Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

[QUOhagahahaaaTE="longi mapexa, post: 33484265, member: 306162"]
maajabu msomi wa shahada nne hajui kazi za fasihi katika jamii
[/QUOTE]
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?" Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Kuna mahali hata akina Isaac Newton walikosolewa.
elimu si kigezo cha kutokosolewa, ingekuwa ni hivyo basi wasomi wasingefungwa na washitaki wao wasiosoma, mwambieni ni ujinga kuwa na mawazo ya namna hiyo
 
Roma arudi shule jamani

Mtu anaefundisha au aliwahi kufundisha chuo sio wa kumfananisha na alieishia darasa la saba jamani huo ni ukweli usiopingika

Mwakyembe alipasua GPA kubwa Bachelor akabakizwa kuwa mwanataaluma UDSM huwezi fananisha na Msanii yeyote hapa nchini
wewe fala kweli kufauli Gpa kubwa kabaki chuo ndio akili kubwa huyo alikuwa anakalili njoo mtaani ndio utajua wanafanya mambo mkubwa walikimbia kukaa huko utumwani
 
Sasa nimeelwa kumbe hawa watu walio onja sumu na kupona inaelekea ni wabishi sana ! Inaonekana hata mungu amewablock wasiingie kwenye mahakama za mbinguni maana mungu hata akitaka kuya hukumu yaende Motoni yanabisha matokeo yake yatataka kuishi mahabusu ya mbinguni kula vya Bure mpaka Siku ya mwisho Wa dunia kwenye hukumu ya pamoja ndiyo yapatikane na kosa
 
Yaani nyimbo hata wiki haina.
Mapovu yametoka YAKUTOSHA na chenji imerudi [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2].
Hizo digrii zake ni kama za profwesa LIPUMBA.
 
Wape. Waambie ukweli. Kushabikia ujinga hakujawahi kumtoa mtu. Wasanii wote waliotajirika dunian sio wale waliochanganya siasa na sanaa. Wasanii wote dunian kote waliojaribu kuchanganya siasa na sanaa waliishia kubaya sana.

Sanaa haijawahi kuchanganywa na siasa na ikabaki kuwa sanaa.

Mnavochangia jaribun kuwa real kwenye reality. Sio kushabikia vitu ambavyo havijawahi kuwa positive hapa dunian.
Kwani Roma kakwambia anataka kuwa msanii mkubwa duniani??
 
Asingesema nisingejua kuwa ana Degree nne.. [emoji16][emoji16][emoji16]

Sasa ajitahidi kuzitumia Degree zake nne tuzione kwa vitendo na siyo mdomoni..

Kama kweli anazo lakini! [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mh.Waziri,kuna mahali ktk katiba yetu panaposema angalau kujuwa na kusoma tu bila ya kujali ukomo wa darasa nakadhalika,unaweza chaguliwa kuwa mbunge,na ukiwa mbunge unaweza chaguliwa kuwa Spika.
Mh.Waziri huenda hujamuelewa Roma au wananchi hawajakuelewa weye kuhusu maandiko yako uliyo yakana ambayo yalikunyanyuwa
Mh Waziri....hakuna atakae ishi milele,tupendane tumuogope Mungu,tumuombe msamaha.
 
King msukuma nae ni std seven tu.
Kaisadia nini Dunia wewe... Kusoma kasoma yeye ili apate kula na kuishi yeye na familia yake.. Bakhersa hajasoma kumbuka lakini anamuona mwenye Degree ni Fala tu...

Inamaana Mwakyembe siku akikutana na Yesu atamuambia wewe Yesu hujasoma utanishauri nini? IQ aliyotumia Waziri ni Ujinga... aache kujimwambafai...
 
Huyo Roma naona amechoka kulala na mkewake..ni mpenda sifa za kijinga

..inaelekea hujausikiliza wimbo wote na kwa umakini.

..Roma amemsifia mtukufu kwa ukusanyaji mapato, ujenzi wa fly over, na amesema mtukufu aombewe.
 
Roma amedanganywa na wanasiasa wabaya tu
Ninakuelewa, pamoja na kwamba sikubaliani na wewe.
Unachomaanisha, ambacho Waziri Harrison George Mwakyembe hawezi kukipinga ni kwamba, Roma Mkatoliki akikengeuka akaimba siasa kwa mtindo wa Harmonize (na sasa Nandy), atasifiwa sana na wale wenye digrii 4 au zaidi.
Roma Mkatoliki hataambiwa kuwa muziki wa siasa haulipi. Badala yake atatunzwa sana na Wanasiasa wenye digrii nyingi na kushawishiwa kugombea ubunge.
 
Back
Top Bottom