PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mnamo tarehe 29 Juni 2025, Roi Paul Chitanda, anayetambulika pia kama Mgalatia wa Kipindimbi, alichukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Udiwani wa Kata ya Boma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Chitanda aliwahi kuwania nafasi hiyo na kushindwa kwa tofauti ya kura moja pekee, jambo lililoacha historia isiyosahaulika katika kata hiyo. Safari hii, amerudi tena akiwa na ari mpya na dhamira ya kuendeleza maendeleo katika kata yake.
Kwa sasa, Roi Chitanda ni Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM Kata ya Boma, nafasi anayoitumikia kwa bidii, huku akijipambanua kama kijana mwenye dira ya maendeleo na mshauri wa wenzake katika masuala ya kisiasa.
Hatua yake ya kuchukua fomu inaonyesha nia yake ya dhati ya kuendelea kulitumikia taifa kupitia udiwani, na kuendeleza juhudi za kuwaletea wananchi wa Boma maendeleo.
Hatua yake ya kuchukua fomu inaonyesha nia yake ya dhati ya kuendelea kulitumikia taifa kupitia udiwani, na kuendeleza juhudi za kuwaletea wananchi wa Boma maendeleo.