Afisa Mteule Drj 2
JF-Expert Member
- Mar 21, 2017
- 3,865
- 4,506
Kwa nyie wa dar roho zenu zitarudi kwa mungu wenu wa dar bashite
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Avatar yako inamuonesha jini,wewe hayo mambo ya mungu unayajulia wapi?Roho ni sehemu ya Super Natural power.
Ni sehemu ya Mungu. Hivyo haionekani na haitakuja kuonekana.
Ukifa Roho hurudi kwa Mungu kwani ni sehemu yake. Wakati Mwili hurudi mavumbini kwani mwili ni sehemu ya Mavumbi.
Mbona hata sasa hatuna uhuru wa kuchagua kurudi nyuma katika muda? Ningetaka kurudi 1982 nikae na wapendwa fulani waliofariki, lakini siwezi.Sasa mkuu Mungu angemnyima mwanadamu uhuru wa kuchagua tu wewe na mimi si tungekuwa tu ma robot Alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua kumtii au kutokumtii hii ndio free will ambayo inatufanya mimi na wewe tuwe wanadamu bila hiyo sisi tungekuwa hatuna tofauti na roboti.
Kuhusu Yeye kushindwa hilo swala halina mashiko kwa sababu mpira haukuwa miguuni kwake bali ulikuwa kwenye miguu ya Adamu na Hawa kwamba wamtii waishi milele au wamkaidi wafe plain and simple.
Allah alishaumba hivyo-malaika, kama nilivyokueleza, Mwanadam ni 'another best creation' na Allah baada ya kumuumba mwanadamu alisema 'Hakika amemuumba mwanadam katika umbo lililo bora kabisa;' kabla ya malaika aliumba Majin ambao nao walikuwa na 'free will' lakin hawana umbo!! hao walifanya ufisad Mkubwa katika ardhi akawaondosha na kuwaleta malaika.Umehubiri, hujajibu swali.
Swali bado linasimama, kwa kuwa halijajibiwa.
Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
Hujajibu swali.
Mkuu huwa mara nyingi nakusoma, hii ndio hoja yako kuu,na kwakweli ndio hoja ya msingi kwa kila mwanafunzi aliyekamilika "huru" ajifunzae au atakaye kuzijua KWELI KUU za Mungu....nami lilikuwa swali langu la kwanza kabisa,,,,,, Kwanini Mungu muweza yote aruhusu kuwepo huu ulimwengu mbaya wenye vifo, magonjwa nknk.Hujajibu swali.
Kamakuna Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, mwenye upendo wote, alikuwa na uwezowakuumba ulimwengu vyovyote alivyotaka, aliwezakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo, hakuumba ulimwengu huo.
Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniilhali yeye ni mwenye uwezowote, ujuzi wote na upendo wote?
Hujajibu swali hili.
Na jua linaweza kupiga supernovae leo lisichomoze kesho.Ukisema huna uhakika hiyo haifanyi jua lisichomoze kesho,kwa maana linaweza likachomoza au lisichomoze. Na hivyo hivyo hata kama watu wanaoamini mungu kushindwa kuthibitisha haifanyi kuwa hakuna mungu,hivyo kama mungu yupo basi yupo tu na kama hayupo basi hayupo.
Sasa wewe umeshindwa kuthibitisha kuwa jua litachomoza kesho lakini hiyo haifanyi usiamini kuwa jua halitachomoza kesho ila wewe unaona hawawezi kuthibitisha kuwepo kwa mungu hivyo ni uthibitisho kuwa mungu hayupo.
Hoja ya kuzaliwa bila baba isikusumbue sana, yupo Adam ambaye hana baba wala mama lakin sio Mungu, kwenye biblia kuna mtu anaelezewa kuwa hana baba hana mama hana mwanzo hana mwisho huyo ndio unapaswa kumshangaa sana zaid ya Yesu ambaye anajieleza Mwaenyewe kwenye Yoh.17 : 3ntabhaligwa uliwahi kumuona binadamu aliezaliwa na mwanamke tuu?? Ambapo hakutokana na sex ya mume na mke??
Hujajibu swali,unakubali tu kwamba hujui jibu.Allah alishaumba hivyo-malaika, kama nilivyokueleza, Mwanadam ni 'another best creation' na Allah baada ya kumuumba mwanadamu alisema 'Hakika amemuumba mwanadam katika umbo lililo bora kabisa;' kabla ya malaika aliumba Majin ambao nao walikuwa na 'free will' lakin hawana umbo!! hao walifanya ufisad Mkubwa katika ardhi akawaondosha na kuwaleta malaika.
Anayeendeshwa kwa kanuni si Mungu.Mkuu huwa mara nyingi nakusoma, hii ndio hoja yako kuu,na kwakweli ndio hoja ya msingi kwa kila mwanafunzi aliyekamilika "huru" ajifunzae au atakaye kuzijua KWELI KUU za Mungu....nami lilikuwa swali langu la kwanza kabisa,,,,,, Kwanini Mungu muweza yote aruhusu kuwepo huu ulimwengu mbaya wenye vifo, magonjwa nknk.
Kwa bahati mbaya sijawahi jibiwa na yeyote yule, achilia mbali kuzunguka ktk madhehebu mengi na kujifunza kwao. Haikukatisha kiu yangu ya kujifunza....
Kwa haraka nimegundua haya, kwanza sio kweli kwamba Mungu ni muweza wa yote, bali ya Uungu wake tu, mfano, Mungu hawezi sema "uongo" ,hawezi tenda yasiyo haki,, lakini kubwa zaidi naye yuko governed na Principles,, kanuni.
Kwahiyo, sio kweli kwamba, Mungu alifanya vyote alivyovifanya pasi kufuata kanuni fulani za uumbaji, zilifuatwa... na kila kilichoumbwa ni lazima kifuate hizo kanuni za kiungu pia. Kila kiumbe lazima kile ili kiishi, ni kanuni hii, na nyinginezo nyingi.
Kwanini huu ulimwengu uko kama ulivyo leo? Kuvunjwa kwa kanuni zile ambazo zingefuatwa usingekuwa ulivyo leo, na kuvunja kanuni ndiyo hiyo waiitayo dhambi. Kikanuni, mwanadamu alitakiwa ale mbogamboga za kondeni,matunda na nafaka tu, kwa kula nyama na mazao yake mwanadamu anavunja kanuni, hivyo hawezi kuwa salama, mengi ya leo ni uvunjifu wa kanuni.
Nilichosema, Kuna vitu Mungu hawezi kufanya na akivifanya, Uungu wake unamtoka, pia nimesema kuna kanuni zilifutwa ktk uumbaji na viumbe vilitakiwa kuzitii na kinyume chake ni nje ya malengo ya Muumbaji. Sijui kama nimeeleweka Mkuu.
Kutaka kuzijua hizo kanuni, jiulize kwanini kuna nadharia ya namba 7 duniani, tena hata kwa jamii zilizokuwa nje ya mafungamano, nadharia ya damu kama sadaka,,, nknk.
Usichanganye habari mkuu uhuru tuliopewa ni wa kumtii au kutokumtii na ndiyo maana Adamu anapewa sheria kuwa Usile maana siku utakapokula hakika utakufa kwa hiyo Adamu uhuru aliokuwa nao ni wa kuaamua kutokulila au kulitafuna lile tunda.Mbona hata sasa hatuna uhuru wa kuchagua kurudi nyuma katika muda? Ningetaka kurudi 1982 nikae na wapendwa fulani waliofariki, lakini siwezi.
Utasemaje tumepewa uhuru wa kuchagua wakati hatuwezi kurudi nyuma katika muda?
Ukisema kunyimwa uhuru wa kuchagua ni kuwa ma robot, mbona sasa hatuwezi kurudi nyuma katika muda, kwa hiyo kwa kushindwa kurudi nyuma katika muda tunakuwa ma robot?
Mungu kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kama isivyowezekana kurudi nyuma katika muda?
Kama Yesu mwenyewe ametamka, halafu mtu mwingine akatamka linalopinga hilo , utamwamini nani?Kama utapenda pitia Ufunuo1:10-18 utamwona YESU akiwa kwenye uhalisia wake kamili,,,,hapa alimtokea mmoja wa mitume wake 12 aliekuwa ametupwa kwenye kisiwa kimoja nchini uturuki..Yesu ni zaidi ya unavyoweza kufikiri au kukadiria hana level za chini kama unavyoona.Level yake iko beyond our imagination..
Uungu wake uko kikanuni, yeye Mwenyewe ni kanuni,,,, na kutokuzitii ni kujibomoa.Anayeendeshwa kwa kanuni si Mungu.
Maana ana kanuni zilizo juu yake.
Na kanunihizi zitazaa swali jingine, kwa ninikanuniziwe hizi na si zingine? Zimetoka wapi?
Unajichanganya.Usichanganye habari mkuu uhuru tuliopewa ni wa kumtii au kutokumtii na ndiyo maana Adamu anapewa sheria kuwa Usile maana siku utakapokula hakika utakufa kwa hiyo Adamu uhuru aliokuwa nao ni wa kuaamua kutokulila au kulitafuna lile tunda.
Huo uhuru unaouongelea wa kwenda nyuma ya wakati yaani Time travel mwanadamu hakupewa huo uwezo.
Kanuni zake za msingi ni zipi kwa mfano, nitajie tano muhimu.Uungu wake uko kikanuni, yeye Mwenyewe ni kanuni,,,, na kutokuzitii ni kujibomoa.
Hakuna hata kitu kimoja kinachojisimamisha na kikaendelea kuwepo bila ya kwanza kutii kanuni, hii ni kanuni ya asili ya kuendelea kuwepo.
Hata nyumba, magari, wanyama, mawe nk hutii kanuni fulani ili existence yao iwepo,
Umeshindwa kujibu swali langu,,,,,kuhusu kumwamini nani ktk biblia ni suala gumu hasa kwa upande wako,,,maana tayari una dhamira na mtazamo wako wa kipekee....Una namna unavyomwelewa Yesu na unaamini ndio 3.14 yako.Hoja ya kuzaliwa bila baba isikusumbue sana, yupo Adam ambaye hana baba wala mama lakin sio Mungu, kwenye biblia kuna mtu anaelezewa kuwa hana baba hana mama hana mwanzo hana mwisho huyo ndio unapaswa kumshangaa sana zaid ya Yesu ambaye anajieleza Mwaenyewe kwenye Yoh.17 : 3
Kwanza suala la uwepo wa mungu linahitaji imani na ndiyo maana imeelezwa kwa atakaye amini atapata nini na atakayeamua kutokuamini atapata nini. Hivyo utaona suala zima la mungu linahitaji imani na si kwamba ni jambo liliokosekana uhakika na ndiyo maana watu wakaamua tu kuamini.Sawa, na kama hakipo, kushindwa kuthibitisha kwamba hakipo hakuthibitishi kwamba kipo.
Namna pekee ya kujua kwa hakika kwamba kitu kipo ni kuthibitisha kwamba kipo.
Ndiyo maana nakuuliza, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kama huwezi, huna hakika kwamba yupo.
Kama huna hakika kwamba yupo ,unaweza kuamini yupo wakati hayupo.
Kwanini unafikiri unapoamini yupo, imani yako ni sawa, yupo, na imani yako si potofu kwamba unaamini yupo wakati hayupo?
Kwanza suala la uwepo wa mungu linahitaji imani na ndiyo maana imeelezwa kwa atakaye amini atapata nini na atakayeamua kutokuamini atapata nini. Hivyo utaona suala zima la mungu linahitaji imani na si kwamba ni jambo liliokosekana uhakika na ndiyo maana watu wakaamua tu kuamini.
Na kuna mambo ambayo hufanya mtu aamini uwepo wa mungu na kuna kuna ishara zenye kufanya uone mungu yupo.
Lakini pia mwisho wa siku ndiyo tutaweza kupata uhakika kuwa kumbe ni kweli yupo au kumbe hayupo ilikuwa story,nadhani umenielewa naposema hiyo mwisho.