Tuweke mambo ya rangi na asili ya mtu kwenye perspective.Hivi kati ya mtu aliyezaliwa Madras huko India na kuja Bongo ukubwani huku akiwa na passport wa India,Bongo na Canada,na yule aliyezaliwa Kongwa,na kusoma Pugu,kisha kuja Mlimani kabla ya kuukwaa ukubwa serikalini,nani anayepaswa kuwa na machungu zaidi na "nchi yake" (assuming kuwa huyo Mdosi nae ni mwananchi)?Jawabu la wazi ni,HUYO MBANTU MWENZETU.
Siku zote nimekuwa na-question allegiance ya hawa magabachori kwa taifa letu.Lakini kabla ya kuwalaumu moja kwa moja huwa najiuliza,hivi kama mie ningekuwa nawaona hawa waingereza wanaitafuna nchi yao bila huruma,nini kingenizuia mie kufuata mkumbo iwapo kwa kufanya hivyo nisingejikuta naishia jela?Kwa maana hiyo,wadosi wanaweza kufanya wafanyayo kwa vile "wenye nchi halisi" wanaendekeza maslahi binafsi kuliko nchi yao.
Hata hivyo,kwa vile two wrongs do not make a right,wizi na ujambazi wa wahindi hauwezi kuhalalishwa na tamaa,wizi,ujambazi,ubadhirifu na ubabaishaji unaofanywa na "watanzania wasio na asili ya India" (wazawa!!!??).