Tetesi: Roma Mkatoliki akimbia nchi, sasa anaishi uhamishoni

Vipi kiongozi wetu ndo angekuwa anakosolewa na watu Kama wamarekani wafanyavyo?.
Unahisi Nini kingetokea?
 
unafikiri alitekwa kwa sababu zipi kile kipindi
Mpaka leo Roma hajathibitisha nani alimteka, duniani kila siku watu wanatekwa, wengine wanajiteka kwasabubu mbali mbali lakini haisababishi wao kukimbilia kukimbilia nje na kuomba hifadhi. Swala la hifadhi ni pana kuliko mnavyolifikiria. Mpaka athibitishe kama misha yake yako hatarini Kwa sababu za KISIASA, KIJINSIA au KIIMANI ndio atasikilizwa. Maswala mengine yote yanatakiwa yashugukikiwe na dola ya nchi husika anayotoka.
 
hujui kitu kuhusu marekani ni vema ukafunga domo
 
Hakuna anayemtafuta au hata kumtisha maisha yake hapa Tanzania, amekaa hapa muda wote hata baada ya hoja ya kutekwa bila kuguswa na yoyote. Uhamiaji wa marekani wana mtandao mpana kujuwa nani yuko hatarini, nani ni mbabaishaji. Muda utaongea.
Watu sasahivi wamebuni njia za kupiga hela huko ughaibuni. Alianza Ansbert Ngurumo, akafuatia TL na sasa Roma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata huko marekani wao kwa wao wanapotezana sana wakiona ww ni mdudu kwao, kama sio kupotezwa utapigwa hata sumu bila ww kujua, marekani nako hamna uhuru huo ambao wengi wetu huwa tunauwazia humu.

Roma arudi tu , hana cha kuhofia, kufa kupo tu, anaeua nae atakufa.
 
Haahahaahaa!!! Nilifikiri unaimba ipap kumbe unabana pua,usamehewe amina.
 

Mkuu

Kuna jitu moja la ajabu sana,lenye kipara na lenye Kiswahili na Kiingereza kibovu sana lipo pale njia ya kwenda Kigamboni

Hovyo sana

Litakuja kupata aibu sana na historia
 
Unajua polisi kuna kitengo cha Fraud? Unafikiri kwanini yule mwanachuo wa UDSM aliposema ametekwa walimkamata na kumpandisha kizimbani? Kesho nenda sehemu kajifiche ndugu au mtu yoyote asijue halafu wapigie simu ndugu na marafiki uambie umetekwa kisha waambie wakaripoti polisi. Baada ya wiki 3 jitokeze uone shughuli yake. Ndiyo utajua kama ni mradi wa kujiteka uko vipi. Jaribu kupitia vifungu vya sheria vitakusaidia kuliko kusoma umbea jamii forum na mitandao mingine ya kijamii.
Kifupi tu. Udanganyifu wa aina yoyote ni kosa la kisheria kwahiyo hapo wakigundua umejiteka lazima ukanyee ndoo kwanza ili iwe fundisho kwa wengine. Huo mfano kajaribu halafu uje utoe mrejesho hapa.
 
Hahahaha, hizi ndio akili za Watanzania
 
Wacha aende kama kaona kuna dalili ya kufa kwa "ugonjwa wa moyo".
 
Nchi hii wanaotakiwa kuimba ni wanaosifu na kuabudu watawala pekee, wanaokosoa hawatakiwi hapa nchini, nchi yetu sasa hivi inaongozwa na mkuu wa malaika hajawahi kukosea, yeye kila anachofanya ni kizuri tu.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna anayemtafuta au hata kumtisha maisha yake hapa Tanzania, amekaa hapa muda wote hata baada ya hoja ya kutekwa bila kuguswa na yoyote. Uhamiaji wa marekani wana mtandao mpana kujuwa nani yuko hatarini, nani ni mbabaishaji. Muda utaongea.
Sio Roma pekee ambaye yuko hatarii, kila mtanzania hivi sasa anaishi kwa hofu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…