Kifurukutu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 4,641
- 6,694
Happy new year 2020 wanaJF
Kwa kitendo hiki kama ni kweli kulingana na nilivyosikia, basi nchi yetu imefikia pabaya
Msanii wa Hip hop Roma Mkatoliki baada ya kutoa ule wimbo wake "Naitwa roma" unaohusu maswala ya siasa za hapa nchini hususani zinamrengo wa kuipinga serikali, msanii huyo sasa amekimbia nchi kwa kuhofia usalama wake kufuatia kutoa kibao hicho
Roma Mkatoliki kwa sasa amekimbilia nchini Marekani akihofia kukamatwa, kutekwa, na kuuliwa na serikali hii ya Rais Magufuli
itakumbukwa miaka ya nyuma msanii huyo alitekwa na kuumizwa vibaya, mpaka sasa waliofanya tukio hilo ni watu wasiojulikana
Nahoji kama Mtanzania wa kawaida, haki ya mtanzania kuishi katika nchi yake hapa inatazamwa vipi?
Uhuru wa kujieleza na kukosoa hapa nchini ni wa kitabaka tu? Yaani CCM ndio wanahaki ya kuukosoa upinzani pekee?