Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Unaweza kuthibitisha kuwa jua litatoka kesho?Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaweza kuthibitisha kuwa jua litatoka kesho?Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Mkuu Alwatan habari yako, mkuu huwezi jifunza jambo kwa watu wasio na ujuzi na jambo hilo zaidi itakuwa ni mabishano yasiyo na tija, michango itolewayo humu kuhusiana na swali lako haikidhi kiu yako ya jibu.Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
Mwanachuo gani kashawahi kujibu swalihilo? Wapi?Mkuu Alwatan habari yako, mkuu huwezi jifunza jambo kwa watu wasio na ujuzi na jambo hilo zaidi itakuwa ni mabishano yasiyo na tija,michango itolewayo humu kuhusiana na swali lako haikidhi kiu yako ya jibu.
Nilikushauri na pia narudia tena kama unataka elimu kuhusu majambo haya haswa kwa upande wa uislam basi wako wanachuoni wenye elimu juu ya haya mambo, kinyume cha hapo ni mabishano yasiyo na tija na ukomo pia
Kwa "kuthibitisha" una maana gani?Unaweza kuthibitisha kuwa jua litatoka kesho?
Binadamu wanachagua kama tetemeko la ardhi litokee au lisitokee?Binadamu tumeumbiwa uhuru wa kuchagua na kutenda. Unaweza ukachagua kufanya ubaya au wema ila vyote vina matokeo yake.
Hujaelewa swali.Kosa lako mkuu ni kutokujua Maandiko maana iko wazi kabisa kwamba hapo mwanzo ulimwengu ulikuwa hauna baya lolote hata kifo hakikuwepo na ndio maana Mungu alimuambia Adam kuwa siku utakapolishika hili tunda na kulila hakika utakufa(Mwanzo 2:16-17) na kifo kimeingia duniani baada ya mwanadamu kuasi sheria ya Mungu na kulila lile tunda la ujuzi wa mema na mabaya hivyo basi kifo sio mpango wa Mungu bali ni matokeo ya uasi wa mwanadamu dhidi ya sheria ya Mungu na kwanzia baada ya huo uasi dhidi ya sheria takatifu ya Mungu ndipo mwanadamu alipoanguka dhambini ule utukufu wa Mungu aliokuwa nao ukamtoka (Mwanzo 3:7) hapo ndipo wanadamu tukaanguka katika dhambi tukawa watumwa wa sheria ya dhambi na kifo yaani kiufupi ni kuwa wanadamu wote waliokuja ulimwenguni baada ya uasi wa Adamu na Hawa walijikuta chini ya sheria ya dhambi yaani kwao dhambi iko ndani yao wired in their genes na pia ni lazima wafe maana wazazi wao waliasi yaani Adamu na Hawa.
Kwa hiyo mabaya haya ulimwenguni si mpango wa Mungu bali ni matokeo ya Uasi wa mwanadamu dhidi ya sheria ya Mungu na ndio maana tunakufa mkuu na si vinginevyo.
Mkuu basi subiri, muda si mrefu utakutana na watakao kujibu kwa kina kuhusu swali lako.Mwanachuo gani kashawahi kujibu swalihilo? Wapi?
Nataka a clear cut answer, si mahubiri.
Muda simrefu una dakika ngapi? Nitakutana nao majina yao kina nani? Una uhakika na hiliau unakisia kisia tu kama unavyokisia kisia Mungu yupo?Mkuu basi subiri, muda si mrefu utakutana na watakao kujibu kwa kina kuhusu swali lako.
Yani una uhakika ya kuwa jua lazima litachomoza kesho?Kwa "kuthibitisha" una maana gani?
Nikishindwa kuthibitisha hilo litathibitisha Mungu yupo?
Nikisema sina hakika, hilo linathibitisha Mungu yupo?Yani una uhakika ya kuwa jua lazima litachomoza kesho?
Kama wewe kutokuwa na akili haithibitishi kwamba Mungu yupo,na pia nawe utambuwe haya maswali yako ya "kwanini hivi na isiwe vile" hayafanyi kuwa hakuna mungu vinginevyo uthibitishe kutokuwepo kwake,na kama utasema haiwezekani kuthibitisha kitu kisichokuwepo basi tambua huwezi kuwa na uhakika kuwa hicho kitu hakipo hata kama kweli hakipo kiuhakika.Hata kamasina akili, hilo halithibitishi kwamba Mungu yupo.
Zaidi, linaonesha Mungu hayupotu.
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote asingeumba ulimwengu ambao una kiumbe asiye na akili.
Sawa, na kama hakipo, kushindwa kuthibitisha kwamba hakipo hakuthibitishi kwamba kipo.Kama wewe kutokuwa na akili haithibitishi kwamba Mungu yupo,na pia nawe utambuwe haya maswali yako ya "kwanini hivi na isiwe vile" hayafanyi kuwa hakuna mungu vinginevyo uthibitishe kutokuwepo kwake,na kama utasema haiwezekani kuthibitisha kitu kisichokuwepo basi tambua huwezi kuwa na uhakika kuwa hicho kitu hakipo hata kama kweli hakipo kiuhakika.
Uthibitisho haufanyi kitu kiwepo bali unatoa uhakika wa kuwa kitu hicho kitu kipo,hata watu wasipothibitisha kama hicho kitu basi kitaendelea tu kuwepo.
Ndio mpango wake wa kwanza ulishindwa na hii ni kwa sababu alimpa mwanadamu free will uhuru wa kuchagua na mwanadamu akachagua kutokumtii na kumheshimu na hivyo basi akaandaa mpango mwingine sasa wa ukombozi wa mwanadamu ambapo ilimbidi Yeye sasa aje kumkomboa mwanadamu kutoka katika mauti na alifanya hivi kwa kuuvaa mwili wa mwanadamu na Akaja kumfia mwanadamu na kumkomboa kutoka katika kifo.Hujaelewa swali.
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani kabisa kuwepo?
Unaposema mabaya si mpango wa Mungu, ina maana Mungu mpango wake umeshindwa? Mungu kashindwa kufanya alichotaka?
Mpango wake wa kwanza ulishindwa?Ndio mpango wake wa kwanza ulishindwa na hii ni kwa sababu alimpa mwanadamu free will uhuru wa kuchagua na mwanadamu akachagua kutokumtii na kumheshimu na hivyo basi akaandaa mpango mwingine sasa wa ukombozi wa mwanadamu ambapo ilimbidi Yeye sasa aje kumkomboa mwanadamu kutoka katika mauti na alifanya hivi kwa kuuvaa mwili wa mwanadamu na Akaja kumfia mwanadamu na kumkomboa kutoka katika kifo.
Kama unataka kuelewa ni vizur ungesikiliza kwanza, hizo dhana kinzani zilishaelezewa vizur sana sio lazima nirudie tena ndio mana nikakwambia usikilize hiyo clip uniulize swali, Hakuna ubishi kwa roho ipo na ikiondoka ndio kifo huja (like an exchange).Hujajibu swali, na huyo Dr. siwezi kuangalia video yake sasa hivi.
Mungu wako ambaye humuelewi kiasi cha kuweza kumuelezea vizuri, unawezaje kumtofautisha na uongo mwingine wowote tu ambao nao haueleweki kiasi cha kuweza kuelezeka vizuri?
Na kamahuwezi kumtofautisha huyu Mungu wako kwa kumuelezea vizuri,sawa na uongo mwingine tu ambao huwezikuuelezea vizuri, kwa nini Mungu wako huyu naye asiwe uongo tu?
Sasa mkuu Mungu angemnyima mwanadamu uhuru wa kuchagua tu wewe na mimi si tungekuwa tu ma robot Alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua kumtii au kutokumtii hii ndio free will ambayo inatufanya mimi na wewe tuwe wanadamu bila hiyo sisi tungekuwa hatuna tofauti na roboti.Mpango wake wa kwanza ulishindwa?
Mungu alishindwa?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote atashindwa vipi?
Mungu alishindwa kumpa mwanandamu uhuru wa kuchagua mazuri tu katikaulimwengu ambao hauna mabaya?
Mbona mwili ni wangu lkn pia sina maamuzi nao? Mfano naweza nikaumia na kuvunjika au kupata jeraha lolote kwenye mwili wangu bila idhini yangu?Yeah!!
Ndio maana huna uamuzi nayo. Wala hujui habari zake. Ikiamua kutoka inatoka na wala huwezi kuizuia.
Ukisema huna uhakika hiyo haifanyi jua lisichomoze kesho,kwa maana linaweza likachomoza au lisichomoze. Na hivyo hivyo hata kama watu wanaoamini mungu kushindwa kuthibitisha haifanyi kuwa hakuna mungu,hivyo kama mungu yupo basi yupo tu na kama hayupo basi hayupo.Nikisema sina hakika, hilo linathibitisha Mungu yupo?
Sipo katika sehemu ninayoweza kusikiliza,na wewe unaweza kujenga hoja kutoka ulichosikiliza kutokana na hoja zangu.Kama unataka kuelewa ni vizur ungesikiliza kwanza, hizo dhana kinzani zilishaelezewa vizur sana sio lazima nirudie tena ndio mana nikakwambia usikilize hiyo clip uniulize swali, Hakuna ubishi kwa roho ipo na ikiondoka ndio kifo huja (like an exchange).