-Ni ulimwengu wa mbadilishano/Trade oeiented.
Maisha ya mwanadamu katika kila kitu kina mbadilishano.Naamanisha utatenda hili upate lile.Hakuna kinachokuja bure.Na kila upande mwema au mbaya huvutia kwake kwa sera nzuri lakini zenye masharti ya mficho ndani yake.Tumeumbiwa free will katika kufanya maamuzi,amua leo unataka mema au mabaya?Amua nani unayetaka kumtumikia?Mungu ama shetani maana wote ni roho.Maamuzi yako ndiyo yatakayoainisha ni nini kikupate baadaye.Na usije ukajidanganya huko utakapochagua kuenenda ndipo utapata malipo yake.Umeamua kupata vitu kwa uhalali pasipo dhuluma wala manung'uniko hakika utapata mema yadumuyo.Lakini unatafuta kwa dhuluma,ushirikina,kutumia mwili wako isivyo halali au kwa ushawishi wa pesa ama zawadi ndiyo yapo mafanikio ya muda mfupi yenye kilio kwako au kwa wengine.Unatoa nini upate nini?Kama ulivyosema kaka unaburudisha mwili leo lkn unazoa roho au mapepo yanaweza kukudhuru mwenyewe afya ya mwili na akili pia na uchumi.
Je unatumia nyezo gani katika mbadilishano?
(Moyo wako,pesa,kuiba nyota za watu,uchawi,kumwaga dammu za watu nk).
Jiulize mwisho wa hayo yote unayoyafanya yanakupa amani ya moyo na ungependa utendewe hivyo kupata mafanikio au kutatua shida zako?
Ninachoamini dhambi husameheka lakini madhara yake je?Vipi kwa wengine wasiojua baba au mama alitoa nini apate nini?