Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Kama Mungu hana ithibati, utajuaje kwa uhakika kwamba yupo na si hadithi tu?
Habari yafooo mkuu.
Kama nilivotangulia kusema hapo mwanzoni Imani haina ithibati. Imani ni kubwa kuliko sayansi, sayansi inajihusisha na vitu vyenye ithibati pekee.
 
Kutokuonekana kwake na kutothibitika kwake ndiko kunamfanya awepo.

Yapo mambo ambayo kutokuwepo kwayo ndipo uwepo wao ulipo
Kinachofanya ukubali hili japo halionekani wala kuthibitika na usiamini uongo ambao hauonekani wala kuthibitika ni nini?
 
Habari yafooo mkuu.
Kama nilivotangulia kusema hapo mwanzoni Imani haina ithibati. Imani ni kubwa kuliko sayansi, sayansi inajihusisha na vitu vyenye ithibati pekee.
Hujajibu swali nililouliza, ulilojibu sijauliza.

Nikikwambia nyumbani kwako ukumbini mwako ni makao makuu ya Umoja wa Mataifa na wewe ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaendesha kikao sasa hivi utaamini?
 
Kuna mtu kasema roho ni sehemu ya Mungu, kwa hiyo Mungu yupo ndani yangu, nikipata shida nae anapata, njaa magonjwa tunashirikiana, imekaaje?
 
"Na wanakuuliza kuhusu roho?, waambie roho ni katika mambo ya Mola wako mlezi na nyie hamkupewa elimu ya roho isipokuwa kidogo"
~Qur'an
Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
 
Hakuna utata wowote wapi roho inaenda baada ya kifo. Biblia takatifu imetoa ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo. Wanaosema kuna utata au wanaoleta hoja tofauti na Biblia hivyo yote ni kazi ya Shetani kuupotosha ukweli. Someni Biblia mkiongozwa na roho wa Bwana mtaelewa vema.
Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
 
Kama Mungu yupo, Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, Mungu huyu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani, kaumba huu ambao mabaya yanawezekana?
Unataka kumpangia Mungu cha kuumba? Yeye kaamua kuumba hivi angeumba kama unavyotaka ungeuliza pia kwa nini hajaumba hivi.
Alafu kuniuliza mimi swali la 'kwa nini...' Huku ukihusisha nafsi nyingine isiyo mimi hilo swali kwangu ni irrelevant.
 
Hivi wakati yai la mwanamke linapoungana na mbegu ya mwanaume ni wakati huo roho inashuka kutoka kwa Mungu na kuanzisha maisha au maisha yanajianzisha yenyewe? Na kama inashuka kutoka kwa Mungu, zipo aina moja au kuna ya kike na kiume? Ya kizungu, kiafrika, kichina nk. Anatuma nyingine inaazisha maisha ya akili finyu na akili ya kutisha, mtoa hoja mimi sina jibu, ila kinachokufanya uishi ndio roho ilipotaka kwangu ni utata
Mpaka sasa hakuna aliyeweza kuthibitisha uwepo wa roho wala Mungu.
 
Unataka kumpangia Mungu cha kuumba? Yeye kaamua kuumba hivi angeumba kama unavyotaka ungeuliza pia kwa nini hajaumba hivi.
Alafu kuniuliza mimi swali la 'kwa nini...' Huku ukihusisha nafsi nyingine isiyo mimi hilo swali kwangu ni irrelevant.
Si habari ya kumpangia. Ni habari ya kutafuta logical consistency.

Wewe unayesema yeye kaamua kuumba hivi, wakati huwezi kuelezea sababu, huelewi sababu. Kama huelewi sababu humuelewi. Kama humuelewi huelewi unachoamini. Kama huelewi unachoamini unaweza kuamini kitu ambacho hakipo.

Nakuuliza wewe swali la kwa nini kuhusu Mungu huyu kea sababu unamuamini.

Ukishindwa kujibu huelewi unachoamini.
 
Je kuna maisha baada ya kifo? Ujue sijui sielewi haya mambo kila MTU anasema lake
 
Si habari ya kumpangia. Ni habari ya kutafuta logical consistency.

Wewe unayesema yeye kaamua kuumba hivi, wakati huwezi kuelezea sababu, huelewi sababu. Kama huelewi sababu humuelewi. Kama humuelewi huelewi unachoamini. Kama huelewi unachoamini unaweza kuamini kitu ambacho hakipo.

Nakuuliza wewe swali la kwa nini kuhusu Mungu huyu kea sababu unamuamini.

Ukishindwa kujibu huelewi unachoamini.
Yaani ikishakuwa namuamini ndio nijue sababu gani kafanya hivi na sababu gani hakufanya hivi?
Huwezi kuniuliza mimi kwa nini fulani kafanya/hakufanya hivi.
Kuamini nisichokielewa/kisichokuwepo ni hali yangu wacha nipambane nayo
Kutokujua kwa nini mungu hajaumba hivi au vile hilo ni tatizo lako pambana nalo mwenyewe. Tusihusishane ebo!
 
Ungebaki kwako na imani yako, imani ingebaki kuwa yako.

Ukija JF na kusema hii ni imani yako, na huu ndiyo ukweli, tayari ushatoka kwenye mipaka ya imani yako na kuingia kwenye mahubiri kwamba imani yako ni kweli.

Ukishasema kwamba imani yako ni kweli, unahitajika kujibu maswali na kuitetea.

Wewe unasema imani yako ni kweli halafu huwezi kuitetea, huwezi kujibu maswali.

Kwa sababu imani yako si kweli.

Ni utunzi tu wa watu.
 
Back
Top Bottom