Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Roho ni sehemu ya Super Natural power.

Ni sehemu ya Mungu. Hivyo haionekani na haitakuja kuonekana.

Ukifa Roho hurudi kwa Mungu kwani ni sehemu yake. Wakati Mwili hurudi mavumbini kwani mwili ni sehemu ya Mavumbi.
Avatar yako inamuonesha jini,wewe hayo mambo ya mungu unayajulia wapi?
 
Sasa mkuu Mungu angemnyima mwanadamu uhuru wa kuchagua tu wewe na mimi si tungekuwa tu ma robot Alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua kumtii au kutokumtii hii ndio free will ambayo inatufanya mimi na wewe tuwe wanadamu bila hiyo sisi tungekuwa hatuna tofauti na roboti.
Kuhusu Yeye kushindwa hilo swala halina mashiko kwa sababu mpira haukuwa miguuni kwake bali ulikuwa kwenye miguu ya Adamu na Hawa kwamba wamtii waishi milele au wamkaidi wafe plain and simple.
Mbona hata sasa hatuna uhuru wa kuchagua kurudi nyuma katika muda? Ningetaka kurudi 1982 nikae na wapendwa fulani waliofariki, lakini siwezi.

Utasemaje tumepewa uhuru wa kuchagua wakati hatuwezi kurudi nyuma katika muda?

Ukisema kunyimwa uhuru wa kuchagua ni kuwa ma robot, mbona sasa hatuwezi kurudi nyuma katika muda, kwa hiyo kwa kushindwa kurudi nyuma katika muda tunakuwa ma robot?

Mungu kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kama isivyowezekana kurudi nyuma katika muda?
 
Umehubiri, hujajibu swali.

Swali bado linasimama, kwa kuwa halijajibiwa.

Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?

Hujajibu swali.
Allah alishaumba hivyo-malaika, kama nilivyokueleza, Mwanadam ni 'another best creation' na Allah baada ya kumuumba mwanadamu alisema 'Hakika amemuumba mwanadam katika umbo lililo bora kabisa;' kabla ya malaika aliumba Majin ambao nao walikuwa na 'free will' lakin hawana umbo!! hao walifanya ufisad Mkubwa katika ardhi akawaondosha na kuwaleta malaika.
 
Mwanadamu ni nafsi na Neno la Mungu liko wazi kabisa ambapo linasema kuwa pumzi ya Mungu ndio iliyomfanya mwanadamu kuwa nafsi hai (Mwanzo 2:7) kwa hiyo bila pumzi ya Mungu mwanadamu anakufa na hii iko wazi kabisa pale ambapo Adamu na Hawa baada ya kula tunda wakajiona kuwa wako uchi na hii ina maanisha kuwa ule Utukufu wa Mungu ambao Adamu na Hawa walikuwa nao uliondoka yaani in short ile Pumzi ya Mungu iliondoka na ndio maana basi binadamu aliweza kufa kwa sababu ile pumzi ya Mungu iliyokuwa inamfanya mwanadamu kuwa kiumbe hai iliondoka.

Kwa hiyo unaposema kuwa roho/nafsi ya mwanadamu haifi inabidi ujiulize kuwa je Mungu alisema uongo pale aliposema Hakika mtakufa? La! bali alisema ukweli kwa sababu hadi sasa binadamu tunakufa na la pili la kujiuuliza ni nani alisema kuwa hakika hamtakufa bali mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya ndipo utakapojua kuwa ni yule baba wa uongo na yeye ndiye aliyedumisha huu uongo kuwa roho haifi.
 
Hujajibu swali.

Kamakuna Mungu, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, mwenye upendo wote, alikuwa na uwezowakuumba ulimwengu vyovyote alivyotaka, aliwezakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo, hakuumba ulimwengu huo.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekaniilhali yeye ni mwenye uwezowote, ujuzi wote na upendo wote?

Hujajibu swali hili.
Mkuu huwa mara nyingi nakusoma, hii ndio hoja yako kuu,na kwakweli ndio hoja ya msingi kwa kila mwanafunzi aliyekamilika "huru" ajifunzae au atakaye kuzijua KWELI KUU za Mungu....nami lilikuwa swali langu la kwanza kabisa,,,,,, Kwanini Mungu muweza yote aruhusu kuwepo huu ulimwengu mbaya wenye vifo, magonjwa nknk.

Kwa bahati mbaya sijawahi jibiwa na yeyote yule, achilia mbali kuzunguka ktk madhehebu mengi na kujifunza kwao. Haikukatisha kiu yangu ya kujifunza....

Kwa haraka nimegundua haya, kwanza sio kweli kwamba Mungu ni muweza wa yote, bali ya Uungu wake tu, mfano, Mungu hawezi sema "uongo" ,hawezi tenda yasiyo haki,, lakini kubwa zaidi naye yuko governed na Principles,, kanuni.

Kwahiyo, sio kweli kwamba, Mungu alifanya vyote alivyovifanya pasi kufuata kanuni fulani za uumbaji, zilifuatwa... na kila kilichoumbwa ni lazima kifuate hizo kanuni za kiungu pia. Kila kiumbe lazima kile ili kiishi, ni kanuni hii, na nyinginezo nyingi.

Kwanini huu ulimwengu uko kama ulivyo leo? Kuvunjwa kwa kanuni zile ambazo zingefuatwa usingekuwa ulivyo leo, na kuvunja kanuni ndiyo hiyo waiitayo dhambi. Kikanuni, mwanadamu alitakiwa ale mbogamboga za kondeni,matunda na nafaka tu, kwa kula nyama na mazao yake mwanadamu anavunja kanuni, hivyo hawezi kuwa salama, mengi ya leo ni uvunjifu wa kanuni.

Nilichosema, Kuna vitu Mungu hawezi kufanya na akivifanya, Uungu wake unamtoka, pia nimesema kuna kanuni zilifutwa ktk uumbaji na viumbe vilitakiwa kuzitii na kinyume chake ni nje ya malengo ya Muumbaji. Sijui kama nimeeleweka Mkuu.

Kutaka kuzijua hizo kanuni, jiulize kwanini kuna nadharia ya namba 7 duniani, tena hata kwa jamii zilizokuwa nje ya mafungamano, nadharia ya damu kama sadaka,,, nknk.
 
Ukisema huna uhakika hiyo haifanyi jua lisichomoze kesho,kwa maana linaweza likachomoza au lisichomoze. Na hivyo hivyo hata kama watu wanaoamini mungu kushindwa kuthibitisha haifanyi kuwa hakuna mungu,hivyo kama mungu yupo basi yupo tu na kama hayupo basi hayupo.

Sasa wewe umeshindwa kuthibitisha kuwa jua litachomoza kesho lakini hiyo haifanyi usiamini kuwa jua halitachomoza kesho ila wewe unaona hawawezi kuthibitisha kuwepo kwa mungu hivyo ni uthibitisho kuwa mungu hayupo.
Na jua linaweza kupiga supernovae leo lisichomoze kesho.

Kushindwa kuthibitisha kitu kama kipo au hakipo hakuoneshi lolote kuhusu kuwapo au kutokuwapo hicho kitu.

Unaweza kushindwa kuthibitisha kitu kipo, kwa kitu ambacho hakipo.

Unaweza kushindwa kuthibitisha kitu kipo, kwa kitu ambacho kipo.

Kwa hiyo kushindwa kuthibitisha kitu hakuna maana yoyote.

Ukitaka kujua kitu kipo, njai pekee ya kujua kwa hakika, ni kuthibitisha kwamba kipo.

Ndiyo maana nakuuliza, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kamaunaweza, thibitisha.

Na ukishindwa, unajuaje kwamba yupo, umeshindwa kuthibitisha tu kwamba yupo, na si kwamba hayupo na umeshindwa kuthibitisha yupo kwa sababu hayupo?
 
ntabhaligwa uliwahi kumuona binadamu aliezaliwa na mwanamke tuu?? Ambapo hakutokana na sex ya mume na mke??
Hoja ya kuzaliwa bila baba isikusumbue sana, yupo Adam ambaye hana baba wala mama lakin sio Mungu, kwenye biblia kuna mtu anaelezewa kuwa hana baba hana mama hana mwanzo hana mwisho huyo ndio unapaswa kumshangaa sana zaid ya Yesu ambaye anajieleza Mwaenyewe kwenye Yoh.17 : 3
 
Allah alishaumba hivyo-malaika, kama nilivyokueleza, Mwanadam ni 'another best creation' na Allah baada ya kumuumba mwanadamu alisema 'Hakika amemuumba mwanadam katika umbo lililo bora kabisa;' kabla ya malaika aliumba Majin ambao nao walikuwa na 'free will' lakin hawana umbo!! hao walifanya ufisad Mkubwa katika ardhi akawaondosha na kuwaleta malaika.
Hujajibu swali,unakubali tu kwamba hujui jibu.

Nimeuliza.

Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?

Hujajibu swali.
 
Mkuu huwa mara nyingi nakusoma, hii ndio hoja yako kuu,na kwakweli ndio hoja ya msingi kwa kila mwanafunzi aliyekamilika "huru" ajifunzae au atakaye kuzijua KWELI KUU za Mungu....nami lilikuwa swali langu la kwanza kabisa,,,,,, Kwanini Mungu muweza yote aruhusu kuwepo huu ulimwengu mbaya wenye vifo, magonjwa nknk.

Kwa bahati mbaya sijawahi jibiwa na yeyote yule, achilia mbali kuzunguka ktk madhehebu mengi na kujifunza kwao. Haikukatisha kiu yangu ya kujifunza....

Kwa haraka nimegundua haya, kwanza sio kweli kwamba Mungu ni muweza wa yote, bali ya Uungu wake tu, mfano, Mungu hawezi sema "uongo" ,hawezi tenda yasiyo haki,, lakini kubwa zaidi naye yuko governed na Principles,, kanuni.

Kwahiyo, sio kweli kwamba, Mungu alifanya vyote alivyovifanya pasi kufuata kanuni fulani za uumbaji, zilifuatwa... na kila kilichoumbwa ni lazima kifuate hizo kanuni za kiungu pia. Kila kiumbe lazima kile ili kiishi, ni kanuni hii, na nyinginezo nyingi.

Kwanini huu ulimwengu uko kama ulivyo leo? Kuvunjwa kwa kanuni zile ambazo zingefuatwa usingekuwa ulivyo leo, na kuvunja kanuni ndiyo hiyo waiitayo dhambi. Kikanuni, mwanadamu alitakiwa ale mbogamboga za kondeni,matunda na nafaka tu, kwa kula nyama na mazao yake mwanadamu anavunja kanuni, hivyo hawezi kuwa salama, mengi ya leo ni uvunjifu wa kanuni.

Nilichosema, Kuna vitu Mungu hawezi kufanya na akivifanya, Uungu wake unamtoka, pia nimesema kuna kanuni zilifutwa ktk uumbaji na viumbe vilitakiwa kuzitii na kinyume chake ni nje ya malengo ya Muumbaji. Sijui kama nimeeleweka Mkuu.

Kutaka kuzijua hizo kanuni, jiulize kwanini kuna nadharia ya namba 7 duniani, tena hata kwa jamii zilizokuwa nje ya mafungamano, nadharia ya damu kama sadaka,,, nknk.
Anayeendeshwa kwa kanuni si Mungu.

Maana ana kanuni zilizo juu yake.

Na kanunihizi zitazaa swali jingine, kwa ninikanuniziwe hizi na si zingine? Zimetoka wapi?
 
Mbona hata sasa hatuna uhuru wa kuchagua kurudi nyuma katika muda? Ningetaka kurudi 1982 nikae na wapendwa fulani waliofariki, lakini siwezi.

Utasemaje tumepewa uhuru wa kuchagua wakati hatuwezi kurudi nyuma katika muda?

Ukisema kunyimwa uhuru wa kuchagua ni kuwa ma robot, mbona sasa hatuwezi kurudi nyuma katika muda, kwa hiyo kwa kushindwa kurudi nyuma katika muda tunakuwa ma robot?

Mungu kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kama isivyowezekana kurudi nyuma katika muda?
Usichanganye habari mkuu uhuru tuliopewa ni wa kumtii au kutokumtii na ndiyo maana Adamu anapewa sheria kuwa Usile maana siku utakapokula hakika utakufa kwa hiyo Adamu uhuru aliokuwa nao ni wa kuaamua kutokulila au kulitafuna lile tunda.

Huo uhuru unaouongelea wa kwenda nyuma ya wakati yaani Time travel mwanadamu hakupewa huo uwezo.
 
Kama utapenda pitia Ufunuo1:10-18 utamwona YESU akiwa kwenye uhalisia wake kamili,,,,hapa alimtokea mmoja wa mitume wake 12 aliekuwa ametupwa kwenye kisiwa kimoja nchini uturuki..Yesu ni zaidi ya unavyoweza kufikiri au kukadiria hana level za chini kama unavyoona.Level yake iko beyond our imagination..
Kama Yesu mwenyewe ametamka, halafu mtu mwingine akatamka linalopinga hilo , utamwamini nani?
 
Anayeendeshwa kwa kanuni si Mungu.

Maana ana kanuni zilizo juu yake.

Na kanunihizi zitazaa swali jingine, kwa ninikanuniziwe hizi na si zingine? Zimetoka wapi?
Uungu wake uko kikanuni, yeye Mwenyewe ni kanuni,,,, na kutokuzitii ni kujibomoa.

Hakuna hata kitu kimoja kinachojisimamisha na kikaendelea kuwepo bila ya kwanza kutii kanuni, hii ni kanuni ya asili ya kuendelea kuwepo.

Hata nyumba, magari, wanyama, mawe nk hutii kanuni fulani ili existence yao iwepo,
 
Usichanganye habari mkuu uhuru tuliopewa ni wa kumtii au kutokumtii na ndiyo maana Adamu anapewa sheria kuwa Usile maana siku utakapokula hakika utakufa kwa hiyo Adamu uhuru aliokuwa nao ni wa kuaamua kutokulila au kulitafuna lile tunda.
Huo uhuru unaouongelea wa kwenda nyuma ya wakati yaani Time travel mwanadamu hakupewa huo uwezo.
Unajichanganya.

Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo kama alivyoumba ulimwengu ambao time travel haiwezekani?

Hujajibu swali hili.

Ukisema habari za uhuru aliopewa mtu,hilo si jibu.

Baba hampi mtoto wake mchanga asiye na akili pevu maziwa na sumu, ili tu mtoto awe na uhuru wa kuchagua kunywa maziwa aishi au sumu afe.

Huyo baba akifanya hivyo, kisha mtoto akachagua sumu na kufa, atashitakiwa na kufungwa.

Sasa kwa nini Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kutupa viumbe vyake maziwa tu, asitupe sumu kabisa, kwa nini katupa maziwa na sumu?

Kwa nini tumuhukumu huyu baba mwenye uwezo wenye mwisho, upendo wenye mwisho na ujuzi wenye mwisho hukumu mbaya, wakati mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote tunamsifu kwa kufanya kitu kile kile?
 
ROHO NI NAFSI INAYOTOFAUTISHA MTU MMOJA NA MWINGNE. ROHO HAIFI, ILA MWILI HUFU.

KATIKA IMANI YA KRISTO, MTU AKIFA ROHO HUENDA MBINGUNI NA KUHUKUMIWA
 
Uungu wake uko kikanuni, yeye Mwenyewe ni kanuni,,,, na kutokuzitii ni kujibomoa.

Hakuna hata kitu kimoja kinachojisimamisha na kikaendelea kuwepo bila ya kwanza kutii kanuni, hii ni kanuni ya asili ya kuendelea kuwepo.

Hata nyumba, magari, wanyama, mawe nk hutii kanuni fulani ili existence yao iwepo,
Kanuni zake za msingi ni zipi kwa mfano, nitajie tano muhimu.
 
Hoja ya kuzaliwa bila baba isikusumbue sana, yupo Adam ambaye hana baba wala mama lakin sio Mungu, kwenye biblia kuna mtu anaelezewa kuwa hana baba hana mama hana mwanzo hana mwisho huyo ndio unapaswa kumshangaa sana zaid ya Yesu ambaye anajieleza Mwaenyewe kwenye Yoh.17 : 3
Umeshindwa kujibu swali langu,,,,,kuhusu kumwamini nani ktk biblia ni suala gumu hasa kwa upande wako,,,maana tayari una dhamira na mtazamo wako wa kipekee....Una namna unavyomwelewa Yesu na unaamini ndio 3.14 yako.
 
Sawa, na kama hakipo, kushindwa kuthibitisha kwamba hakipo hakuthibitishi kwamba kipo.

Namna pekee ya kujua kwa hakika kwamba kitu kipo ni kuthibitisha kwamba kipo.

Ndiyo maana nakuuliza, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kama huwezi, huna hakika kwamba yupo.

Kama huna hakika kwamba yupo ,unaweza kuamini yupo wakati hayupo.

Kwanini unafikiri unapoamini yupo, imani yako ni sawa, yupo, na imani yako si potofu kwamba unaamini yupo wakati hayupo?
Kwanza suala la uwepo wa mungu linahitaji imani na ndiyo maana imeelezwa kwa atakaye amini atapata nini na atakayeamua kutokuamini atapata nini. Hivyo utaona suala zima la mungu linahitaji imani na si kwamba ni jambo liliokosekana uhakika na ndiyo maana watu wakaamua tu kuamini.

Na kuna mambo ambayo hufanya mtu aamini uwepo wa mungu na kuna kuna ishara zenye kufanya uone mungu yupo.

Lakini pia mwisho wa siku ndiyo tutaweza kupata uhakika kuwa kumbe ni kweli yupo au kumbe hayupo ilikuwa story,nadhani umenielewa naposema hiyo mwisho.
 
Sawa, sinatatizo na imani, nina tatizo na imani potofu.

Hata ukipanga mkutano wa kesho, unapanga kwa imani.Unaamini kesho itakuwepo, jua litachomoza,hutafariki usiku wa leo. Hiyo yote ni imani. Bila imani hatuwezi hata kupanga mambo ya kesho.

Sina tatizo na imani, nina tatizo na imani potofu.

Kama imani, Chidi Benz ana imani kwamba ametoa nyimbo na wasanii wakubwa kina Rihanna na 2Pac.

Hiyo ni imani pia.

Na anaweza kukwambia u prove kwamba hajatoa hizo nyimbo, ukashindwa ku prove.

Lakini kumbe imani hiyo ni potofu, Chidi Benz hajatoa nyimbo hizo.

Sasa, utajuaje kwamba imani yako wewe ni sahihi, Mungu yupo, na si imani potofu kama ya Chidi Benz, kwamba unaamini Mungu yupo wakati hayupo?
 
Back
Top Bottom