Roma Mkatoliki: Mastaa acheni unafiki wa Instagram

Roma Mkatoliki: Mastaa acheni unafiki wa Instagram

Magnesium

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2014
Posts
317
Reaction score
185
Msanii anayefanya muziki wa Hip Hop kiharakati zaidi, Roma Mkatoliki kaamua kuwafungukia mastaa wenye tabia ya kuomboleza misiba kupitia account zao za Instagram pekee bila kushiriki msiba.

Roma amefunguka hayo kufuatia msiba wa mwanzilishi wa kundi la Tip Top Connection ambaye pia ni kaka yake Babu Tale, Abdul Bonge ambapo Roma amehoji baadhi ya maswali.. Yasome hapo chini:

Yupi bora kati ya;
1. ANAEFIKA NYUMBA/ENEO LA MSIBA HARAKA BILA KUPOST INSTAGRAM!! 2.ANAEWAPIGIA SIMU WAFIWA AMA KUWATUMIA UJUMBE WA POLE WAFIWA KWA NJIA YA TXT YA KAWAIDA AU WHATSSAP
BILA KUPOST INSTAGRAM!! 3.AMBAYE ANAPOST INSTAGRAM KUHUSU MSIBA NA KISHA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE BILA HATA KUSHIRIKI MSIBANI WALA KUWASOGELEA WAFIWA!! NB: #INSTAGRAM ISITUHARIBU

#AKILI #NGUVU #UWEZO#MAARIFA
#UTU #AMANI #UPENDO#HESHIMA
#THAMANI

#INSTAGRAM tumeijua juzi tu isitutawale kiasi kwamba iwe ndio inaendesha maisha yetu katika kila jambo!! Kuchunguza nani kapost na nani hajapost!!Mashabiki msiwakwaze wasanii na wasanii msiwakwaze mashabiki wenu!!
Kwani kabla instagram haijafika tuliishije!!?? #Pole kwa #familia ya #TIPTOP

cc Babutale @dj_kwame madeeali kassimmganga tundamantz
#WE_FEEL_YO '_PAIN_HOMIES
 
Last edited by a moderator:
Umeongea kweli kaka roma utandawazi unatupeleka pabaya mno
 
Hili ni dongo kwa jamaa anajiita Bikira wa kisukuma,maana jana alijifanya kuandika upuuzi wake insta akiwaponda mastaa amabao hawajapost insta kuhusu msiba,#well said Roma
 
ni ujinga kabisa ifike mahali tuheshimu mila na desturi zetu
 
Kaongea uzuri but sijui kama watamuelewa wenzie watanzania uzungu umetujaa mpaka tumewapita hao walioleta hiyo teknoloji.
 
Back
Top Bottom