Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Ubaya na uzuri ni kitu kimoja / like darkness and light /noise and silence..
You can't have one without the other.
Mwanga hutokea gizani.
Hujajibu swali langu, Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao kuna uzuri lakini ubaya haupo na hauwezekani kuwepo?

Hili ndilo swali langu, ambalo hujalijibu.
 
Umeandika hadithi nzuri, lakini hujajibu swali nililouliza.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani kufanyika?
 
Sasa hapo ndio ugumu wa biblia unapokuja. Yesu ni Mungu lakini Mungu huyo alikufa. Je alipokufa roho yake ilienda wapi?
.
Mungu ni Roho, Yesu ni mwili alimukaa Mungu(roho) hapa duniani ili kutenda yale aliyotenda.
Miili yetu irudiyo mavumbini tuna ahadi ya kufufuliwa siku ya mwisho na kuishi milele. Wa Yesu ulifufuka kama mtangulizi wetu kutuonyesha mfano ulio hai wa ile yetu itakavyofufuka na alipaa nao kuelekea mbinguni.

Huu ni mwili wa utukufu.
 
Umeandika hadithi nzuri, lakini hujajibu swali nililouliza.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani kufanyika?
Umekisia tu kuwa nilikuwa na dhamira ya kujibu chochote hapa au una uhakika?

Nilichoandika ndicho nilitaka kuandika,hayo mengine ni yako wewe...
 
Umekisia tu kuwa nilikuwa na dhamira ya kujibu chochote hapa au una uhakika?

Nilichoandika ndicho nilitaka kuandika,hayo mengine ni yako wewe...
Nani kaongelea dhamira yako? Nani anakisia sasa wewe unayeongelea kwamba nimekisia kuhusu dhamira yako, ambayo siwezi kuijua - na hata nikiiongelea nitakuwa nakisia tu, hivyo wewe kusema nakisia nipointless, ingawa sikuwa naiongelea- au mimi niliyesema fact tu?

Mimi nimesema fact.

Fact ni kwamba hujajibu swali langu.

Au umejibu? Unataka kupinga hiyo fact?
 
Yooote hayo uliyoyaandika nisome andiko gani ili nielewe?
 
.
Hizi tafsiri zilizo mawazo ya hisia zenu zinazojengwa juu ya itikadi ya madhehebu yenu ndio zimekua taabu kuu kwa wale wanaowasikia.
Nafikiri unamzungumzia Samweli na wala siyo Nathan. Biblia inasema kuwa aliyepandishwa kutoka kaburini ni Samweli. Wala haijawahi kutoa ufafanuzi popote wa aya hizi zimhusuzo Samweli.

1 Samweli 28
14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.

15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.
 
Yooote hayo uliyoyaandika nisome andiko gani ili nielewe?
Uelewa wa hili haupo katika mstari mmoja bali kusudi lote la kuandikwa biblia. Soma biblia yote ukiwa umetulia na kumwomba roho wa Mungu akuongoze katika ufahamu/uelewa
 
Uelewa wa hili haupo katika mstari mmoja bali kusudi lote la kuandikwa biblia. Soma biblia yote ukiwa umetulia na kumwomba roho wa Mungu akuongoze katika ufahamu/uelewa
Biblia yote haizunzumzii kitu kimoja tu. Ina mambo mengi. Unaponiambie nisome biblia yote ni kukimbia wajibu wako wa kunifundisha.
Ndio maana Ufunuo wa Yohana hauzungumzi sawa na Injili ya Yohana.
 
Uelewa wa hili haupo katika mstari mmoja bali kusudi lote la kuandikwa biblia. Soma biblia yote ukiwa umetulia na kumwomba roho wa Mungu akuongoze katika ufahamu/uelewa
Mtu anapotaka kujua Yesu alizaliwa mji gani hawezi kusoma biblia yote.
 
Ndio maana adam alipuliziwa pumzi yaani roho. Ova
 
Sasa hapo ndio ugumu wa biblia unapokuja. Yesu ni Mungu lakini Mungu huyo alikufa. Je alipokufa roho yake ilienda wapi?
Lakini kama ilivyoandikwa, mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

Inamaana kwamba kumpenda Mungu kunaendana sana na kutamani kujifunza kutoka kwake, kukubaliana na Neno Lake yaani inakupasa uamini pasipo kutilia shaka yoyote ile. [Hapa inakubidi ulazimishe akili zako za kibinadamu zikubaliane na kilichoandikwa]

Ndipo unaangaziwa mwanga wa kuyaelewa mambo ambayo akili ya kawaida ya kibinadamu ni ngumu kuyaelewa. Yaani kwa kifupi unavuviwa hali ya UFAHAMU wa kiroho.
 
This fellow is simply ignorant of many things, whetever he said about soul is stark nonsense. He is fallacious in his arguments. Quran is just a story book,
 
Biblia yote haizunzumzii kitu kimoja tu. Ina mambo mengi. Unaponiambie nisome biblia yote ni kukimbia wajibu wako wa kunifundisha.
Ndio maana Ufunuo wa Yohana hauzungumzi sawa na Injili ya Yohana.
.
Biblia inazungumzia kusudi lililoshikana nalo ni kuumbwa kwa ulimwengu na vyote vilivyomo, kuanguka kwa mtu/binadamu , ukombozi wa mtu alieanguka, njia Mungu alizo/anazopitia hata ukamilifu.

Mistari mingi ya biblia imelibeba/ficha hili kusudi ndio maana biblia haisomwi tu kama gazeti ila inasomwa ndani ya mstari kuweza kufunua kusudi la kuandikwa kwake.
 
Wewe ni mkristo wa dhehebu gani??
 
Roho ndio mtu mwenyewe halisi...Mwili ni kama jumba tu (housing) la roho ya binadamu..Mtu halisi yupo ndani ya mwili.
 
Binadamu anapokufa huenda kukusanywa na jamaa ya watu wake waliotangulia,,,mahali pa kusubiri katika ulimwengu usioonekana..Ona mfano wa Musa au Ndugu yake haruni....Torati 32:48-50
 
Roho ni nguvu ya uhai ya viumbe hai. Kila kiumbe hai kina roho ya uhai na kinapokufa maana yake uhai katika huo mwili umetoweka.

Tofauti ya viumbe wengine wenye uhai na mtu ni moja kuu. Mtu ana nafsi na hii ndio utu yaani tabia ya Mungu ndani yake. Nafsi ni tabia ya roho ambayo ndio uungu. Wanyama na mimea wana roho ya uhai lakini hawana utu yaani nafsi.

Roho haifi ila huhama na mwili wa damu na nyama ulioachwa na roho hurudi mavumbini bali nafsi ya ule mwili humrudia muumba ambae ndie asili yake
 
Binadamu ana sehemu tatu,,MWILI,,NAFSI NA ROHO...Nafsi inajumuisha eneo lote la ufahamu(mawazo, maamuzi, dhamira na hisia) ila nafsi imefungamana na Roho ya binadamu.

Kitabu cha Ayubu 38:36
"Je! ni nani alietia hekima moyoni?
Au ni nani alietia ufahamu rohoni?" Wengi wametatanishwa na swala kwamba mawazo yanaanzia kichwani au moyoni?? Hata Albert Einstein nimemwona ktk utata huu..Binadamu yuko asilimia kubwa ktk roho.

Na yapo maisha mengine baada ya haya katika reality..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…