Tetesi: Roma Mkatoliki akimbia nchi, sasa anaishi uhamishoni

Tetesi: Roma Mkatoliki akimbia nchi, sasa anaishi uhamishoni

Huko Marekani wenyewe wanajiandaa kumshtaki raisi wao,kiongfozi huyo huyo wa Marekani alitaka kuweka ukuta kujitenganisha na nchi fulani.
Marekani hiyo hiyo watu weusi wanakula chuma hadi wakiendesha gari vibaya,lakini siyo vibaya ukiruka mavi ukakanyaga dimba.
Vipi kiongozi wetu ndo angekuwa anakosolewa na watu Kama wamarekani wafanyavyo?.
Unahisi Nini kingetokea?
 
unafikiri alitekwa kwa sababu zipi kile kipindi
Mpaka leo Roma hajathibitisha nani alimteka, duniani kila siku watu wanatekwa, wengine wanajiteka kwasabubu mbali mbali lakini haisababishi wao kukimbilia kukimbilia nje na kuomba hifadhi. Swala la hifadhi ni pana kuliko mnavyolifikiria. Mpaka athibitishe kama misha yake yako hatarini Kwa sababu za KISIASA, KIJINSIA au KIIMANI ndio atasikilizwa. Maswala mengine yote yanatakiwa yashugukikiwe na dola ya nchi husika anayotoka.
 
hujui kitu kuhusu marekani ni vema ukafunga domo
Huko Marekani wenyewe wanajiandaa kumshtaki raisi wao,kiongfozi huyo huyo wa Marekani alitaka kuweka ukuta kujitenganisha na nchi fulani.
Marekani hiyo hiyo watu weusi wanakula chuma hadi wakiendesha gari vibaya,lakini siyo vibaya ukiruka mavi ukakanyaga dimba.
 
Hakuna anayemtafuta au hata kumtisha maisha yake hapa Tanzania, amekaa hapa muda wote hata baada ya hoja ya kutekwa bila kuguswa na yoyote. Uhamiaji wa marekani wana mtandao mpana kujuwa nani yuko hatarini, nani ni mbabaishaji. Muda utaongea.
Watu sasahivi wamebuni njia za kupiga hela huko ughaibuni. Alianza Ansbert Ngurumo, akafuatia TL na sasa Roma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata huko marekani wao kwa wao wanapotezana sana wakiona ww ni mdudu kwao, kama sio kupotezwa utapigwa hata sumu bila ww kujua, marekani nako hamna uhuru huo ambao wengi wetu huwa tunauwazia humu.

Roma arudi tu , hana cha kuhofia, kufa kupo tu, anaeua nae atakufa.
 
Na waliyonifanyiaga central haki ya mungu siwezi sema,
Maana wale wasenge walidiriki mpaka kunigeuza nyuma,
Wakanimwagia Mbegu siwezi meza siwezi tema,
Ndo maana sikushangaa ile ghafla toka CCM kwenda chadema,
Wanasema kitanda ukitandika sharti ukilalie,
Nikajitia ukamanda yatakwisha wacha nivumilie,
Kila kiza kikitanda ndo machozi wacha mi nilie,
Penzi akatia parapanda kuwaalika waje washambulie....
Ooh mbona sikomiii
Sikomi.....
Licha ya mateso haya
Haahahaahaa!!! Nilifikiri unaimba ipap kumbe unabana pua,usamehewe amina.
 
Happy new year 2020 wanaJF

Kwa kitendo hiki kama ni kweli kulingana na nilivyosikia, basi nchi yetu imefikia pabaya

Msanii wa Hip hop Roma mkatoriki baada ya kutoa ule wimbo wake "naitwa roma" unaohusu maswala ya siasa za hapa nchini hususani zinamrengo wa kuipinga serikali, msanii huyo sasa amekimbia nchi kwa kuhofia usalama wake kufuatia kutoa kibao hicho

Roma mkatoriki kwa sasa amekimbilia nchini Marekani akihofia kukamatwa, kutekwa, na kuuliwa na serikali hii ya Magufuli

itakumbukwa miaka ya nyuma msanii huyo alitekwa na kuumizwa vibaya, mpaka sasa waliofanya tukio hilo ni watu wasiojulikana

Nahoji kama mtanzania wa kawaida, haki ya mtanzania kuishi katika nchi yake hapa inatazamwa vipi?

Uhuru wa kujieleza na kukosoa hapa nchini ni wa kitabaka tu? yaani ccm ndio wanahaki ya kuukosoa upinzani peekee?

Mkuu

Kuna jitu moja la ajabu sana,lenye kipara na lenye Kiswahili na Kiingereza kibovu sana lipo pale njia ya kwenda Kigamboni

Hovyo sana

Litakuja kupata aibu sana na historia
 
Unajua polisi kuna kitengo cha Fraud? Unafikiri kwanini yule mwanachuo wa UDSM aliposema ametekwa walimkamata na kumpandisha kizimbani? Kesho nenda sehemu kajifiche ndugu au mtu yoyote asijue halafu wapigie simu ndugu na marafiki uambie umetekwa kisha waambie wakaripoti polisi. Baada ya wiki 3 jitokeze uone shughuli yake. Ndiyo utajua kama ni mradi wa kujiteka uko vipi. Jaribu kupitia vifungu vya sheria vitakusaidia kuliko kusoma umbea jamii forum na mitandao mingine ya kijamii.
Kifupi tu. Udanganyifu wa aina yoyote ni kosa la kisheria kwahiyo hapo wakigundua umejiteka lazima ukanyee ndoo kwanza ili iwe fundisho kwa wengine. Huo mfano kajaribu halafu uje utoe mrejesho hapa.
Ni mradi alioubuni kwa muda mrefu, kujiteka, kutoa nyimbo ya kuchafuwa watu fulani ili iwe kisingizio kama hapa Tanzania hayuko salama. Lakini Wamarekani sio wajinga, Bobi Wine alishidwa kubadili ukaaji wake nje, sidhani kama Roma ana kigezo chochote cha kubeba kesi yake.
 
Hahahaha, hizi ndio akili za Watanzania
 
Wacha aende kama kaona kuna dalili ya kufa kwa "ugonjwa wa moyo".
 
Nchi hii wanaotakiwa kuimba ni wanaosifu na kuabudu watawala pekee, wanaokosoa hawatakiwi hapa nchini, nchi yetu sasa hivi inaongozwa na mkuu wa malaika hajawahi kukosea, yeye kila anachofanya ni kizuri tu.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna anayemtafuta au hata kumtisha maisha yake hapa Tanzania, amekaa hapa muda wote hata baada ya hoja ya kutekwa bila kuguswa na yoyote. Uhamiaji wa marekani wana mtandao mpana kujuwa nani yuko hatarini, nani ni mbabaishaji. Muda utaongea.
Sio Roma pekee ambaye yuko hatarii, kila mtanzania hivi sasa anaishi kwa hofu!
 
Back
Top Bottom