adamu hakuwa na baba wala mama. (Mwanzo 1.26- 27).
Kama wa Yesu ni muujiza wa Adam ni muujiza mardufu. Hali kadhaalika Paulo amewaandikia Waebrania:
Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Waebrania 7.1-3
Tunaona basi Biblia inatuhakikishia kuwa Yesu hakuwa pekee mwenye kuzaliwa bila ya baba. Wapo waliomtangulia katika muujiza huu. Kama huo ndio ungu, basi wangelikuwa Adam na Melkizedeki wa mbele, ambaye anasimuliwa na Biblia kuwa alikuwa
"hana baba, hana mama, hana mwanzo wala mwisho".
Hoja nyingi zimetolewa kukanya fikra ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aligeuka binaadamu akaishi duniani kwa sura ya Yesu wa Nazareti. Hoja hizo ziko za misahafuni mpaka za kisayansi. Katika Qur'ani ameshabihishwa Yesu na Adam.
Hali kadhaalika muujiza ulitokea kabla kidogo tu ya kuzaliwa Yesu, alipochukua mimba Elizabeti, mke wa Zakaria na ilhali huyo mama ni tasa tangu ujana wake na hapo kesha zeeka na kapindukia miaka ya kuzaa. Mumewe, naye, Zakaria alikuwa ni mkongwe.
Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'ani, Sura ya Al Imran:
Akasema Zakaria: Mola wangu! Vipi nitapata mtoto, na hali ukongwe umesha nifika, na mke wangu ni tasa? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.
(Qur'ani) Al Imran 3.40
Ilipofika zamu ya Maryam kuchukua mimba Qur'ani inasema:
(Maryam) akasema: Mola Mlezi wangu! Vipi nitampata mtoto na hali hajanigusa mwanaadamu ye yote? (Mwenyezi Mungu) akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho; anapohukumu jambo, huliambia: Kuwa! Basi likawa.
(Qur'ani) Al Imran 3.47
Hizi ni hoja za misahafu, ni hoja za watu wenye imani. Wapo wengineo ambao wamepuuzilia mbali hadithi yote hiyo ya kuwa Maryam kachukua mimba bila ya kuingiliwa na mtu. Hao ni kama Mayahudi ambao wanamtukana Yesu na mama yake kwa kusema kuwa hiyo ni mimba ya haramu. Miongoni ya wataalamu wa Kizungu wenye asli ya Ukristo wapo wanaoamini hayo. Wanasema kuwa imani ya kuzaliwa na mama bikra ilikuwako tangu zamani katika dini za kipagani (kishirikina) kabla ya kuja Yesu. Bikra Rea Silvia alimzaa Romulus wa Roma. Horus wa Misri alizaliwa na Isis, malkia bikra wa mbinguni.
Hoja inayotolewa kama ilivyokuwa hizi na nyenginezo ni hadithi za kubuni tu zilioenea pande za Bahari ya Kati, basi ndio hivyo hivyo hadithi ya kuwa Maryam alikuwa bikra alipochukua mimba na kumzaa Yesu ni hadithi ya kubuni kuiga zile zilizotangulia.
Mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri anawashutumu wakuu wa Kanisa kwa kutafuta kila kipengee katika Biblia kutoa ushahidi kuwa kuzaliwa kwa Yesu na bikra kuliaguliwa mbele.
Kipande kinachonukuliwa mno ni kile kiliomo katika Isaya ambacho kinasema:
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Isaya 7.14
Mtaalamu huyu anasema maneno haya hayakukhusu kuzaliwa kwa Yesu hata chembe. Kwanza neno la asli halikutaja "bikira" lakini ni "mwanamke kijana". Tafsiri nyingine kama Revised Standard Version zimefuata hivyo ilivyo asli. Neno la Kiebrania liliotumiwa ni almah ambalo maana yake ni mwanamke kijana au msichana. Neno bikra kwa Kiebrania ni bethulah, kama ilivyo katika Kiarabu batuul. Na haya mambo ambayo yametokea zaidi ya miaka 700 kabla ya Yesu yalikhusiana na mke wake Isaya ambaye alikuwa umri wake ni miaka 20 wakati ule na kweli akaja kumzaa mtoto mwanamume. Ama hilo neno Imanueli, maana yake ni Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi, na wala sio maana yake kuwa huyo mtoto kuwa ndiye Mungu. Lugha ya Kiebrania imekaribiana na Kiarabu, na kwa Kiarabu ni Ma'anallah, nalo ni jina la kawaida, na kama kwamba kumwombea kheri huyo mwenye kuitwa. Mtaalamu Isaac Asimov ameeleza wazi juu ya utabiri huu wa Isaya katika kitabu chake, Asimov's Guide to the Bible.
Mtaalamu mwengine mwenye kupima mambo kiakili aitwaye G. Vermes amesema katika kitabu chake Jesus the Jew(Yesu Myahudi) akidai kuwa hili neno "bikira" hata lilivyotumiwa kwa Mariamu yawezekana sana kuwa maana yake ni kuwa mdogo mno kwa uzazi, kama walivyokuwa Sara, Hanna na Elizabeti kuwa ni wakongwe mno, au tasa.
Mwishoe kuna maoni ya mwana-sayansi na daktari juu ya hili suala la kushika mimba mwanamke hali naye ni bikra. Dr. T.H. Van de Velde M.D. akiandika katika kitabu chake cha kitaalamu, Ideal Marriage (Ndoa Bora) anasema:
"Mara nyingi imewahi kutokea, ijapokuwa ni nadra, kushika mimba kwa kupenya mbegu ya uzazi katika utupu wa mwanamke bila ya kuingiza kabisa dhakari, au utupu wa mwanamume. Mifano kama hiyo ni muhimu kabisa kimaisha. Ni dhaahiri kuwa inathibitisha vitu viwili. Kwanza, kuwa katika hali maalumu yawezekana mimba kutiwa ijapokuwa kizinda hakikupasuliwa. Na pili ya kwamba mbegu ya uzazi yaweza kufika ndani ya utupu wa mwanamke kwa njia isiyokuwa moja kwa moja, kwa mfano kwa mguso wa kidole..."
Hapana shaka pana utaalamu mkubwa katika mawazo na fikra hizi, za kidaktari, za kisayansi au za kiakili; lakini ni Qur'ani ndiyo inauweleza ukweli kwa maneno mepesi kabisa hata watoto wachanga wakaweza kuelewa na ikawa ya kuwatukuza Yesu na mama yake:
Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa mchanga kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. Hii ni kweli inayotoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka.
(Qur'ani) Al Imran 3.59-60