*JE, YESU NI MWANA WA MUNGU?*♂
Hilo☝ ni swali ambalo linawasumbua watu wengi sana hasa wale wenye imani tofauti na ya Kikristo. Wamekuwa wakipata shida sana katika kulielewa hili jambo lakini kwa neema ya Mungu leo wote wanaenda kupata majibu ya swali hili tena ni jibu thabiti kibiblia. Ndugu zangu Mungu wetu wa mbinguni ndiye muumba wa mbingu na nchi na kila kilichomo.
Kutokana na baadhi ya imani zingine wanaamini kuwa Mungu hawezi kuzaa na hawezi kuwa na mke katika hili jambo, watu wameshindwa kuelewa uzazi unaozungumziwa katika Biblia na wakati imani zao wanaamini ya kwamba Mungu ameumba viumbe vyote.
Tatizo linaloonekana hapa ni uzazi tu na sio kitu kingine kwa sababu wamekuwa wakiuliza, *kwanini Mungu azae?*
Kwa habari ya kuzaa, *Je! Mungu anazaa au hazai?*♂
Kwanza tuangalie kuna aina ngapi za uzazi. Yohana 3:6 inasema *“kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho”* kutokana na aya hii tunagundua ya kwamba kuna aina mbili za uzazi, nazo ni uzazi wa kimwili na uzazi wa kiroho.
Na Biblia inasema kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho, hivyo Wakristo wanaposema YESU ni mwana wa Mungu wanamaana ni mwana wa Mungu Kiroho na sio uzazi wa kimwili kama ambavyo mimi na wewe tumezaliwa kutoka kwa wazazi wetu.
Mfano wa uzazi wa Kiroho Yakobo 1:18 inasema, *“kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake”*.
Ukisikia Mungu ana wana basi usifikirie kwamba ana mke, hapana yeye anatuzaa sisi kwa Roho.
*Je, kutokana na Biblia wazo la YESU kuitwa mwana wa Mungu linatokana na nini?*♂
Biblia katika kitabu cha Luka 1:34-35 inasema, *“Mariamu akamwambia Malaika, litakuwaje neno hili maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli, kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu"*
Biblia ipo wazi sana hivyo imethibitisha kwamba YESU ni Mwana wa Mungu kiroho.
Na katika maandiko ya Biblia takatifu YESU mwenyewe anakili ya kwamba ni Mwana wa Mungu. Katika kitabu cha Yohana 9:35-38 Biblia inasema hivi, " *Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia. Kwa kinywa chake YESU KRISTO anashuhudia ya kwamba yeye ni Mwana wa Mungu aliye hai"*
Natumaini rafiki zangu mumeelewa dhana nzima ya YESU KRISTO kuitwa Mwana wa Mungu na wakristo katika ulimwengu wote.
NB:-Nadhani kwenye maelezo yangu hapo juu NIMEFAFANUA kila kitu, YESU ni mwana wa MUNGU, kuna msemo mtoto wa nyoka naye ni nyoka, kwahiyo mwana wa MUNGU naye ni MUNGU
NOTE"Tito 2:13 . tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Imeandaliwa na Mwinjilisti Danny Ayubu,,
kwa mafundisho zaidi wasiliana nami kwa,,0627285492
Ufunuo 22:21
. Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.