Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Hivi uliwahi kuelewa nia ya Yesu kwenye kitabu cha Yohana 8:1-24 kwa nini Yesu hakuitimiza sheria ya torati kama ilivyotakiwa kwa Huyo mwanamke?

Roman 7:1-25 na Roman 8:1-27 Hapa utapata picha nzima ya nilichokieleza hapo juu na utaelewa kwa undani kwa nini Wakristo hawaishi kwenye sheria tena, kama walioshi Wakati wa sheria kabla ya Yesu.
 
Kuhusu Paulo Acts 9:15 ni mstari unaokupa picha kwamba Paulo alichaguliwa Miongoni mwa wengi. Hakutenda chochote kwa ajili ya sifa kwake ila kwa faida ya aliemtuma ambae naamini hata wewe unamjua ni Yesu.
 
Ni aghalabu sana kiongoz wa kiimani kuruhusu waumini na wasio waumini kuuliza maswali baada ya mada. Pengine utamaduni wa kuuliza maswali magumu ungekuwa ni Lazima, tusingeshuhudia utitiri wa madhehebu duniani, mengi yakiwa kwa maslahi ya viongozi wao.

Ni kiongoz mmoja tu (anayefahamika kwa sasa duniani) ambae ameenda mbali zaidi na kuruhusu maswali hata nje ya mada alizozungumzia na amekuwa akijibu kwa ufasaha na kutoa hata marejeo. Huyo Si mwingine bali ni Dr. Zakir Naik. katika video hii amejibu kuhusu kifo, kukata roho, roho ni nini na inaenda wapi baada ya kifo?


Tusidanganyane hata kidogo, Kama roho haionekani utajuaje habari zake na utajuaje kama hurudi kwa Mungu? Roho ni imani tu na watu wanaamini kwa sababu ya imani tu. Hakuna binadamu ambae anaweza kuthibitisha uwepo wa roho hata awe na uwezo na akili zilizopitiliza.

Roho ni sawa na mapepo, yanavuma katika imani na akili za watu lakini hakuna binadamu hata mmoja anaeweza kukiri kumwona pepo hata kwa msaada wa darubini ya ki- electronic.
 
7 Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.


Torati 14:

Ukiongelea nguruwe kuwa ni najisi usije ukasahau kwamba na ngamia pia ni najisi.......

Zaidi huyu Mungu angekuwa ni mmoja kwa muslimu na Christian asingejichanganya namna hii......

Sisi hata ngamia twala hatufungwi....ila wengi wamempenda Pork maana nyama yake ni nzuri sijui ina viwatilifu gani.....
 
Matayo 5:17-48 ndio unapata picha halisi ya jinsi anavyoitimiliza torati na haina tofauti na kilichoandikwa kwenye Roman7 na Roman 8.

YESU Anasema badala ya kuzini hata kutamani tu mwanamke ni zinaa, anaangalia zaidi chanzo cha zinaa. Hakuna kumwacha mke zaidi amezini tu, mtu akikupiga shavu moja geuza na la pili(hakuna jino kwa jino tena as per sheria) kwa hio mwanamke akizini ni ndoa inavunjika tu sio kumpiga mawe hadi afe. Kwa hio Yesu ameeleza vizuri namna ya kuitimiliza torati in modern way na anaeleweka vizuri.

Na ukimsoma vizuri utaona hakuna alipotofautiana na mitume wake.
 
Hivi uliwahi kuelewa nia ya Yesu kwenye kitabu cha Yohana 8:1-24 kwa nini Yesu hakuitimiza sheria ya torati kama ilivyotakiwa kwa Huyo mwanamke?????


Roman 7:1-25 na Roman 8:1-27 Hapa utapata picha nzima ya nilichokieleza hapo juu na utaelewa kwa undani kwa nini Wakristo hawaishi kwenye sheria tena,,kama walioshi Wakati wa sheria kabla ya Yesu.
Mat. 5 ipo waz, ipi inaipinga? Vifungu hivyo ulivyotoa havijaipinga concept nzima iliyopo, bado huwez na hutaweza kupinga kuwa Yesu amekuja kutimiliza Taurat kwa sababu ni maandiko ya biblia ambayo unajinasibu unaiamini.
 
7 Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.


Torati 14:

Ukiongelea nguruwe kuwa ni najisi usije ukasahau kwamba na ngamia pia ni najisi.......

Zaidi huyu Mungu angekuwa ni mmoja kwa muslimu na Christian asingejichanganya namna hii......

Sisi hata ngamia twala hatufungwi....ila wengi wamempenda Pork maana nyama yake ni nzuri sijui ina viwatilifu gani.....
Hakuna mahala katika Quran ngamia kakatazwa, kumbuka katika uislam tunaamini Quran na sio biblia, ila tunawakumbusha kwamba katika kitabu mnachokiamin mbona hamkifuati?

Tulipokichambua kitabu chenu tukaona kuwa kumbe na nyinyi kwa asilimia kubwa mmefundishwa Uislam na hicho kitabu chenu wenyewe, kwa hiyo mkikifata kikamilifu mtagundua yafuatayo ambayo yapo wazi:
I. Hakuna Mungu apasae kuabudiwa isipokuwa Allah

2. Mtume Muhammad ni mjumbe wa M'nyez Mungu na ni ukomo wa Manabii.

Hayo mawili yaliyopo kwenye biblia yenu mkiyaamin
mnatakiwa muwe Waislam
Ila kwa sababu hamuifat biblia yenu kikamilifu, mnaendelea kujipotosha
 
7 Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.


Torati 14:

Ukiongelea nguruwe kuwa ni najisi usije ukasahau kwamba na ngamia pia ni najisi.......

Zaidi huyu Mungu angekuwa ni mmoja kwa muslimu na Christian asingejichanganya namna hii......

Sisi hata ngamia twala hatufungwi....ila wengi wamempenda Pork maana nyama yake ni nzuri sijui ina viwatilifu gani.....
Hatuwezi kuifata biblia yote kwa sababu yapo mambo mengine yaliyoandikwa humo hayana hadhi ya kuwa katika neno la Mungu, ni dhahir wanadam wameandika humo, ndio mn kuna hitilafu nying sana katika biblia, ambazo zinaashiria kuwa maneno yake hayawez 'as a whole' kutoka kwa Mungu
 
MTUME KWA WAISRAILI

10- MTUME KWA WAISRAILI

Tumekwisha ona kutokana na maneno ya Injili na maandiko mengine ya Agano Jipya tuliyoyanukulu kwamba Yesu ametumwa na Mwenyezi Mungu. Ametumwa awendee nani? Hebu tuiache Biblia itueleze:



Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akisema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani za bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.

Mathayo 15.21-28



Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina. Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu: Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa." Ikiwa ipo shaka yo yote katika akili ya mtu kuwa maana ya maneno hayo ni kuwa Yesu anasema kuwa hakutumwa kwa kabila nyengine zo zote ila Waisiraili tu na atazame mwenye shaka tafsiri kubwa kabisa ya Wakristo inayoeleza maana wazi maneno ya Biblia, The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi: "Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:



Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.

Mathayo 7.6



Mbwa na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili. Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi. Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu. Kama asemavyo Isaac Asimov katika kitabu chake Guide to the Bible (Uwongozi kwa Biblia):

"Suala liliopo ni nani hao mbwa na nguruwe wnaokusudiwa katika mstari huu? Yaweza kuwa maana ya mstari huu ni kuwa haifai kufunza ukweli wa dini kwa wale wasiotubu katika kejeli zao, au wale waliozama katika madhambi, lakini hayo hayaelekei kabisa. Basi mtu amfundishe nani? Wale waliokwisha amini? Yesu mwenyewe anakanya hayo, kwani aliposhutumiwa kuwa anachanganyika na wenye dhambi ananukuliwa kusema: Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.

Mathayo 9.12



"Upande mwengine, huku kutaja mbwa na nguruwe huweza kuwa ni maneno aliyoyachagua Mathayo kulipa nguvu wazolake kuwa isifanywe juhudi kubwa kueneza mafunzo ya Yesu miongoni mwa Mataifa mengine. Labda ni nadhari ya Mathayo kuwa ipo khatari kubwa ya hayo Mataifa kuudhika na juhudi za kutaka kuwatanasarisha na kwa hivyo wakawatesa Wakristo; itakuwa ndio 'watageuka na kuwararua'.Na hayo kwa hakika waliwahi kuyafanya. Yaweza kuwa aliona kuwa yale Mataifa yaliyoukubali Ukristo bila ya kuijua Sharia ya Musa yangeweza kuyavuruga mafunzo ya Yesu: 'na kuyakanyaga chini ya miguu yao.'"


Na juu ya kauli ya Yesu : "Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa," Asimov anasema:

"Hapa Mathayo kwa uwazi anatuletea Yesu ambaye kazi yake ni ndani ya mipaka ya uwananchi wa Kiyahudi tu."


Tukiendelea na isemavyo Biblia juu ya ujumbe wa Yesu tunapata ushahidi zaidi kutokana na Injili ya Mathayo:



Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Mathayo 10.5-6



Hao Thenashara ni wanafunzi wake kumi na mbili aliowateua mwenyewe Yesu kutangaza mafunzo yake. Hapo anawapa amri zilizo wazi kuwa wasiwaendee watu wa Mataifa, yaani wasiokuwa Waisraili. Hao wanafunzi kumi na mbili ndio wanaoitwa katika Biblia "mitume" kwa kuwa walitumwa na Yesu. Na wao kama yeye mwenyewe hawakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa Israel" kwani "si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."


Kwa nini Yesu alisema maneno kama haya ya kukataa na kukataza kuwafunza dini ila Waisraili tu? Kwa nini alitumia mifano mibaya kama hivyo "mbwa" na "nguruwe" kwa kuwakusudia hao watu wengine wasio Mayahudi, yaani ndio mimi na wewe mwenzangu? Wataalamu wa Kikristo na wasio Wakristo wamestaajabishwa na maneno hayo. Ni maneno machache katika aliyoyasema Yesu ambayo yamewatatiza wasomaji Wakristo kuliko maneno haya. Wapo wanaoona kuwa Yesu alitumia matusi yale kuwaita wote wasio Mayahudi kufuata mwenendo wa Kiyahudi, yaani ndio hivyo Mayahudi wawaonavyo binaadamu wote wasio kuwa wao. Na wapo wasemao kuwa Yesu akipenda kufunza kwa mifano, na hivyo anafananisha kama kwamba yeye anaamini hiyo imani mbovu ya Kiyahudi ya kudharau watu wasiokuwa kabila yao. Na wapo wengine kama Asimov ambao wanaona maneno yale ni ya Mathayo, na yeye Mathayo (au ye yote yule aliyeandika Injili hiyo) kamuambatisha nayo Yesu maneno hayo, kwa kuwa yeye mwandishi alikuwa Mkristo wa kabila la Kiyahudi na anacho kiburi cha Kiyahudi.


Ama kusema kuwa hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa Israeli inaonekana kama kilivyosema kitabu cha The Interpreter's Bible kuwa Yesu hakika kwanza aliamini kuwa alitumwa kwa Waisraili tu. Ni jambo la kustaajabisha kuwa Mungu au Mwana wa Mungu aje duniani atumwe na kwanza asiujue utumwa wake ila aamini tu kuwa katumwa kwa watu wake wa Kiyahudi basi. Na kama yeye ni Mungu au Mwana wa Mungu, katumwa na nani? Kama katumwa na Mungu, basi yeye si Mungu. Si hilo tu, bali hata akiwa ni Nabii na Mtume wa Mungu tunamtaraji aujue tangu mwanzo huo ujumbe wake aliokuja nao, asiwe kutapatapa, kupapasa, na kuhangaika katika jambo la msingi.


Hapana haja ya kuyatafutia tafsiri hii na maana hii, hayo maneno yaliyo wazi ya Yesu Kristo. Yesu hakika hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Yesu hakika kawakataza "mitume" wake wasende kuwahubiria mataifa mengine. Yesu ni kweli kaonya kuwa kuwafundisha mafunzo yake hayo mataifa mengine ni sawa sawa na kuwapa mbwa kilicho kitakatifu, na kuwatupia lulu nguruwe. Kwa nini ikawa hivi? Ikiwa Yesu kweli katumwa na Mungu, kwa nini ujumbe wake uwekewe mipaka kwa jamaa zake tu wa Kiisraili, na yeye asikiuke mipaka ile? Naam, zipo sababu zenye nguvu kwa hayo.


Kwa hakika hayo hayakuwa mageni, wala Yesu hakuwa Mtume wa mwanzo kutumwa hivyo na Mwenyezi Mungu. Mitume wote waliokwisha kuja kabla yake walikuwa ni Mitume wa vikundi vyao tu, na zama zao tu, na walikuja na mafunzo yao maalumu machache. Musa alikuwa hivyo, na Yesu hali kadhaalika. Hali yake hali ya wenziwe, ila yeye alikuwa ndiye Mtume wa mwisho katika Mitume waliotumwa kwa kabila maalumu. Kwa nini Mwenyezi Mungu akafanya hivyo?


Kwa nini Yesu alikatazwa, mathalan, asiwahubirie yeye wala wafwasi wake, Waafrika, au Wazungu, au Wahindi, au Machina, au Waarabu? Amekatazwa kwa sababu kabila zote hizo zilikuwa hata hazijachukua khatua ya mwanzo ya kuamini Mungu Mmoja. Kabila hizo na mataifa hayo yalikuwa makafiri ama wa kuabudu masanamu, au kuabudu mapango au miti au viumbe vyengine au kuabudu wanaadamu wenzao.



Na ujumbe wake Yesu ni kutengeneza mwenendo, tabia ya watu ambao tangu hapo wanayo imani ya Mungu mmoja. Yeye hakuwa na uwezo wala muda wa kujenga tangu chini. Yeye kazaliwa katika umma wenye kuamini Mungu Mmoja, umma wenye sharia ya Mwenyezi Mungu. Kazi yake kwa muda mchache alioishi na kuhubiri ni kiasi ya kuwapiga msasa tu Mayahudi ambao walikwisha tahiriwa, wanajua cha halali na haramu, na muhimu kabisa wanamjua Mwenyezi Mungu Mmoja, asiyezaa wala kuzaliwa. Ila yao Mayahudi ni kutokuwa na huruma, na kuifanya dini sharia tu isiyo na roho na imani. Mayahudi waliishika sharia ya Musa kwa dhaahiri yake, lakini waliutupilia mbali uchamngu wa Ibrahimu, wakashika ya kuonekana na watu, na wakatupa ya ndani anayoyaona Mwenyezi Mungu na dhamiri zao. Walipoacha "mitume" wa Yesu amri hiyo ya Mungu ya kutowendea makafiri wasiomjua Mungu wala msingi wa sharia, ndipo mafunzo ya Yesu yalipochafuka.



Kwani hao makafiri walipoingia katika Ukristo walijigeuza jina tu, lakini waliingiza karibu yao yote ya kikafiri katika dini ya Yesu, ikaitwa Ukristo, na hali sio Ukristo kabisa aliyoufundisha Yesu. Mahekalu yao ya kipagani yakageuzwa makanisa, na mizimu na mapango yao yakawa ndio monastari za Kikristo. Lau kuwa Wana wa Israili wangeli mwitikia Yesu, basi Ukristo usingelichafuka kama ulivyo chafuka.


Upton Sinclair akiandika juu ya wakati ilipoingia Dola ya Kirumi katika Ukristo na ikaufanya ndio dini rasmi ya taifa, amesema kwa masikitiko: "Ulikuwa ni ushindi kwa Kanisa, na kwa mwenyewe mwenye kuanzisha (yaani Yesu) ni kushindwa kwa muda. Maana yake ni kuwa maadui zake wamelichukua jina lake, mafunzo yake, na nguvu zake."


Yesu alionya, lakini Paulo hakusikia:



"Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na wakawararua."


Yaliyosemwa yamekuwa. Kwa kitendo cha Paulo kuwaingiza mapagani wa Kizungu katika dini ya Yesu sharia ya Mwenyezi Mungu ikaambiwa ni laana, ikatolewa ruhusa kula nyamafu, nguruwe na damu, na kila kiuzwacho sokoni bila ya kutia wasiwasi wo wote katika dhamiri. Tohara aliyoamrishwa Ibrahimu na Mwenyezi Mungu na Manabii wote wakaifuata mpaka mwenyewe Yesu na wanafunzi wake, Paulo aliipuuza kuwaridhi makafiri. Imani za kipagani za mungu mwana na utatu zilizoenea katika mila za Mithra, Osiris, Attis n.k. zikaingizwa katika dini ya Kikristo.


Katika ufalme wa mbinguni Yesu ana yakini kuwa hatokuwa nao ila wana wa Israili tu. Injili ya Mathayo inasema:

Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

Mathayo 19.28



Hata katika maombi yake inaonyesha kuwa Yesu alikuwa anajua mipaka yake na uwezo wake. Madai ya kuwa yeye ni mwombezi, mbali kuwa ni mwokozi, wa ulimwengu mzima ni kumsingizia jambo ambalo mwenyewe hakulidhania. Kumpa mtu cheo asichokuwa nacho ni kumtukana, ni kumvika kilemba cha ukoka, kama Mayahudi walivyotaka kumkejeli kwa kumvika taji la miba. Cheo alicho nacho kwa hakika si kidogo. Kuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Mitume na Manabii watukufu ni jambo kuu kweli kweli. Kuwa mtumishi wa Mwenyezi Mungu mwenye kupendeza si utukufu mdogo. Na Yesu alitafakhari nao, na alitafakhari kuwa yeye hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa Ki-Israili. Na hayo si kwa upungufu wo wote kwa upande wake, ila ni kuutumikia ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kuulinda usiharibiwe na washirikina mpaka ufike wakati wa kuja huyo atayekuwa kazi yake ni kuitangazia risala ya Mungu kwa ulimwengu mzima.


Katika Injili ya Yohana ananukuliwa Yesu kusema:



Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa.

Yohana 17.9



Tukiyachungua vilivyo maneno ya Yesu kama yalivyosimuliwa na Mathayo na Marko ya kuwa yeye alitumwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israili, na maamrisho yake yalio wazi kuwapa "mitume" wake wasende kwenye mataifa mengine isipokuwa Mayahudi tu, na kuwa yeye na wanafunzi wake kumi na mbili watakaa katika viti vyao vya utukufu wakizihukumu kabila kumi na mbili za Israili katika ulimwengu mpya wa mbinguni, hatuwezi ila kuhukumu kuwa hao watu anaowaombea Yesu ni hao hao waliokwisha tajwa kabla, yaani wana wa Israili, sio ulimwengu, sio mimi na wewe. Mimi na wewe si Wana wa Israili. Mimi na wewe ni mataifa mengine. Mimi na wewe na ulimwengu, usiokuwa wa Kiyahudi, Yesu kesha sema hatuombei, ikiwa tutakubali maneno yaliyoandikwa katika Injili zote.


Ni jambo linalojuulikana katika historia - na hata ukisoma katika Biblia kitabu cha Matendo ya Mitume utaona - ya kuwa Ukristo kwanza haukuhubiriwa kwa mataifa mengine mpaka alipoingia Paulo. Na yeye alipingwa vikali sana kwa kutoa shauri hiyo na wanafunzi wake Yesu waliomwona na wakawa naye siku zote na wakajifunza vilivyo mafunzo yake na makatazo yake ya kwenda kuwahubiria watu ambao bado ni makafiri. Dr. Marcello Craveri anaandika katika kitabu chake The Life of Jesus:

"Na hapo Paulo akaingia uwanjani. Kwa heba yake ya kitisho na tamaa yake, hakupoteza wakati ila alijifanya kuwa ni mmoja miongoni mwa 'nguzo' za kikundi kile, kama mwenyewe alivyokuwa kwa kejeli akiwaita Yakobo na Petro. Ukazuka ugomvi na ushindani baina yao na Paulo, na khasa katika shauri ovu la huyu Mkristo mpya kutaka kuivusha dini mipaka ya Uyahudi."


Mtaalamu wa Biblia, Dr. Hugh Schonfield, katika kitabu chake, Those Incredible Christians, (Wale Wakristo wa Ajabu) ameandika juu ya Paulo na ugomvi wake na wafuasi wa kweli wa asli wa Yesu hivi:



"Saulo wa leo, aliyetumia jina la Kirumi la Paulo, alionekana kama ni adui aliyepandwa na shetani wa Daudi mpya. Hatimaye alipokuwa mfungwa wa Warumi, hapana Mkristo aliyenyanyua hata udole kumsaidia, la Wakristo wa Yerusalemu wala wa Roma. Juhudi zake Paulo zote, hata kule kukusanya michango kuwasaidia watakatifu masikini wa Yuda, hazikupunguza upinzani dhidi yake. Wale walioshika kani miongoni mwa wana-kanisa la halali walimwona Paulo kuwa ni mtu wa khatari na mharibifu aliyeazimia kupata wafuasi wengi katika Mataifa yasiyokuwa Mayahudi ili apate ushindi wa idadi kuweza kuwapinga Wazee walioko Yerusalemu. Paulo alikuwa ni adui tangu mwanzo, na kwa sababu alishindwa katika ule uadui wake wa wazi, alijipenyeza kwa hila katika kikundi ili aweze kukibomoa kwa ndani. Hili aliweza kulifanya kwa kuitenga Torati takatifu na kumuingiza katika dini ye yote anayetaka kumfuata kwa kutamka tu imani. Ingelifaa asingekubaliwa kabisa mtu huyu; lakini walikuwapo watu ambao hawakujua wala hawakuwa na shaka naye kwa hivyo hawakutambua nini khasa makusudio yake. Na tazama basi ile imani yao imefikisha wapi hali ya mambo! Unasara wote, juhudi ya Masihi mwenyewe ikaingia katika khatari ya kudharauliwa kabisa katika Israili. Kwa sababu Paulu ni mmoja katika wasemaji wao wakubwa, na yeye alikuwa akitangaza kuwa Torati ni baatili, haifai tena kwa uwokofu, ikawa inaaminiwa na Mayahudi wachamngu kuwa wafuasi wa Yesu ni makafiri wa mwisho."


Busara ya Mwenyezi Mungu kukataza mafunzo ya Yesu yasikiuke mipaka ya Israili ni kuwa isije dini ya haki ikaharibiwa na ushirikina wa makafiri ulioenea pande zote katika zama zile. Ulimwengu ulikuwa bado haujawa tayari kupokea ujumbe wa ulimwengu mzima, na huyo mwenye kuweza kubeba ujumbe ule hajazaliwa, na umma wa kutimiza jambo hilo na kulieneza bado haujapikika ukawa tayari. Yaliyotokea tumeyaona. Ukristo tuuonao na ulioenea ulimwenguni sio Ukristo aliofundisha Yesu. Wa Yesu ulitoweka na mwenyewe na wafuasi wake wa mwanzo wa kabila la Kiyahudi. Paulo kaufuja Ukristo.


Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya Mathayo 28.19-20, Injili ya Luka 24.46-49 na Marko 16.15. Mathayo inasema:



Basi, enendeni, mkwafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Mathayo 28.19-20



Luka anatwambia:

(Yesu) akwaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, naweletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kueni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

Luka 24.46-49



Na Injili ya Marko inasema:

(Yesu) akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Marko 16.15


Je, imekuwaje? Yesu ni kigeugeu? Mbona huku anawakataza wanafunzi wake wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima. La, Yesu si mbabaishi, wala si kigeugeu. Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote wafunzwe dini.


Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya "kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu.

Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko. Hizo nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya Marko. Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asli, bali yaliongezwa baadae.

Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.


William Neil akiandika katika tafsiri ya Biblia iitwayo Harper's Bible Commentary anasema:

"Kama lipo jambo lolote katika uchunguzi wa Injili ambalo juu yake wataalamu wamekubaliana, ni kuwa kufika hapa (yaani Marko 16.8) Injili ya Marko inakoma. Sehemu iliyobaki ya sura (yaani 16.9-20) ndio hiyo iitwayo "Kimalizio kirefu" cha Injili. Kimalizio hicho hakionekani katika nakla za miswada ya zamani, na ambacho ni nyongeza iliyopachikwa katika karne ya pili kutokana na maongezo ya Mathayo, Luka na Matendo...ushahidi wa kale kabisa ulioandikwa juu ya Kufufuka (Yesu) haumo katika Injili bali katika barua ya kwanza ya Paulo kuwapelekea Wakorintho 15.3-8."


Maneno hayo ya Paulo aliyowaandikia Wakorintho na ndio mara ya kwanza kutajwa kufufuka kwa Yesu ni haya:

Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maaandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; badaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

1 Wakorintho 15.3-8



Ikiwa kipande chote tangu mstari 9 mpaka mstari 20 katika sura 16 ya Injili ya Marko, kimepachikwa, basi kisa chote cha kufufuka Yesu kimebuniwa. Mwenye kubuni kisa hichi ni Mtakatifu Paulo. Hivyo ndivyo tunavyoweza kuagua kutokana na kuisoma Biblia, kwani maandishi ya kwanza hayamo katika Injili bali yamo katika barua ya Paulo kwa Wakorintho.


Amesema Craveri katika Maisha ya Yesu:



"Paulo alijihakikishia mwenyewe kuwa ijapokuwa Yesu ni kweli alikufa, lazima awe amefufuka, akiuwacha mwili wake wa kidunia nyuma ili avae mwili wa 'kiroho'...Paulo alichanganya mawazo yake mwenyewe ya kikafiri kafiri ya Yesu kuwa na maisha mapya kwamba ni malipo yake kwa mema yake, pamoja na imani ya Kiyahudi ya kuwajibika mapatano na Yehova (Mungu) na agano la pili. Kwa hivyo Paulo akafunza kuwa ndiyo haya khasa yaliyokuwa ni kazi ya Yesu, na hicho ndicho cheo chake machoni mwa Mungu: kafara ya nafsi yake kwa utakatifu wake na kutokuwa na dhambi kwake ili afutie kwa pamoja makosa ya wote."


Ikiwa basi msingi wa hadithi nzima ya kufufuka Yesu hadi ya ubora wake ni kuwa ni ya shaka shaka - licha ya kuwa ni wazi kuwa ni ya uwongo - hapana njia ya kuamini ya Kuwa Yesu wakati wo wote katika historia aliwahi kuamrisha watu "Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu," kwa sababu haya hakuyasema ila baada ya huko kunakoambiwa ni kufufuka.


Katika Biblia ya Kiswahili iliyo mbele yangu iliyotangazwa na The British and Foreign Bible Society 1950 kifungu cha Marko 16 tangu mstari wa 9 mpaka mwisho yaani mstari wa 20 kimetiwa katika mipinde miwili hivi ( ) kuonyesha kuwa maneno hayo hayakuwamo katika maandiko ya asli. Ilivyokuwa imethibitika kuwa hayo ya Marko si madhubuti, basi yaliyonukuliwa na Mathayo na Luka juu ya mambo hayo ya kufufuka, na kuamrisha kwenda kuhubiria watu wa ulimwengu, na kuutaja Utatu, yote hayo ni baatili.


Kwa mukhtasari tunaona kuwa Biblia inashuhudia kuwa Yesu alikuwa ni Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu kwa Waisraili waliopotea njia. Hadithi ya kuwa aliamrisha mafunzo yake yakatangazwe kwa watu wote "kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu" imebuniwa na kuongezwa mwishoni mwa Injili tatu za Mathayo, Marko na Luka. Kadhaalika kuwa Yesu alifufuka kutoka wafu kwa njia ya kimiujiza imeongezwa, na kauli ya Utatu basi ya kuwa mafunzo yakatangazwe "kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu" pia nayo imebuniwa na wala haina asli yo yote ya kweli.
 
Hakuna mahala katika Quran ngamia kakatazwa, kumbuka katika uislam tunaamini Quran na sio biblia, ila tunawakumbusha kwamba katika kitabu mnachokiamin mbona hamkifuati? Tulipokichambua kitabu chenu tukaona kuwa kumbe na nyinyi kwa asilimia kubwa mmefundishwa Uislam na hicho kitabu chenu wenyewe, kwa hiyo mkikifata kikamilifu mtagundua yafuatayo ambayo yapo wazi:
I. Hakuna Mungu apasae kuabudiwa isipokuwa Allah

2. Mtume Muhammad ni mjumbe wa M'nyez Mungu na ni ukomo wa Manabii.

Hayo mawili yaliyopo kwenye biblia yenu mkiyaamin
mnatakiwa muwe Waislam
Ila kwa sababu hamuifat biblia yenu kikamilifu, mnaendelea kujipotosha
Kwa hio kwa sababu kakatazwa nguruwe ndo mnataka na sisi Wakristo tusile nguruwe???


Je! Unakubaliana na mimi kwamba aliekataza nguruwe na ngamia kwenye torati sie huyo aliekuja kuruhusu ngamia na akamuacha nguruwe kwenye blacklist???

Je! Unakubaliana na mimi wakristo na waislam hawamwabudu Mungu mmoja??
 
Hatuwezi kuifata biblia yote kwa sababu yapo mambo mengine yaliyoandikwa humo hayana hadhi ya kuwa katika neno la Mungu, ni dhahir wanadam wameandika humo, ndio mn kuna hitilafu nying sana katika biblia, ambazo zinaashiria kuwa maneno yake hayawez 'as a whole' kutoka kwa Mungu
Hayana hadhi ya kuwa neno la Mungu wa Uislam,,,uislam usiutafute kwenye biblia utachanganyikiwa na kubaki njia panda....Ukistick kwenye uislam utapata direction ya uislam la sivyo mtabaki kumlaumu Paulo wakati sio mtume wa Allah wala hana uhusiano na wowote ule...

Paulo yupo njia nyingine tofauti kabisa wala hana chochote cha kumhusianisha na uwongo...

Kila anaeelewa maneno ya biblia atamshangaa Muislamu akisema ni ya uwongo hasa kama huwa anaupitia uislam wenyewe....Huko kwenye kitabu chenu kuna mambo ya kutisha.
 
Hayana hadhi ya kuwa neno la Mungu wa Uislam,,,uislam usiutafute kwenye biblia utachanganyikiwa na kubaki njia panda....Ukistick kwenye uislam utapata direction ya uislam la sivyo mtabaki kumlaumu Paulo wakati sio mtume wa Allah wala hana uhusiano na wowote ule...

Paulo yupo njia nyingine tofauti kabisa wala hana chochote cha kumhusianisha na uwongo...

Kila anaeelewa maneno ya biblia atamshangaa Muislamu akisema ni ya uwongo hasa kama huwa anaupitia uislam wenyewe....Huko kwenye kitabu chenu kuna mambo ya kutisha.
Hakuna anayetafuta uislam kwenye Biblia, nakusaidia wew kwa sababu ndio kitabu unachokiamin, kina mapungufu mengi lakin yale yanayoshabihiana na Quran ni kweli yanatoka kwa Allah, na ni huyo huyo mmoja aliyenadiwa na Yesu Kwa jina la 'Elloi Elloi' yaan 'Allah Allah'.
 
Nikizingatia post [HASHTAG]#335[/HASHTAG]

Yesu kutumwa kwa wayahudi tu ina maana hata huyo mwanamke asingemponya mwanawe,,,,Maana hicho chakula cha watoto kimojawapo ni huo uponyaji,,,Alimwambia chakula cha watoto hawapewi mbwa akimpima imani na unyenyekevu wake,,,, alipoona yule mwanamke ni mnyenyekevu na mwenye imani alimponya Mwanawe... Hili linakupa jibu kwamba anawapenda hata watu wa mataifa na alikuja kwa ajili yao...



Kuna sehemu nyingine utamwona Yesu kwenye nchi za mataifa e.g
MARKO 5:1-13
Hapa alipita na akamponya mtu wa mataifa,,,la sivyo angemuacha tu aendelee kuwa mwehu huko makaburini.

Luka 7:1-10 alimponya mtu wa mataifa pia,,,Hivyo utajua akiwa anamjua binadamu kiundani na mwalimu Alikuwa akimfundisha binadamu kulingana na madhaifu alioyaona ndani ya moyo kwa Wakati huo huo

John 4:1-42 alipita kijiji cha wasamaria(wamataifa) akaongea na mwanamke mwenye wanaume wengi)slut( na akaona ndani ya moyo wake,,,,akampa darasa kama alivyo...Yesu ni akili kubwa ambayo huwasubua wengi wasiomwelewa..


Luka 24:46-47Yesu anatoa maagizo kabla hajapaa.Kwamba wasubiri nguvu iwajie,,,wasiondoke Jerusalem wasubiri,,,,ikishawajia waende kwa watu wote,,,kuanzia Jerusalem hadi kwa mataifa...

Kwa hio mataifa wangekuwa mbwa kama ulivyoelewa asingewaponya wala kukaa nao sehemu za kuchotea maji.


Pia natamani ungejua kwamba Yesu sio mtume,,,usitumie nguvu kuamini Yesu ni Issa...

Ukiniambia issa ni mtume au nabii nitakubali ila sio YAHSUA IBN MASIH....huyu YAHSUA(Yesu) ni ukurasa mwingine,,,,ndie alieanzisha Ukristo na mitume wake wakamalizia kazi,,,wapo mitume wake wamefia ulaya Italy,,uarabuni uturuki hadi misri...


UKRISTO uliochafuka ni wa madhehebu ya kisasa na mengine baadhi yaliofanana na matawi ya Uislam....ila wanaoelewa wanajua Ukristo wa kweli umetoka wapi na uko wapi...Mtizamo wako ndio unaokufanya uone Ukristo umechafuka pasi na kujua Ukristo na Uislam ni vitu viwili tofauti..Ni ngumu sana nyie kumuelewa Paulo kwa sababu mlitaka aongee vinavyofanana na Uislam,,,pasi na kujua alitumwa na nani kufanya nini,,,,,usije ukajidanganya kuuona Uislam ndani ya biblia ni jambo lisilowezekana kisayansi na hata kiimani...

Bado nimeona ukiamini vijarida vya waliberali kuliko hata vitabu vya marko yohana na luka,,,hili ni jambo la kusikitisha sana,,,sijui Sinclair,,sijui avinini!!craver sijui hugh scofield ha ha haha hahaha,,,hawa waliberali hamna kitu,,,na hivyo vitabu vyao vichafu mathalan ukafungua kurasa zote hutoshangaa kuona ajenda yao mahsusi ya ushoga na upuuzi mwengine usio na mashiko,,,mimi nikisoma hekaya zao huwa naumwa

Hawana cha zaidi ya utterly nonsense....

Huwezi kupinga mambo ya msingi yaliotumia zaidi ya akili kubwa kwa kutumia hadithi zaifu za kipumbaf za waliberali ambao sisi tunaijua nia yao.
 
Hayana hadhi ya kuwa neno la Mungu wa Uislam,,,uislam usiutafute kwenye biblia utachanganyikiwa na kubaki njia panda....Ukistick kwenye uislam utapata direction ya uislam la sivyo mtabaki kumlaumu Paulo wakati sio mtume wa Allah wala hana uhusiano na wowote ule...

Paulo yupo njia nyingine tofauti kabisa wala hana chochote cha kumhusianisha na uwongo...

Kila anaeelewa maneno ya biblia atamshangaa Muislamu akisema ni ya uwongo hasa kama huwa anaupitia uislam wenyewe....Huko kwenye kitabu chenu kuna mambo ya kutisha.
Uchambuzi mfupi wa Quran na biblia utaupata kwa Shk Muhsin kama alivyoandika:


BIBLIA NA QUR'ANI

Yesu aliungama kuwa hakuyasema yote aliyoyataka kuyasema, lakini huyo atakaye kuja yeye ndiye ataitimiza kazi. Mafunzo ya Muhammad juu ya dhambi, juu ya kuhisabiwa haki, na juu ya hukumu yamo katika Qur'ani, kitabu cha namna ya pekee ulimwenguni kwa usafi wake, kutokuwa na migongano yo yote na kuwa hakiwezekani kuigwa mfano wake.

Tangu kilipoteremka kwa Mtume s.a.w. miaka 1400 iliyokwisha pita hakikubadilika hata kwa neno moja, na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, hakitobadilika mpaka Siku ya Kiyama. Sir William Muir, mtoa kombo maarufu wa Uislamu, akiandika katika kitabu chake The life of Mohamet (Maisha ya Muhammad) amesema:

"Labda hapana kitabu cho chote kinginecho duniani ambacho kwa muda wa karne kumi na mbili kilichobaki na maandiko yake safi namna hii."


Tangu Sir William alipoandika hayo karne mbili nyenginezo zimekwisha biringita na Qur'ani imebaki vile vile safi kama siku alipoipokea Mtume Muhammad s.a.w. kwa Mwenyezi Mungu.


Kwa mintaraf ya Biblia lakini hatuwezi kuona msimamo mmoja, kwa sababu kwanza kuwa Biblia si kitabu kimoja, bali ni mkusanyiko wa vitabu vingi vilivyoandikwa na watu mbali mbali, katika zama mbali mbali. Makanisa yanazozana hata kuwa vitabu vipi vikubaliwe kuwa ndio Biblia, na vipi sivyo, vipi vimeandikwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu na vipi sivyo. Mara nyingi inatokea katika kitabu kimojawapo hicho hicho kinapingana wenyewe kwa wenyewe, kamatulivyokwisha ona mfano wake katika hadithi ya kutanasari Paulo iliomo katika kitabu cha Matendo ya Mitume.


Hugh Schonfield akiandika katika kitabu chake Those Incredible Christians, anasema:

"Ndani ya jalada za Biblia twaweza kukuta udanganyifu, mageuzo, na uzushi wa kukusudia kama unavyokuta katika vitabu vyenginevyo nje. Wataalamu wanajua vyema haya; lakini inapokuwa andiko la ndani ya Biblia si la huyo anayedai kuwa ndiye muandishi kila juhudi inafanywa lisitumiwe neno udanganyifu. Hali ni hiyo hiyo kwa maneno anayoambiwa Yesu kayasema na yanajuulikana kuwa si kweli. Tunaviita vitabu kama hivyo kuwa ni vya kikundi cha mawazo ya Kipaulo au Kipetro, na maneno yaliyogeuzwa au yaliyozuliwa tunayaita kuwa ni "ya pili"(Secondary). Kama hatukutumia hila itaonekana kuwa Roho Mtakatifu alishirikiana katika udanganyifu. Ni jambo lililoandikwa na kujuulikana kuwa mpaka ilipokatwa shauri mwishoe vitabu gani vihisabiwe kuwa ni Maandiko Matakatifu baadhi ya vitabu viliomo katika Biblia vilipingwa. Ilitolewa hoja na Wakristo wa kweli kwamba vitabu fulani havikuwa hakika vimeandikwa na hao wanaodaiwa kuwa ni waandishi wake. Pengine jina la mwenye kufanya udanganyifu lilidhukuriwa. Paulo anataja wakati wa uhai wake zilikuwepo barua za uwongo zikienezwa kwa jina lake yeye. Liliokuwa laonekana lafaa ni maslaha ya Kanisa tu. Mawazo yasiyokhusiana hata chembe na ukweli yakitumika kuelekeza maandishi na fikra kinyume na hakika ya walivyosema wenyewe watu kadhaa wa kadhaa wenye maana. Mtindo kama huu ulikuwa ni jambo la kawaida katika kazi ya uenezi hapo kale, na yafaa tuelewe kuwa ilikuwa ni kawaida vile vile miongoni mwa Wakristo wa zamani. Hivi ndivyo mchezo wa kueneza na kupendekeza ulivyokuwa ukichezwa. Na kwa wale wasio na dhamiri wala haya, wanaoamini kuwa muhimu ni lengo sio njia uitumiayo, mchezo huo unachezwa hata hivi sasa."


Asli ya vitabu vya Biblia haipo na haijuulikani, kwa hivyo ndio tunapata nakala nyingi sana. Inakubaliwa kuwa vitabu hivyo kama vilivyo sasa vimeandikwa na waandishi wanaadamu. Juu ya hivyo waweza kugundua baadhi ya maneno ambayo yametokana na Mungu asli yake. Lakini jinsi maandishi yalivyochanganyika, na yalivyoongezwa na kupunguzwa hata inakaribia kuwa ni muhali kulitambua lipi la Mungu na lipi la mwanaadamu ambaye alikuwa anawania madhehebu yake fulani au wazo lake maalumu. Qur'ani ni kinyume cha hayo. Kila neno lake ni la mwenyewe Mwenyezi Mungu. Yote ni maneno yake Mola Mlezi kama alivyofunuliwa kwa ufunuo (Wahyi) Mtume s.a.w., neno kwa neno, na yeye Mtume akiyatamka na wenye kuhifadhi kwa moyo wakihifadhi, na waandishi waaminifu wakiandika. Mkristo, Dr. John B. Taylor, Mwalimu wa Masomo ya Kiislamu katika Selly Oak Colleges, Birmingham anaandika katika kitabu chake Thinking About Islam:



"Tumekwisha hakikisha kwamba Waislamu hawasemi kuwa Muhammad kaandika Qur'ani, lakini kuwa kaipokea na akaisoma. Kama alivyokuwa Muhammad mwenyewe alivyoishughulikia matini ya Qur'ani, vile vile Waislamu wa baada yake walichukua kila taabu kuuhifadhi kwa ukamilifu usafi wa vipande vyote vya Qur'ani. Miaka miwili tu baada ya kufa Muhammad, na kuwa baadhi ya wale waliokuwa wameihifadhi Qur'ani kwa moyo, wakifa vitani, vipande mbali mbali vilikusanywa...Miaka michache baadaye, katika enzi ya Uthman, Khalifa wa tatu kuwatawala Waislamu baada ya kifo cha Muhammad, matini ilipitiwa tena kusahihishwa. Twaweza kusema vipi wale Waislamu wa kwanza walivyoshughulikia na kuwa na hamu kwa kuwa hata khitilafu za matamshi ya pande mbali mbali za ulimwengu wa Kiislamu hazikuruhusiwa katika kuisoma Qur'ani; na kwa hivyo matini rasmi ikahakikishwa inayofuata lafdhi ya Makka, na nakala nyenginezo zote ziliteketezwa kwa amri ya Khalifa. Kwa hivyo tunaweza kuwa na imani ya yakini kuwa hii Quran tuliyo nayo hii leo kamainavyomkinika kibinaadamu ndio ile ile iliyohakikishwa mnamo miaka michache tu baada ya kufa Mtume."


Hayo ni maoni ya mtoa kombo wa Kikristo. Qur'ani ni neno la Mwenyezi Mungu lisio na toa. Hiyo ndiyo maana ya maneno ya Yesu aliponena: "Hatanena kwa shauri lake mwenyewe lakini yote atayoyasikia atanena."
 
Hakuna anayetafuta uislam kwenye Biblia, nakusaidia wew kwa sababu ndio kitabu unachokiamin, kina mapungufu mengi lakin yale yanayoshabihiana na Quran ni kweli yanatoka kwa Allah, na ni huyo huyo mmoja aliyenadiwa na Yesu Kwa jina la 'Elloi Elloi' yaan 'Allah Allah'.
Mimi Huwezi kunisaidia kwa kitu ninachoona hukielewi...Huwezi msaidia anaejitambua...However mimi ninajua vitu kwenye kitabu chenu ambavyo najiuliza unapovisoma huwa unavielewa kama mimi??? Ni vitu ambavyo naamini ungekuwa mkristo,(mfano) ungeshangaa sana waislam wana gut ip ya kuuongelea Ukristo ilhali wapo mahali pa kushangaza kiasi hicho!!!!!

Kiufupi mimi nimesoma sana kitabu chenu...na yapo mengi yapo kwenye kitabu chenu ya kunifanya nisikuelewe kwa namna yoyote unayoweza kuelezea mapungufu ya Ukristo.
 
Ni tafsiri ipi ya lugha inayokupa uhakika kwamba Eloi ni Allah,,,pili kama Yesu Alisema Mungu wangu una uhakika kwamba huyo Mungu ni Allah Subhana wataalah.???? Nataka uelewe kwamba uislam Una Mungu wake na Ukristo una Mungu wake.
 
Ni tafsiri ipi ya lugha inayokupa uhakika kwamba Eloi ni Allah,,,pili kama Yesu Alisema Mungu wangu una uhakika kwamba huyo Mungu ni Allah Subhana wataalah.???? Nataka uelewe kwamba uislam Una Mungu wake na Ukristo una Mungu wake.
Ni tafsir ipi ya Lugha inayokufanya umuelewe Elloi kama God?
 
Mimi Huwezi kunisaidia kwa kitu ninachoona hukielewi...Huwezi msaidia anaejitambua...However mimi ninajua vitu kwenye kitabu chenu ambavyo najiuliza unapovisoma huwa unavielewa kama mimi??? Ni vitu ambavyo naamini ungekuwa mkristo,(mfano) ungeshangaa sana waislam wana gut ip ya kuuongelea Ukristo ilhali wapo mahali pa kushangaza kiasi hicho!!!!!

Kiufupi mimi nimesoma sana kitabu chenu...na yapo mengi yapo kwenye kitabu chenu ya kunifanya nisikuelewe kwa namna yoyote unayoweza kuelezea mapungufu ya Ukristo.
Quran ukiisoma kwa kuielewa huwez ukaendelea kuamini Mungu -mtu, ukaamini kuna mtu ame 'pay for your sins kwa hiyo unaweza fanya dhambi yoyote!
 
Ni tafsiri ipi ya lugha inayokupa uhakika kwamba Eloi ni Allah,,,pili kama Yesu Alisema Mungu wangu una uhakika kwamba huyo Mungu ni Allah Subhana wataalah.???? Nataka uelewe kwamba uislam Una Mungu wake na Ukristo una Mungu wake.
SHK MUHSIN
anaendelea.....


A COMFORTER

Hebu sasa natulichungue hili neno lililofasiriwa Msaidizi katika Bibilia ya Kiswahili, na ambalo limeitwa "Comforter" yaani Mliwazi katika Biblia ya Kiingereza ya zamani ya King James, na likaitwa "Counsellor", yaani Mshauri katika Biblia ya Kiingereza ya Revised Standard Version, na likaitwa "Helper" yaani Msaidizi katika Biblia za Kiingereza mpya mpya kama New World Translation na Good News Bible, na "Mu'azzi", yaani Mliwazi katika Biblia ya Kiarabu ya Darul Kitabul Muqaddas ya Cairo.


Taabu inayotupata katika kuisoma Biblia ni kuwa asli ya maandiko yote yamepotea. Tumebakiwa na nakala za tafsiri tu. Na hata tukipata kwa mfano Injili ya Yohana iliyoandikwa kwa lugha ilioandikwa mwanzo, nayo ni Kigiriki, hatuna ushahidi wo wote kuwa ndivyo ilivyoandikwa hapo mwanzo. Injili hii iliandikwa mwanzo wake kiasi miaka mia baada ya Yesu. Lakini nakala zilio kongwe kabisa zinazopatikana si chini kuliko miaka mia mbili baada ya kuandikwa kwake.
Hali kadhaalika maneno aliyoyasema Yesu tunayapata kwa tafsiri tu, kwani Yesu hakusema Kigiriki wala Kilatini, bali lugha ya kawaida Palastina wakati ule ilikuwa ni Kiaramiya na lugha yao ya dini ni Kiebrania. Zote mbili hizo zina asli moja na Kiarabu. Injili ya Yohana ndio hiyo iliyotaja hiyo bishara ya Yesu kuwa atakuja huyo aitwae Msaidizi. Katika utangulizi wa nakla ya Biblia ya Revised Standard Version imeelezwa kuwa hata hiyo matini ya Kigiriki ilioko "imeharibiwa na makosa yaliyojumlika kwa kukosoea kosea kwa walionukulu muda wa karne kumi na nne." Wataalamu wa Biblia wakubwa kama Rudolf Bultmann (Mprotestanti) na Father John Lawrence Mackenzie (Mkatoliki) wanakubali kuwa sehemu nyengine za Injili si kweli kihistoria, na ya kwamba maneno fulani ya Yesu kwa hakika yamebuniwa na Kanisa la kale. Ye yote asomae maandishi ya wataalamu wa Kikristo wenyewe, bali hata mwenye kusoma hizi hizi tafsiri za Biblia mbili tatu ataona vipi maneno yanavyogeuzwa, yanavyoongezwa, na yanavyopunguzwa, hata kugeuza kabisa makusudio.Encyclopaedia Brittanica (nuskha ya 15) baada ya kueleza hayo imesema: "Ushahidi kuwa hayo hakika yametokea ni mwingi na wa namna mbali mbali." Qur'ani inasema:



Na kuna baadhi yao wanaopindua ndimi zao kwa Kitabu ili mpate kuyafikiri hayo kuwa ni ya Kitabu, wala si ya Kitabu, na wanasema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu; na hali hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu, na wanamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo na hali wanajua.

(Qur'ani) Al Imran 3.78



Je, ni neno gani hilo lilioandikwa Kigiriki kuwa Yesu kalitumia hata wengine wakalifasiri Mliwazi, wengine Mshauri, na wengine Msaidizi, kuwa ndiye wa kutarajiwa kuja? Nakla kongwe kabisa iliyopo ya hiyo Injili imetumia neno la KigirikiParakletos ndilo wanalolifasiri Msaidizi katika Injili ya Kiswahili. Katika Kamusi la Kigiriki neno Parakletos linafasiriwa kuwa ni "mwenye kuitwa kusaidia, mtetezi, mwombezi." Baada ya kuzingatia hayo tuliyoyasema hapo juu vipi yalivyogeuzwa geuzwa maneno, basi si jambo la kustaajabisha ikiwa neno hili Parakletos nalo wamelipotoa waandishi na wanaonukulu kwa karne na karne zilizopita, kama ilivyosemwa katika utangulizi wa Biblia ya Kiingereza ya Standard Revised Version. Tunajua vipi Wazungu walivyolipotosha jina la Muhammad, na kuliandika "Mahomet".



Hali kadhaalika neno la Kigiriki laPeriklitos ni wepesi kulipotoa na kuliandika Parakletos. Kwa dhaahiri khitilafu ni ndogo, lakini kwa hakika neno Periklitosmaana yake ni Msifiwa, ambalo kwa Kiarabu ndio khasa Muhammad au Ahmad au Mahmuud. Jambo la ajabu ni kuwa tangu wakati wa Yesu hapakutokea Mwaarabu mwenye jina hilo ila huyo Muhammad bin Abdullah, ambaye alipewa jina hilo na babu yake tangu kuzaliwa kwake bila ya kujua huyo mzee kuwa mjukuu wake atakuja kuwa Nabii ambaye amebashiriwa na Yesu. Na huyo babu hakuwa Mkristo bali alikuwa akifuata mila ya kishirikina na wala hakuijua Taurati wala Injili. Na wala hakutokea Giriki mwenye jina la Periklitos.


Ni makosa kusema kuwa huyo Periklitos (Msifiwa) aliyefasiriwa kwa kukosea Msaidizi, ni Roho Mtakatifu, ambaye Wakristo wanasema ni nafsi ya Mungu. Ushahidi wa makosa hayo umo humo humo katika Injili ya Yohana. Kama huyo Msaidizi ni Roho Mtakatifu yawaje basi Yesu kusema "yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo (Periklitos) hatakuja kwenu." Roho Mtakatifu twaambiwa ni Mungu wa milele. Je, kwani Mungu hatokuwepo maadamu Yesu yupo? Je, yeye Yesu na Manabii wote waliomtangulia na watakatifu wengine hawakuteremkiwa na Roho Mtakatifu? Hayo yamo katika Agano Jipya na Agano la Kale pia.


Huyo Periklitos (Ahmad au Muhammad) "atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu." Na ndio hivyo ilikuwa ni Muhammad aliyedhihirisha ukweli wote wa Mwenyezi Mungu mmoja, asiyezaa wala asiyezaliwa, na akawaokoa umma mzima wasimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu cho chote, wala mtu ye yote. Ni yeye ndiye aliyewarejesha Wakristo kwenye mafunzo ya Yesu na Musa kwamba Mwenyezi Mungu hana utatu, bali Mungu wao ni Mungu mmoja kama alivyofunza Yesu (Tazama Marko 12.29), na kama alivyoamrishwa Musa (Tazama Kutoka 20.3-4). Ni yeye ndiye aliyemtoa Yesu katika matusi ya Mayahudi walipomshutumu kuwa ni mdanganyifu, na matusi ya wanaojiita Wakristo kumzulia kuwa kafa kifo cha laana msalabani, na kuwa yeye ni mungu wa bandia kama walivyo miungu ya washirikina makafiri. Kweli yote imehakikishwa na huyo Periklitos, Muhammad, Roho wa Kweli. Huyo ambaye "hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena" hawezi kuwa Mungu,bali huyo ni Mtume wa Mungu, Mtume ambaye ametuachia Kitabu kizima ambacho kila neno liliomo humo ni neno alilolisikia kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe. Hicho ni Kitabu pekee duniani, nacho ni Qur'ani.



Na ni Mwenyezi Mungu katika Qur'ani ndiye aliyesema:



Na aliposema Isa bin Mariam: enyi wana wa Israili! Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na kumbashiria Mtume atakayefika baada yangu, jina lake litakuwa Ahmad.

(Qur'ani) As Saff 61.6



Injili ya Mtakatifu Barnaba ambayo ilipigwa marfuku kwa amri ya Gelasius katika mwaka 496 B.K., karne nzima kabla ya kuja Nabii Muhammad s.a.w. inaeleza:

Tena Yesu akasema: Kwa maneno yenu siliwaziki, kwa sababu mnapotaraji mwangaza patakuja kiza; lakini maliwaza yangu ni kwa kuja Mtume ambaye ataivunja kila fikra mbaya juu yangu mimi, na dini yake itaenea na kutanda ulimwengu mzima, kwani hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu alivyomuahidi Ibrahimu baba yetu. Na linalonipa maliwaza ni kuwa dini yake haitakuwa na ukomo, kwani itahifadhiwa na Mwenyezi Mungu. Kuhani akajibu: Baada ya kuja huyo Mtume wa Mungu watakuja manabii wengine? Yesu akajibu: Hawatakuja Manabii wa kweli baada yake waliotumwa na Mwenyezi Mungu, lakini watakuja manabii wengi wa uwongo, na hayo ndiyo masikitiko yangu. Kwani shetani atawanyanyua kwa hukumu ya haki ya Mwenyezi Mungu, na atawaficha chini ya udanganyifu wa injili yangu....Tena akasema kuhani: Huyo Masihi ataitwaje, na ishara gani itaonyesha kuja kwake? Yesu akajibu: Jina la Masihi ni Msifiwa, kwani Mwenyezi Mungu mwenyewe alimpa jina hilo alipoiumba roho yake na akaiweka katika utukufu wa mbinguni.

Injili ya Barnaba Sura 97



Imehaririwa na kufasiriwa kutoka Muswadda uliopo katika Maktaba ya Vienna, Austria, na Lonsdal na Laura, Oxford. Hii Injili ya Barnaba ndiyo inaaminiwa kuwa ni Injili ya pekee iliyoandikwa na mwanafunzi wake mwenyewe Yesu. Zilizobaki zimeandikwa na watu wengine baada yao hao wanafunzi kwisha kufa, lakini yakatumiwa tu majina ya hao wanafunzi. Injili hii ilikuwa inakubaliwa kuwa ni sahihi na Wakristo wa kwanza, na ikitumiwa katika kanisa la Alexandria mpaka mwaka 325 B.K. Mwaka huo ndipo Baraza la Nikaia likaamua kuzikubali hizi Injili nne za Mathayo, Marko, Luka na Yohana ziingizwe katika Biblia kuwa ni maandiko matakatifu, na likapiga marfuku Injili nyenginezo, na mojawapo ni hii ya Barnaba, kuwa ati si sahihi. Vitabu hivyo vilivyokataliwa viliitwa Apokrifa, yaani vinavyofichwa, na hapo zamani ye yote aliyeonakana navyo aliuwawa.


Injili iliyokubaliwa na Baraza kuwa ni sahihi, na iliyomo katika Biblia, Injili ya Mathayo, nayo inatueleza kuwa Yesu alibashiri kutokea kwa Muhammad, ambaye ni katika uzao wa Ismaili, anayefananishwa na jiwe liliokataliwa na wajenzi. Pia Yesu alibashiri kuinuka kwa Umma wa Kiislamu utakaopewa Ufalme wa Mungu, nayo yote hayo yakatimia:



Yesu akwaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.

Mathayo 21.42-44



Yesu kwa maneno hayo tuliyoyanukulu anawaambia Waisraili:


"Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake." Taifa la Israili halitazaa matunda tena. Yesu alililaani. Twasoma katika sura hii hii ya 21 ya Mathayo:



Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.

Mathayo 21.18-19



Wataalamu wa Biblia wanakubaliana kuwa huo mtini ulionyauka, usioleta matunda yake, ni taifa la Israili. Na hatuna haja kutafuta maoni ya mtaalamu ye yote kutufasiria kuwa taifa lizaalo matunda lenye kubarikiwa ni taifa la Ismaili liliomzaa Mtume Muhammad. Biblia yenyewe inatwambia kuwa Mwenyezi Mungu alimwambia Ibrahim:



Na kwa khabari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.

Mwanzo 17.20



Kwa hivyo tunaweza kusema bila ya wasiwasi kuwa Yesu alikusudia kuwambia Mayahudi: "Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu kwa kuwa nyinyi mmeacha amri za Mwenyezi Mungu alizozileta Musa na nilizothibitisha mimi, na ufalme huo watapewa taifa la Muhammad, mwana wa Ismaili, taifa liliobarikiwa na Mwenyezi Mungu, lenye kufuata maamrisho yake kama alivyofundisha Ibrahim na Musa na mimi na Manabii wote waliokuja kabla yangu mimi."


Kama alivyobashiriwa Nabii Ibrahim kuwa katika uzao wake kwa mwanawe Ismail utatokea umma uliobarikiwa wenye kuleta matunda, kadhaalika alibashiriwa Nabii Musa na Mwenyezi Mungu kwamba katika ndugu zao Wana wa Israili, yaani Wana wa Ismaili, atatokea Nabii, naye ni Nabii Muhammad, ambaye Mwenyezi Mungu anawataka viumbe wote wamuitikie na wamfuate. Na ye yote "asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake." Kwa ukamilifu Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii Musa haya:



Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao (yaani Wana wa Israeli) mfano wako wewe (Musa), nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. Lakini nabii atakayenena nena kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena kwa jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana? Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope.

Kumbukumbu la Torati 18.19-22



Zingatia vyema: maneno hayo anaambiwa Nabii Musa a.s., naye ni Nabii wa Wana wa Israili. Nabii anayebashiriwa hatotoka miongoni mwao Wana wa Israili, bali miongoni mwa ndugu zao, yaani Wana wa Ismaili. Lakini Nabii huyo hatokuwa kwa Wana wa Ismaili tu, bali hata wao Waisraili pia, kwani Mwenyezi Mungu anawaambia: "Nitawaondokeshea", yaani wao pia Wana wa Israili. Tena Mwenyezi Mungu anasema: "Mtu asiyesikiliza mananeo yangu atakayosema yule (Nabii) kwa jina langu, nitalitaka kwake." Ni dhaahiri kuwa yawapasa watu wote, mataifa yote, wampokee huyo Nabii atakyetokea katika ukoo wa Ismaili.


Mungu anasema: "Nitatia maneno yangu kinywani mwake." Kitabu gani ambacho kinadai, na madai yenyewe yakawa ya kweli, kuwa ni maneno khasa ya Mwenyezi Mungu isipokuwa Qur'ani? Muhammad alikuwa ni mkalimani wa Mwenyezi Mungu, akiyatamka tu yale yaliyokuwa yakifunuliwa kwake; na waandishi waliokuwepo miongoni mwa wafuasi wake wakiandika na wengine kuhifadhi kwa moyo maneno ya Mwenyezi Mungu wakati ule ule yeye Nabii Muhammad alipokuwa akiyatamka. Mwenyezi Mungu anamuamrisha katika Qur'ani:



Sema: Mimi si kizushi katika Mitume. Wala sijui nitakavyofanywa mimi wala mtakavyofanywa nyinyi. Sifuati ila yaliyofunuliwa kwangu; na mimi si cho chote ila ni Mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.

(Qur'ani) Al Ahqaf 46.9



Mwenyezi Mungu mwenyewe anawakabili kwa majadiliano wenye kutia shaka kuwa hii Qur'ani ni maneno yake au la:



Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomtermeshia Mja wetu, basi leteni sura moja katika mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu ikiwa mnasema kweli. Na mkitofanya - na hakika hamtafanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe ulioandaliwa kwa wakanushao.

(Qur'ani) Al Baqarah 2.23-24



Kwa muda wa miaka 1400 hapajatokea mwanaadamu wala jini aliyeweza kujibu hoja hiyo. Qur'ani ndio muujiza wa kudumu milele. Huu si muujiza wa kusimuliwa ya kwamba ulitokea, na watu wakazozana ulitokea kweli au haukutokea. Huu ni muujiza uliobaki na utabaki ukionekana tangu siku ulipoteremka mpaka leo na mpaka milele. Unaweza kuusoma leo, kesho, kesho kutwa na mtondogoo na daima dawamu, na ukuathiri kwa ufasihi wake uliokuwa hauna mfano, utamu wa maneno yake, ukakuongoza kwa ubora wa mafunzo yake, ukakusaidia kukabiliana na ulimwengu wako, ukaondoa matatizo yako ya kidunia na ya kiroho, ukatengeneza dunia yako na akhera yako.


Yamkinika kuwa mimi nikatuhumiwa kuwa imani yangu inanipelekea kuisifu hivi Qur'ani, lakini hebu natuiachie kalamu ya Muingereza Mkristo, Edward Gibbon, ambaye ni mtaalamu mkubwa wa historia, na bingwa wa uandishi, tuiache kalamu yake isiyo na khofu wala mapendeleo ituhukumie. Gibbon ameandika:



"Hapana kitabu duniani ambacho ndani yake Mwenyezi Mungu ameelezwa kwa utakatifu zaidi, kwa ubora zaidi, kwa usafi zaidi, kwa uzuri zaidi, kwa ukamilifu zaidi, kwa utukufu zaidi, na chenye kustahili zaidi Ungu kuliko Mungu huyu aliyekuwa Muhammad akimuabudu. Ruwaza hii haiwezi kutengenezwa kuliko ilivyo; sifa moja tu ikiondolewa italeta nuksani katika ukamilifu wake, na haiwezekani hata moja kuongezwa bila ya kuonekana kuwa imezidi na haina maana. Ni jinsi hiyo alivyo Mungu wa Muhammad kama alivyoelezwa katika Qur'ani. Kwa ujasiri kweli amepiga chapa isiyofutika kabisa juu ya sahifa za historia wazo la imani safi kabisa ya Mwenyezi Mungu Mmoja wa pekee; na kuliendea wazo hilo mwanaadamu mwenye akili, akitaka asitake, hawezi ila aliendee kwa yakini, hata ingawa pole pole."


Basi ni kitabu hichi ndicho kilichowafanya Waislamu wa zamani wa Vyuo vyao Vikuu vya Cordova (katika Uspania), Cairo, Damascus na Baghdad wakawa ndio waanzishi wa ilimu za Algebra, Alkimya (chemistry), Falaki (Astronomy) na utibabu wa kisasa. Peke yake ni jambo la kustaajabisha kuwa mtu ambaye mwenyewe alikuwa hajui kusoma wala kuandika, katika kaumu ya wajinga, amri ya kwanza iliyofunuliwa kwake - si kusali,wala kutoa zaka, wala kutazama wagonjwa na wazee, bali hata si kuamini Mungu mmoja, bali:



Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba, amemuumba mwanaadamu kwa tone la damu iliyotundikwa. Soma! na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote, ambaye amefundisha kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu yale aliyokuwa hayajui.

(Qur'ani) Al 'Alaq 96.1-5



Umma uliokuwa mjinga, mabedui wa jangwani - hali yao haikukhitalifiana sana na kabila yo yote ya Kiafrika yenye kutangatanga na mifugo yao, kama Wamasai, ambao ndani yake waliokuwa wakijua kusoma na kuandika wakihisabika kwa vidole vya mkono mmoja - Umma kama huo ukaamrishwa la mwanzo la kulifanya ni kusoma, na Mwenyezi Mungu mwenye kutoa amri hiyo hakutafuta sifa kubwa kuliko Aliyefundisha kwa kalamu, Aliyemfundisha mwanaadamu yale aliyokuwa hayajui. Kama huu si muujiza upi mwenginewe? Hii ni Ishara kuwa enzi mpya imekuja, enzi ya kusoma, enzi ya kalamu, enzi ya kutumia akili. Enzi za kugeuza fimbo kuwa nyoka, kufufua walioonekana kama wamekufa, kugeuza maji yakawa mvinyo na mazingaombwe kama hayo zimepita. Hayo labda yafanywe juu ya jukwaa katika majumba ya tamasha kwa kuwastarehesha vijana. Lakini katika mambo yaliyo na uzito kweli yahitaji masomo, kujifunza, na kufundisha kwa kalamu. Huu wakati wa muujiza wa hichi Kitabu kilichoandikwa kwa kalamu na kinachoweza kusomwa milele, na kila mwenye tatizo lake anaweza kulitatua kwa kusoma na kuzingatia vilivyo yaliyoandikwa humu na mwenyewe Mwenyezi Mungu aliyemuumba mwanaadamu kutokana na tone la damu, bali kutokana na mchanga khasa. Zama za muujiza wa kutumia akili na masomo umefika.


Bila ya Qur'ani ilimu zote za Warumi, za Magiriki, za Waajemi, za India, za China, za Misri, na za Iraq, zingelipotea kabisa, badala ya kuwa zimehifadhiwa, na zikazidi kukuzwa na kuendelezwa na zikakabidhiwa ulimwengu huu wa leo.


Kila tunapoona neema ya uvumbuzi wo wote ambao tukafikiri kuwa ndio wa kisasa na umetokana na Wazungu yafaa tushukuru kuwa lau kwamba ingelikuwa Qur'ani haikuamsha ulimwengu, na wakazindukana Waislamu wakatuhifadhia yaliyopita na wakayaongeza mengi sana yao wenyewe tunsingezipata hizi neema za leo, ikiwa ni katika matibabu, ikiwa ni katika vipando, ikiwa katika makaazi, ikiwa katika vyakula, ikiwa katika usafiri, na ikiwa katika fanni zo zote na ilimu zo zote za sayansi. Kitabu hichi ndicho kilichowageuza waliokuwa wakiabudu jua na mwezi na nyota na mawe na mito na miti na milima, kikawaambia kuwa vyote hivyo na vyenginevyo vyote vimeumbwa ili vimtumikie mwanaadamu.



Ni Kitabu hichi kilichokomboa akili za watu zichungue mpaka katika sehemu ambazo watu kabla yake hata hawajaziotea:



Enyi jamii ya majini na watu! Mkiweza kupenye kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni!

(Qur'ani) Ar Rahman 55.33



Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama, na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanaozingatia.

(Qur'ani) Al Baqarah 2.164



Vifungu hivi viwili tu tulivyovinukulu hapa vyatosha kukupa mawazo vipi Qur'ani ilizindua wanaadamu waliolala washughulikie ilimu, na uchunguzi, na utafiti na uvumbuzi. Uropa iliolala katika Karne za Giza (Dark Ages) ilizinduliwa na muamko wa Kiislamu katika kila ilimu. Katika vifungu hivi tunaona mahimizo na ishara ya kuanzisha ilimu za anga (Space Sciences), ilimu za matabaka ya ardhi na uvumbuzi wa maadini (Geology na Minerology), Jiografia, ilimu ya unahodha (Navigation), ilimu ya hali za hewa (Meteriology), na ilimu za zaraa (ukulima). Huu ni mfano mdogo tu; ni kama tone katika bahari. Mwenye kuisoma Qur'ani kwa moyo safi na akili kunjufu atagundua ndani yake uwongofu ambao haupati po pote kwengineko, atapata ilimu ambazo hazipati po pote, na atapata ukunjufu wa moyo ambao hawezi kuupata penginepo.



Katika bishara aliyopewa Musa na Mwenyezi Mungu juu ya kuja Nabii Muhammad aliambiwa: "Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii usimwogope."


Ikiwa Mtume Muhammad alikuwa na sifa yo yote ambayo ilizagaa zaidi kuliko nyengine basi ni hiyo sifa ya kubashiri jambo nalo likatokea kama alivyosema. Hayo yajuulikana kikweli kwa kuwa maisha yake, kinyume na waongozi wa dini zilizotangulia, yalikuwa katika zama ambazo zinajuulikana vyema na wanachuoni wa taarikh (historia). Yeye si mtu wa hadithini, lakini ni mtu wa hakika, anayejuulikana vilivyo, mtu aliyekuwa akikatibiana na kupambana na wakuu wa serikali na dola zilizokuwapo zama zake. Akikatibiana na Mfalme wa Uajemi, na Mfalme wa Rumi, na Wakuu wa Misri na Uhabeshi, na Wakuu wengineo walioko Arabuni na nje ya Arabuni. Kwa kutimia kauli zake, kama tulivyokwisha toa mifano kadhaa wa kadhaa, ndio akaitwa As saadiq, Msema Kweli, Al Amin, Muaminifu.


Bishara aliyopewa Nabii Musa a.s. inasema: "Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe." Hakuja Nabii baada ya Musa aliyefanana naye kama alivyofanana naye Nabii Muhammad. Musa na Muhammad walikuwa wakhubiri wa dini kwa mambo ya kiroho, na vile vile wakawa ni waongozi katika mambo ya dunia. Walikuwa wamekusanya dini na siasa, Unabii na utawala, uwalii na uamiri jeshi. Walikuwa ni maraisi wa kaumu zao, walikuwa mahakimu, walikuwa wapigania uhuru licha ya kuwa wanasiasa. Nabii Musa alipambana na Firauni na kaumu yake, Muhammad alipambana na Abu Jahli na kaumu yake. Musa ilimlazimu akimbie ahame Misri alikozaliwa ende Palastina. Muhammad pia ilimlazimu aongoze watu wake kukimbia adhabu za Makureshi Makka alikozaliwa ende Madina. Nabii Musa kapokea sharia ya Mungu katika Taurati, na Nabii Muhammad kapokea sharia ya Mungu katika Qur'ani. Wote wawili walioa wakawa na wake na wakazaa. Wote wawili walikufa kitandani ulipotimia mwisho wa maisha yao.


Mwenyezi Mungu alimwambia Nabii Musa: "Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa."


"Nabii yule atakufa." Nini maana ya haya? Kufa ni faradhi kwa kila kilio hai. Maana yake atakufa siku si zake, yaani atakufa ghafla naye kijana, au atauliwa. Nabii Muhammad alikufa na umri wake miaka 63, kiasi ya umri wa utuuzima wakati ule na mpaka hivi sasa. Juu ya misukosuko isiyokadirika, na vita alivyopambana navyo, na majaribio ya kumuua aliyofanyiwa katika maisha yake, Mwenyezi Mungu alimsalimu mpaka akafika wakati wake baada ya kutimiza na kukamilisha ujmbe wake aliyopewa, na akafa kitandani, na huku kazungukwa na ahali zake.



Yaliyosemwa katika Taurati pia yamesemwa katika Qur'ani:



Na kama (Mtume) angelizua juu yetu baadhi ya maneno tu bila shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia - kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo; na hapana ye yote katika nyinyi angeweza kutuzuia naye.

(Qur'ani) Al Haqqah 69.44-47



Ama wanavyodai wengine kuwa bishara hii yamkhusu Yesu wamekosea sana. Yesu hakufanana na Musa ila katika kuwa ni Nabii na kuwa ni Mwana wa Israili. Kwa unabii wale wanaomdaia ungu Yesu wanamkatalia kuwa ni Nabii. Ikiwa Yesu kafanana na Musa, basi si Mwana wa Mungu wala si Mungu. Kwa hivyo wanajipinga wenyewe. Bishara inasema wazi kuwa huyo Nabii hatakuwa katika Wana wa Israili, bali miongoni mwa ndugu zao, nao ni Wana wa Ismaili. Yesu ni Muisraili. Kwa hoja hii pia Yesu siye aliyebashiriwa hapa. Nabii huyo aliyebashiriwa kama ni wa kweli hauliwi, wala hafi kijana. Yesu, kama wanavyodai Mayahudi na wakaamini Wakristo, aliuwawa msalabani, tena yungali kijana. Ikiwa bishara hii wanataka kumuambatisha nayo yeye Yesu, basi itakuwa wanamtuhumu kuwa Yesu ni nabii wa uwongo "aliyenena neno kwa kujikinai kwa jina la Mungu, ambalo hakuagizwa kulinena." Mwenyezi Mungu apishe mbali. Zaidi ya hayo Nabii Isa kinyume na Nabii Musa na Nabii Muhammad (rehema na amani ya Mungu iwashukie wote) hakuja na sharia yo yote. Yeye alifuata ile ile sharia ya Musa iliomo katika Taurati, na mwenyewe kasema yeye hakuja ila kutimiza tu. Wala yeye hakuongoza watu katika mambo ya kilimwengu, bali alimwachia Kaisari ulimwengu na yeye kashughulikia mambo ya akhera, ufalme wa mbinguni.


Miezi mitatu tu kabla ya kifo chake Mtume Muhammad s.a.w. aliyataja maneno ya Mwenyezi Mungu aliyoteremshiwa:



Leo waliokufuru wamekata tamaa katika Dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.

(Qur'ani) Al Maida 5.3



Miaka mia sita kabla ya haya Yesu naye alisema: "Chakula changu ni kufanya mapenzi ya yeye aliyenituma na kutimiza kazi yake."


Wote wawili wamekutana kwenye kutenda apendayo Yeye aliyewatuma, na huo ndio Utume, na huo ndio Unabii, na huo ndio Uislamu. Kutenda mapenzi ya Mwenyezi Mungu ndio waajibu wa binaadamu, na katika hayo ndio hupatikana wema, na katika hayo ndio kuhisabiwa haki katika maisha haya na maisha ya milele ya baadaye. Huko ni kufuata mwenendo wa maumbile aliyowaumbia Mwenyezi Mungu wanaadamu wote kama mwenyewe asemavyo:



Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la mwenyewe Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu; hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa, walakini watu wengi hawajui.

(Qur'ani) Ar Rum 30.30
 
Back
Top Bottom