Roho yangu inaanza kukaa mbali na huyu ndugu yangu, je nina makosa mimi kutopokea simu zake?

Nyie acheni kumdanganya mwenzenu, toka lini binadamu akafurahi aonapo mwenzie amefanikiwa ukiachana na wazazi wako???? Aunt anakuloga huyo
 
Mmmmh akili yangu haitaki kumuhukumu hivyo, sababu ni mtu mwema kwangu, na sina ushahidi Wowote dhidi yake, anyways Mungu anajua vyote Keenly
Wengi walioonekana ni wema kwetu, walituliza, anyway Mwamini Mungu tu mkuu
 
Ndugu huyo jamaa yako ana akili za kimasikini.
Mtu anakuuliza unafanya kazi gani? Kazi yangu itakusaidia nini?
 
kwanza unatakiwa kujiridhisha ,Uliizaji wake ni waheri au washari?
wapo ambao hukuuliza kwa nia njema ili kujua maendeleo yako na changamoto zako ,ili akusaidie kimawazo na wakati mwingine hata kukuombea barka ,Au kama una mazuri basi kufurahia neema zako ,
Wakati mwingine mtu anaweza kukuliza ukahisi ana nia njema ,kumbe kinyume chake ,anataka kujua mipango yako aivuruge ,Au kama alishaivuruga anataka kujua je amefanikiwa kiasi gani ? Dunia yasasa sio ya kumwamini mtu ,inawezekana akawa ana nia njema au uovu ,haya yote yawezekana .
 
Wasiwasi wako wa kumwambia ukweli ndo uhalisia halisi!

Kiufupi huyo shangazi yako sio mtu mzuri, hayo maswali mostly yanaulizwaga na wachawi

Be careful[emoji848]
 
Hayo maswali na udadisi ningemjibu kama ananipa ushirikiano wowote kuhakikisha nafanikisha majibu ya maswali yake, vinginevyo nampotezea tu kama unavyofanya.

Kibongo bongo hatupendani, si ajabu anakuchimba chimba kwaajili ya udaku ambao hauna maana yyt kwake na kwako.

Wakati mwingine ushirikina. Rejea maelezo yake kwako kwamba baadhi ya ndugu humkaushia simu zake pia
 
Mkuu umesema kitu cha ukweli
 
ni kweli kaka lakini kwanini tuwe na hofu na kila mja, hivi ni kweli
kila hatima zetu zipo mikononi mwa watu wabaya
 
Shangazi anatamani kuona ukifanikiwa jaman...
 
Wewe Kama nafsi yako inataka kukaa mbali nae fanya ivyo...heri ya wali nyama kuliko walimwengu.
 
ni kweli kaka lakini kwanini tuwe na hofu na kila mja, hivi ni kweli
kila hatima zetu zipo mikononi mwa watu wabaya
Una point ya msingi kiukweli, ila elewa tu katika maisha ya kawaida na maisha ya utafutaji kuna namna unatakiwa kuishi na watu unakutana nao na wale unaowaamini kwa kuwaita ndugu.

Usiwe na Hofu na mtu yeyote ila jifunze kuwa MAKINI na kila mmoja unayekutana naye au kuishi naye.

Zaidi ya yote ishi maisha ya kujiwekea mipaka na ukiasi katika kufanya na kuongea pia mambo yanayogusa maisha yako moja kwa moja.

Adui wa kweli ni mjanja sana kuliko unavyofikiri na wakati mwingine anaweza kuwa yule unayemwamini sana kupita kiasi.

Point ya msingi : Adui wa kweli ni mjanja sana.
 
mm nimekuwa mtu muwazi sana kwenye maisha yangu sijafanikiwa bado ila pia bado sijaona changamoto za hawa wapumbavu katika maisha yangu, Nina dada yangu naye msimamo wake ni huo kiasi kwamba mpaka kujua anafanya nini kwa sasa ni vigumu mno.
 
mm nimekuwa mtu muwazi sana kwenye maisha yangu sijafanikiwa bado ila pia bado sijaona changamoto za hawa wapumbavu katika maisha yangu, Nina dada yangu naye msimamo wake ni huo kiasi kwamba mpaka kujua anafanya nini kwa sasa ni vigumu mno.
Kuna mambo mengine maisha yanakufundisha muda unapofika.

Jambo la muhimu ni kutomwamini kila mtu unayekutana naye.

Kuwa makini haina maana uwachukie, HAPANA.

Ishi nao kwa upendo na amani ila "Usiamini kuwa hawawezi kukufanyia lolote baya"

Binadamu wote tumeumbiwa roho ya ubinafsi hivyo kubadilika ni jambo la kawaida.
 
Shangazi yako anakujali. Anapenda kujua maendeleo yako...... Sasa mbona una mchukia tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…