Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Kama utapenda pitia Ufunuo1:10-18 utamwona YESU akiwa kwenye uhalisia wake kamili, hapa alimtokea mmoja wa mitume wake 12 aliekuwa ametupwa kwenye kisiwa kimoja nchini uturuki.

Yesu ni zaidi ya unavyoweza kufikiri au kukadiria hana level za chini kama unavyoona.Level yake iko beyond our imagination.
 
4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.Mwana ni Mkuu kuliko Malaika

5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote,Ndiwe mwanangu,Mimi leo nimekuzaa?Na tenaMimi nitakuwa kwake baba,Na yeye atakuwa kwangu mwana?

6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.

7 Na kwa habari za malaika asema,Afanyaye malaika wake kuwa pepo,Na watumishi wake kuwa miali ya moto.

8 Lakini kwa habari za Mwana asema,Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele;Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi;Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

10 Na tena,Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,Na mbingu ni kazi za mikono yako;

11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;Nazo zote zitachakaa kama nguo,

12 Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,Na miaka yako haitakoma.

13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,Uketi mkono wangu wa kuumeHata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Waebrania1:5-14. Ukielewa utamwelewa Yesu.
 

Naomba ujibu kwa hoja, usilete mahubiri.

Jibu swali ninalouliza, usijibu ambayo sijauliza huku ambalo nauliza hujibu.

Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
 
anajiamini hapangiwi
 
Utajuaje kwamba Mungu anaumba apendavyo na si kwamba hayupo umedanganywa tu ikiwa huwezi hata kuelezea kwa nini kapenda ubaya uwezekane badala ya kupenda ubaya usiwezekane?
Nimedanfanywa nani?Hivi nikuulize watu karibu wengi hakuna anaependa kufa lakini tunakufa,hivi huoni kama kuna nguvu inakulazimisha ufe japo hupendi
 
anajiamini hapangiwi
Hujajibu swali, sina hakika hata kama umelielewa swali.

Kama Mungu wa Biblia yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, aliyeumba mbingu na nchi, ambaye alikuwa na uwezo wa kuuumba ulimwengu vyovyote alivyotaka, kwa nini kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya yawepo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo?

Hujajibu swali.
 
Nimedanfanywa nani?Hivi nikuulize watu karibu wengi hakuna anaependa kufa lakini tunakufa,hivi huoni kama kuna nguvu inakulazimisha ufe japo hupendi
Kama kuna nguvu inanilazimisha kufa,hilo halithibitishi Mungu yupo.

Kwa kweli, kifo kinaonyesha Mungu hayupo zaidi ya kinavyoonyesha Mungu yupo.

Kwa nini?

MnasemaMungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Kama ni kweli, Mungu huyu hapendi kuona viumbe wake, wanateseka.Hapendikuona wanaopendana wanatengana.

Kifo kinaleta mateso mengi, kinatenganisha wanaopendana. Bila shaka wewe una watu katika familia yako waliofariki ungependa wawepo leo.

Sasa basi, inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaumba ulimwengu ambao kifo kinawezekana kuwepo, wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?

Hujajibu swali hili.
 
Mkuu Al-Watan Mungu aliumba ulimwengu ambao binadamu anaweza kuishi kwa maamuzi [free will] anaweza akachagua kuishi katika ulimwengu usio na mabaya kabisa wala kupata mahitaji kwa jasho Au kuishi katika ulimwengu huo huo kukiwa na mazuri na mabaya kwa pamoja.

Kwa hio ile free will aliopewa binadamu alichagua..Binadamu ni mali ya Mungu hivyo Mungu alimleta duniani kwa malengo yake.

Mungu Alikuwa na plan yake kuanzia mwanzo ila binadamu kwa kuwa na free will aliamua kuishi nje ya plan, kwa hio kama asingeamua tofauti basi hili swali lako lisingekuwepo leo kwa sababu dunia isingekuwa na shida. Angalia mwanzo wa maisha ya binadamu kwenye bustani ya Eden iliokuwa Iraq.
 
Unaelewa kwamba swali nililokuuliza hujalijibu na swali ulilolijibu sijakuuliza?
 
Unaelewa kwamba swali nililokuuliza hujalijibu na swali ulilolijibu sijakuuliza?
Aliumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana kwa sababu,,binadamu anaeishi katika huu ulimwengu amepewa akili na nguvu ya kuyakabili hayo mabaya na kuyashinda...Iko rewards kwa binadamu alieshinda mabaya yanayomzunguka.
 
hakuna mtu atakuambia roho ni nini utadanganywa tu hapa hilo swali limeulizwa karne na karne hata manabii hawakuweza kujibu hilo swali
 
Aliumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana kwa sababu,,binadamu anaeishi katika huu ulimwengu amepewa akili na nguvu ya kuyakabili hayo mabaya na kuyashinda...Iko rewards kwa binadamu alieshinda mabaya yanayomzunguka.
Na wanyama ambao hawana akili, Mungu anafurahia kuona wanakufa kwa matetemeko ya ardhi, mioto, mafuriko, magonjwa?

Na watu ambao hawajapewa akili ya kuyashinda mabaya je? Mungu atawahukumu kwa kuwa hajawapaakili ya kuyashinda mabaya?

Huyo Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kwa nini ampe kiumbe wake mabaya mengi sana ili kuja kumpa reward? Angempa mazuri tu katikaulimwengu ambao mabaya hayapo angepungukiwa nini?
 
Wewe ni mkristu jina ambaye hujatambua mafundisho msingi ya dini yako, katika ukristo kuna fumbo la utatu mtakatifu, yaani mungu mmoja katika nafsi tatu. Kwa Yesu ilikuwa ni Mungu kujidhihirisha kwetu katika umbo la mtu, hata alivyokufa roho yake ilibaki kuwa hai na haikufa. Pia injili ya John inatamka wazi kuwa Yesu ni Mungu.
 
Binadamu amepewa ulimwengu autawale na atawale viumbe wengine, kwa hio wanyama au viumbe vingine vikiwa na shida binadamu ndio mwenye wajibu kuviangalia kwa maana hio rewards ya mahangaiko ya binadamu inatoka kwa hao viumbe pale anapotunza mazingira na kuwatunza miongoni mwa hao viumbe.

Kwa hio Mungu amemuumba binadamu na mazingira yanayomzunguka na amempa nyenzo zote zinazofaa kuyatawala. Zaidi shida ni Kitu cha kusadikika tu labda ambazo wewe unaona hazina suluhisho tu.
 
Binadamu ana uwezo wa kuzuia tetemekola ardhi lisiue wanyama?

Shida nikitu cha kusadikika tu?

Sasa mbona mtu anahukumiwa dhambi kwa kufanya mabaya ambayo yanamletea shida mwingine?
 
Binadamu ana uwezo wa kuzuia tetemekola ardhi lisiue wanyama?

Shida nikitu cha kusadikika tu?

Sasa mbona mtu anahukumiwa dhambi kwa kufanya mabaya ambayo yanamletea shida mwingine?
Sasa hivi kuna vifaa vya kupredict tetemeko,,dhoruba na vimbunga na kwa sababu ya akili alio nayo binadamu kuna aina ya ujenzi wa nyumba za kujenga maeneo ya matetemeko e.g Japan kwa hio ukiangalia utaona kwa asilimia nyingi binadamu ameyamudu na kuyajua mazingira yake yote ndio maana unaona research facilities maeneo mbalimbali.

Hii yote ni kutumia akili aliotupa Mwenyezi kuyatawala mazingira yote
 
Sasa hivi, na hao wote waliokufa na kuumia vibaya sana kabla je?

Mungu kwa nini kachia muda wote huo wafe kwa ukatili sana wakati alikuwa na uwezo wote,ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao hauna ubaya wowote?
 
Shida kama ina solution sio shida.Ukiumwa unaenda hospital, ukiwa huna pesa unazitafuta, ukimtamani mwanamke unamtongoza,,akinikataa najipanga vizuri au natongoza mwingine, njaa nakula.

Yaani kila kitu kilicho shida kina solution. Na shida unayoona kubwa unaweza mueleza mtu akaona inaweza kusoviwa kirahisi.
 
Kwanini Mungu mjuzi wa yote mwenye uwezo wote na ujuzi wote atengeneze shida na solution? Kwa nini asitengeneze ulimwengu ambao hauna shida?

Kisha, solution ya kifo ni nini? Kifo ni shida inayotenganisha wanaopendana, hawapendi kutenganishwa ndiyo maana wanalia kwenye misiba.

Solution ya kuzui kifo ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…