Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Hakuna aneyejuwa siri ya Mungu, jinsi alivyo itengeneza kwa binadamu, mungu pekee ndiye anajuwa hilo.kinachotakiwa amini katika mafundisho ya mungu. Wasio amini waendelee kutoamini kwani wao wanaongjzwa na shetani kutoamini katika mungu.

Binadamu ni rahisi sana kuamini matendo au miujiza ya shetani kuliko Miujiza ya mungu. Huwezi amini mungu , kama usiporuhusu roho yako iongozwe na roho mtakatifu.
 
Sasa kama Mungu ana siri kuhusu roho hayo mafundisho yake anafundisha nini ili tuyaamini? Maana kama roho hajatufunulia sasa tunajifunza nini?
 
Kweli kabisa na hili ndio jibu kwa wale wanaopinga kuwa hakuna Mungu. Mungu ni roho haonekani kwa macho ya nyama na damu.
Unatofautishaje mtu anapokuambia kitu cha uongo ambacho hakipo, akakwambia kipo ila ni roho ila hakionekani kwa macho ya nyama na damu na habari za Mungu?

Unawezaje kusema "Huu ni uongo, unachosema hakipo" kwa mtu anayesema uongo huo, halafu hapo hapo ukasema Mungu yupo?

Kinachoutofautisha uongo huo na habari za Mungu ni nini?
 
Yee mwenyewe kasema sio Mungu
Mungu yupo?

Tutajuaje yupo kwa uhakika?

Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
 
Roho ni sehemu ya Super Natural power.

Ni sehemu ya Mungu. Hivyo haionekani na haitakuja kuonekana.

Ukifa Roho hurudi kwa Mungu kwani ni sehemu yake. Wakati Mwili hurudi mavumbini kwani mwili ni sehemu ya Mavumbi.
Saaafi. lakini naomba niongezee kitu hapo, baada mtu kufa roho yake hurudi kwa Mungu kwaajili ya kusubiri hukumu kulingana na mtu husika kwa namna alivyoishi katika siku za uhai wake. Ahsante
 
Kama wanasayansi wanaweza kuset vitu vikawa automatic, iweje Mungu ashindwe? nadhan Mungu ashaweka uumbaji wake ktk automatic system pengine now anaumiza kichwa(sorry God has no any example) afanye nin kipya ktk creativity yake...
Shetani ana nguvu sana za kumpotosha binadamu juu ya mungu. Watu wanashindwa kuami hata huwo uwezo wa wanasayansi wamepewa na mungu.
 
Mungu ni roho.
Roho ni mimi.
Mimi ambaye sio physical body, astral body, etheric body, lower mental, higher mental buddhic, or atmic. Mimi niliezidi consciousness ya aina yoyote ile. Mimi ambaye nipo nilikuwepo na nitakuwepo muda wote.

Kwa sababu nipo duniani inabidi niwe na properties zinazoruhusu kuwepo duniani kwa physical body.

Ukitaka kuelewa kuhusu mungu na roho kwa akili hutaweza sababu mungu ni zaidi ya akili na hana umbo wala rangi wala sauti. Kwa mbali unaweza soma theosophy books vikakupa mwanga lakini bado hutakua umemjua mungu. Sababu mungu au roho hauwezi kuijua ila unaweza kuwa. Na ili uwe ni lazima uende zaidi ya mwili, akili na consciousness yoyote ile.
 
Ni wapi nimesema imani yangu ni kweli? Hebu onesha!

Unamlisha mtu maneno kisha unaweka hitimisho kwa maneno uliyomlisha huo ni usanii.
 
Majibu yako hapa kwa ufupi.... SOMA

i. Kila kitu duniani hu vibrate. Kuna molecular movement in every object in the universe. Kiwe jiwe, meza uliyokalia, air etc

ii. Object yoyote inaonekana kwa macho kwa sababu speed ya vibration ni ndogo. Mfano risasi iliyotoka kwenye bunduki sio rahisi kuiona kwa macho kwa sababu hiyo,tofauti na ukirusha jiwe analiona . Hivyo hivyo miili yetu inaonekakana sababu ya low vibration

iii. Roho ni matter, lakini ni subtle matter ambayo vibration yake ni ya hali ya juu sana. Kwa hiyo haionekani wala kushikika. Katika hali hiyo physical property yake hupotea na kuchukua form nyingine. Subtle, or spirit form. Ndiyo maana halisi ya kutoonekana kwa roho. Ujue roho ni pysical thing ambayo imebadili form kuwa spirit. Ni kama maji ambayo ni physical, yawaza kubadili form na kuwa steam etc. Inauwezo wa kuwa ndani mwa mtu ambapo mwili ni physical kwa sababu nayo ni physical in a changed form.

iv. Roho ikitoka kwenye mwili ina option nyingi. Moja ni kwamba inaweza kukaa duniani ikiriranda randa hadi ipate mwili wa kuingia ili izaliwe upya yaani re carnation au ahera( nether world) au mbinguni ambapo level hizi zinaitwa planes.

v. Roho itakaa kwenye plane kutegea spiritual level yake ambayo inategemea matendo yake hapa duniani. The higher spiritual level is saint hood, while the lowest is ghost( demons, devils, and negative energies)
 
Safi sana. Hii idea sikuwahi kuifikiri. Umeiongezea maarifa
 
Kwa hiyo imani yako ni uongo?
Huwezi kuonesha kwa sababu sijasema. Ni maneno tu ulinilisha ili ujivike uhalali wa kunihusisha kwenye suala lako la kutokujua kwa nini mungu hivi mara vile ambalo nimeshakuambia tusihusishane.

Kila mtu apambane na suala lake.
Hapa napo utanilisha maneno mengine ili uibue hoja nyingine ili huu mjadala upate kuendelea. [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Ni mjadala wa kipuuzi kulishana maneno wacha niutue.
 

Kama kweli ungekuwa unataka kila mtu apambane na suala lake, usingeposti habari za imani yako hapa.

Ukiposti habari za imani yako hapa, unaihubiri kwa namna moja au nyingine. Unasema inafaa kufuatwa, kwa sababu, angalau wewe unaifuata.

Ndiyo maana mtu anapata uhalali wa kusema kwamba, ukiposti habari za imani yako hapa, unasema kwamba imani yako ni ukweli.

Kwa nini uposti imani yako hapa kama si ya kweli?

Unajibalaguza. Hujajibu swali.

Imani yako ni ukweli au uongo?

Mbona unakwepa kujibu swali hili?
 
Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
Al watan... Ipo siku utaelewa.
Hayo mabaya yasipowezekana au yasipokuwepo utajuaje mazuri. Kumbuka unayaita mazuri kwakuwa unayatambua mabaya
 
Al watan... Ipo siku utaelewa.
Hayo mabaya yasipowezekana au yasipokuwepo utajuaje mazuri. Kumbuka unayaita mazuri kwakuwa unayatambua mabaya

Sikumoja siku gani? Una hakika na hilo au unakisia tu kama unavyokisia kuwepo kwa Mungu?

Kwa hiyo Mungu wako alishindwa kuumba ulimwengu ambaouna mazuri tu, mabaya hayawezekanina unayajua mazuri?

Kama mabaya hayapo, kuna mazuri tu, kuna umuhimu gani wa kuyajua haya mazuri na si mabaya?
 
Ubaya na uzuri ni kitu kimoja / like darkness and light /noise and silence..
You can't have one without the other.
Mwanga hutokea gizani.
 
Nimekaa hapa napiga ugali na mlenda na dagaa wakavu huku nasoma hii post yako na nimecheka hadi nimepaliwa...

Jamaa akaniuliza "sasa si hicho kisimu chako cha mchina utakidondoshea kwenye huo mlenda?" Nikamjibu nasoma "vurugu" za jamaa huku mtandaoni jombaa na hakidondoki kitu hapa iwe dagaa au haka ka mchina....

Huwa nasoma post zako maana unaandika kama mashairi hivi na inavutia sana kusoma...

Hiki ndicho nilichokibakiza....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…