Roho ya umauti

Roho ya umauti

karma alvin

Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
51
Reaction score
8
Habar zenu wanajamvi.

Mimi nimekua na tatizo la kutaka kujiua mara kwa mara.

Ninapoishi nakaa kwa ndugu yangu, huyu ndugu yangu amekua na tabia ya kuninyanyasa na saa ingine kunidhalilisha mbele za watu, pia siku hizi amekua anapenda sana kuniuliza kama mimi ni taira au mzima hii hali imenichosha sana sitamani kuendelea kuishi hapa duniani ndo hii hali ya kutaka kujiua inapojia kitu baya ni kwamba nina mtoto haya mawazo yakinijia huwa natamani kujiua mimi pamoja na mtoto sababu naogopa nikimuacha atapata shida sana.

NAOMBENI MNISAIDIE HATA KWA MAWAZO NIWEZE KUKABILIANA NA HII HALI MAANA IMEKUA IKINIANDAMA MARA KWA MARA.
 
Mkuu kwanza pole kwa yote. Me nakushauri hapo sio sehemu sahihi kwako, hama hapo ikiwezekana hama mkoa nenda mbali na huyo ndugu yako, suala la kujiua ni kupoteza matumaini na kuvunjika moyo, wake up timiza malengo yako na muandalie future nzuri mtoto wako just know that wewe ndio mtu pekee anaekutegemea, muonyeshe njia ya maisha...never give up
 
Nimeumia sana. usikate tamaa hayo ndiyo maisha. kumbuka kujiua ni dhambi isiyo sameheka ni PM tuongee vizuri ninakamradi ka ufugaji kuku hakana usimamizi mzuri huenda tukaelewana na kusaidiana
 
Kama kweli una mtoto na unakaa kwa ndugu yako,nadhani hayo maneno anayokupa ni tiketi ya kutaka wewe uhame hapo.Maisha ni kujaribu ndugu.Nilikuwa katika same situation kama wewe kibaya zaidi mimi aliyekuwa ananifanyia hivyo ni baba yangu mzazi.Nilipokuwa nahama kwenda kwa ndugu,alikuwa anakuja kunichukua maana walikuwa wanamuogopa.
Siku niliamua,na sasa here I'm.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Akufukuzae hakuambii 'tokaaaaa'... popote utaishi mungu ndiye atakujadhi.
huyo kakutupa ila mungu kakuhifadhi. we sepa 2
 
Jipange,uondoke hapo,maisha ni kitendawili.anayekuona taahira kesho atakuja kukuomba msaada.Piga moyo konde katafute maisha kwingine.
 
habar zenu wanajamvi. mimi nimekua na tatizo la kutaka kujiua mara kwa mara. Ninapoishi nakaa kwa ndugu yangu, huyu ndugu yangu amekua na tabia ya kuninyanyasa na saa ingine kunidhalilisha mbele za watu, pia siku hizi amekua anapenda sana kuniuliza kama mimi ni taira au mzima hii hali imenichosha sana sitamani kuendelea kuishi hapa duniani ndo hii hali ya kutaka kujiua inapojia kitu baya ni kwamba nina mtoto haya mawazo yakinijia huwa natamani kujiua mimi pamoja na mtoto sababu naogopa nikimuacha atapata shida sana. NAOMBENI MNISAIDIE HATA KWA MAWAZO NIWEZE KUKABILIANA NA HII HALI MAANA IMEKUA IKINIANDAMA MARA KWA MARA.
Karma, kwanza pole!.
pili wewe pia una matatizo!, hauko sawa!, ile tuu kufimkiria kujiua its insanity!, sababu pekee iliyokufanya hujajiua ni huyo mwanao tuu!. Nawashauri ndugu zako watakaosoma humu, kwanza wakusaidie kuondokana na tatizo lililokufanya wewe kulazimika kuishi hapo kwenye manyanyaso na masimango!, pili wakusaidie kutatua tatizo lako la kisaikolojia linalokusibu, ndipo uruhusiwe kuhama na mwanao, maana matatizo kote yapo, ukihama kwenye matatizo, ukakutana na matatizo mengine, bili kutibu chanzo cha insanity yako, una risk ya kuja kutuulia mwanetu na ndipo ujimalize!.

Ni PM, nikueleze tatizo lako, u deal nalo kwanza ndipo ufikirie kuhama!.
Pasco.
 
Pole sana, najua unavyojisikia mimi pia nilipitia maisha ya kulelewa kwa ndugu niliyopitia Mungu pekee ndio anajua, na hivi leo nina kwangu na maisha yangu mazuri tu lakini huwezi amini ule uchungu umegoma kuondoka kila nikikumbuka bado napata maumivu moyoni nimeshaomba Mungu sana aniondolee hiyo hali ya uchungu lakini sijui atajibu lini, cha msingi ndugu yangu ondoka hapo, hata kama hali yako ni ya kuweza kupanga chumba kimoja na kula mla mmoja anza hivyo hivyo, kuliko hali hiyo usipohama hapo iko siku lengo lako litatimia, nilichojifunza katika maisha haya ukitaka kuishi vzr na ndugu kaa mbali uwe na kwako na vyako lakin ukiwa dependent kwao UMEKWISHA
 
pole sana
kwa aliepitia hali hiyo anajua unavojiskia
cha msingi tafuta sehemu nyingine ukakae
ni heri kunyanyasika kwa mtu baki kuliko kwa ndugu...

tafuta sehemu nyingine ukae,na jishughulishe,ukiwa busy inasaidia kuputoa hayo mawazo

Mungu akusaidie sana
 
dada achakuwa na mawazo finyu, nikweli kunyanyaswa kunaumiza sana lakini isiwe sababu ya wewe kufa, embu amka kwanini umnganganie huyo ndugu yako kiasi hicho achananae katafute maisha yako uoga wako ndio umaskini wako amka toka katika wafu bibie
 
Ukweli inaumiza sana. Tukushukuru kwa kuonyesha moyo wa kumsaidia mkuu na tunaomba feedback. be blessed
Nimeumia sana. usikate tamaa hayo ndiyo maisha. kumbuka kujiua ni dhambi isiyo sameheka ni PM tuongee vizuri ninakamradi ka ufugaji kuku hakana usimamizi mzuri huenda tukaelewana na kusaidiana
 
Dada achana na huyo ndungu yako, tafuta hata kwa mtu ukae ukafanye kazi za ndani kama hujasoma. Kuna watu wana roho nzuri sana ambao wanaishi na wafanyakazi vizuri na watoto wao. Ninakuomba sana sana Mungu amekupangia maisha mazuri na mwanao, achana na ndugu wengi ni wabaya sana na manyanyaso. Wengi wetu tumepitia huko na tukakomaa na leo hi tuko na keyboard na tunaajiri. Sasa kimbia kabisa, pata tu pa kuanzia upate hela kidogo ujitegemee na vibiashara vidogovidogo. Ukijiua na mwanao ni jehanamu tu na mateso ya milele. Maisha ni matamu sana, tena ukiyaanza kwa tabu unamaliza kwa furaha eti!!! Wale ndugu zangu leo hii wakipata shida mimi wa kwanza simu!!! Ha ha ha!!! Halafu nawakomesha, wakiwa na vikao vyao uchwara vya harusi vya kimaskini nawashushia mchango wa haja!!!! Wakikwama bajeti imebana mara wanataka wanandugu waongezee deficit nawaambia acha natoa!!! Mimacho inawatoka wazee wakisikia kuwa nanihii ndiyo kaokoa jahazi!!!! Kuna mmoja akiniona utasiki ampe Fulani kitu akae, pole mwanangu!!! wakati alipokuwa na hela mama mjane anatusomesha kwa tabu alimwambia "ungekuwa unaweka fedha kidogokidogo ili usomeshe watoto, sisi hatuna hela, kama huna hela za kusomesha acha watoto wawe majambazi mtaani na wewe rudi kwenu". Leo hii sisi wote ni wafalme na malkia na mama yetu ni mkuu wa malkia!!! Hakujiua kwa sababu ya manyanyaso ya ujane!!! sasa wewe binti mzuri ni kwa nini unatak ufe!!! we love youuuuuuu mwaaaaaa!!!
 
Pole dear, kwani maisha ni hapo kwake tu, maisha popote, jitahidi uondoke utaona jinsi maisha yalivyo matamu
 
pole ndugu jitahd utafute ki2 cha kukuingizia kipato huyo anakufanyia hvyo kwasababu anaona hauna msaada kwake pia anashndwa kukuambia uondoke kwake.

kujiua sio solution ndugu ukizngatia ni dhambi kubwa ndugu utamuacha mtoto pasi mahitaji jaman mmmh ucfikie huko mungu akusaidie uondokane na mawazo mabaya kiasi hiko.
 
Haya maisha wengi tu tumepitia,basi hatusemi ila mimi nina roho ya hivi''bora kufa nimesimama kuliko nimepiga magoti''mimi nilianza kujitegemea na 18yrs old ndani ya jiji hili la dar niliona siwezi dharaulika hata hausgel aloikuwa anaheshimika aisee niliaga nikaondoka! Leo hii mimi nikifika pale ni mfalme na wananipigia simu mbona umetususa!
Kutoka hapo nimejifunza kukaa mbali na ndugu.sio mwisho wa maisha dada yangu fanya mambo yote usimwache mtoto kimbia nae popote uendako walimwengu sio watu kabisa watamchoma moto
 
Back
Top Bottom