ROMA MKATOLIKI CV!!!! Sio tu Msanii??

luvcyna

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2009
Posts
1,848
Reaction score
1,940
Huyu kijana huwa ananigusa mno na mashairi yake...hii imepelekea kubaki na maswali mengi kichwani kila ninaposikia nyimbo zake, je inawezekana....??
Ila hapana, kuna kila dalili akawa na zaidi ya usanii unless mashairi yake yawe yanatungwa na mwingine naye awe mwimbaji tu...tofauti na hivyo basi tuseme ana elimu ya ziada ukitofautisha na hawa wasanii tulionao kwenye hiki kizazi kipya.

Mengi ya yaliyomo kwenye mashairi ya huyu kijana yanakosoa walio viongozi kwa ujasiri wa ajabu na nyimbo zikizidi kuuzika kwa kasi ya ajabu....

Kwa uzuri tu tufahamishane kuhusu walau Cv yake....Anastahili pongezi kwani anaonekana hanunuliki na wanasiasa kwa ajili ya kuwasifia kwa nyimbo pindi wawapo majukwaani kama ambavyo wengi tumewaona na waliojikuta wakipoteza wengi wa mashabiki kutokana na wao pasipo uelewa wamekuwa wakiwagawa wapenzi wa nyimbo zao kwa itikadi za vyama vya siasa wanavyovitumikia..
 
dogo namkubali sana.hatofautiani sana na fid q sema yeye mashairi yake yanatoka na biblia yaani amenukuu kwenye biblia.
 
anaitwa Ibrahim Mussa,anatokea Tanga...nasikia yupo pale Ud,CoICT...anapiga computer science,hapo sijui ni dip au jiwe,mwenye kufahamu atujuze!
 
daa huyu jaama namkbali sana hasa kwenye ile nyimbo ya mathematics..namfananisha ujio wake na akina mkoloni..
 
mpiga kelele tu uyo,usimfananishe na fid q
 
anajua sana! Ni zaidi ya msanii, ni mwanaharakati!
 
Anyway kuna kingine kinachonipa walakini hapa,..kuna tokea malalamiko siku za usoni kuhusu hawa clouds kuwatenda ndivyo sivyo wasanii wengi kwa kuwatumia katika matamasha yanayowaingizia millions of shs..kisha kuwatosa pasipo malipo sahihi yanayolingana na kazi yao...

1.Mara kadhaa sijaona clouds wakimsogelea,ni je wanamuogopa kutokana na msimamo wake?
2.Mara nyingi tunawasikia watangazaji wa clouds waliowasimulizi wa muziki wa hiphop wakiziongelea nyimbo zinazohit za hiphop,.mbona hawaisimulii hiphop iliyotukuka kutoka kwa huyu kijana?
 
anaitwa Ibrahim Mussa,anatokea Tanga...nasikia yupo pale Ud,CoICT...anapiga computer science,hapo sijui ni dip au jiwe,mwenye kufahamu atujuze!
Nashukuru kwa taarifa mkuu,..i think he dserve tht
ila kuna kamstari kake katka kibao kinachoitwa mathematiks kanasema mwambieni sirudishi kadi ya chama kama nakaya, hii haileti picha flani kuonyesha yupo upande flani au ni just msimamo?? halafu pia hapo aliposema mwambieni anamaanisha nani vile?
 
Angekuwa anaimba reggae ningemuita B.Marley wa Tz. He is a strong activist.
 

Me Ni Mfuatiliaji mzuri wa swahili Hip Hop. Na kwa kumbukumbu zangu hawa clouds kuna kipindi wali-vow kuiangusha swahili hip hop, kipindi kile cha wagosi wa kaya, mapacha na wengine wengi. Cha kushangaza sasa hivi hip hop imerudi tena na kwa nguvu tena kutokana na uwepo wa medias nyingine nyingi, na clouds wanakumbatia wanahip hop wachache sana. Ukiimba concious Hip hop hawakutaki.
Now Back to Roma, huyu jamaa hawamzoei wanamuogopa kwa sababu watanzania wengi wamemkubali na haogopi kusema lolote. Kwa mfano kwenye moja ya nyimbo zake iitwayo "Mathematics" kule ndani kampaka Ephraim Kibonde. Mstari unasema ".... Kibonde wewe ni member wa Loan Board au TCU???" Hii ni kutokana na Kibonde kuzngumzia mkopo kuwa wanafunzi wanautapanya.
 
Asante kwa burudani bwana Lokisa, naomba msinichoke na mswali, mbona jamaa hapa anaonekana kavaa gwanda? imekaaje hii?



Gwanda huyu jamaa ndio kama sare yake ya kazi.
Magwanda hata kabla hayajakuwa official Chadema wear yalikuwa ni mavazi ya wanaharakati wengi na wakombozi walopita. Baadhi Ya wankombozi waliotumia Au Kuvaa magwanda ni kama
1. Ernesto Che Guevara
2. Fidel Castro
3. J.K Nyerere (picha nyingi zipo)
4. Wapiganiaji uhuru wengi wa South Africa

Na wengine wengine wengi, so hii ni kama uniform ya wanaharakati nahisi ndio sababu ya huyu Kijana pia kuzitumia.

Pia Khaki Inaonekana kuwa ni kama vazi la Concious Artists wengi kama kina "Ice Cube", "Common", na wengine wengi.
Roma Mkatoliki Ni One The Most Realest MCs Kuonekana Tanzania Hii
 



Me naona jamaa yuko neutral, huo mstari kautumia tu kuonesha msimamo. Na kama anashabikia chama chochote ambayo ni haki yake kikatiba nahisi haoneshi kwenyew mziki wake. Nasema hivyo kwa sababu enzi za kampeni alikataa nyimbo zake zisitumiwe na Chadema wala chama chochote cha siasa
 
mpiga kelele tu uyo,usimfananishe na fid q

pole kama hujapata ujumbe toka kwake au kama sio wewe ni gamba maana magamba hawajifunzi mazuri na mema hata siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…