luvcyna
JF-Expert Member
- Feb 24, 2009
- 1,848
- 1,940
Huyu kijana huwa ananigusa mno na mashairi yake...hii imepelekea kubaki na maswali mengi kichwani kila ninaposikia nyimbo zake, je inawezekana....??
Ila hapana, kuna kila dalili akawa na zaidi ya usanii unless mashairi yake yawe yanatungwa na mwingine naye awe mwimbaji tu...tofauti na hivyo basi tuseme ana elimu ya ziada ukitofautisha na hawa wasanii tulionao kwenye hiki kizazi kipya.
Mengi ya yaliyomo kwenye mashairi ya huyu kijana yanakosoa walio viongozi kwa ujasiri wa ajabu na nyimbo zikizidi kuuzika kwa kasi ya ajabu....
Kwa uzuri tu tufahamishane kuhusu walau Cv yake....Anastahili pongezi kwani anaonekana hanunuliki na wanasiasa kwa ajili ya kuwasifia kwa nyimbo pindi wawapo majukwaani kama ambavyo wengi tumewaona na waliojikuta wakipoteza wengi wa mashabiki kutokana na wao pasipo uelewa wamekuwa wakiwagawa wapenzi wa nyimbo zao kwa itikadi za vyama vya siasa wanavyovitumikia..