Roman Abramovich: Utajiri wa Damu, Risasi na Umafia

Mkuu The bold,

Hongera sana kwa uandishi wa makala zako nzuri zenye kusisimua, kuburudisha, kuelimisha na kutafakarisha,

Ushauri wangu kwako Mimi kama mdogo wako ni kwamba, "Hakuna ulazima wa wewe kuweka wazi kuwa una access ya taarifa za kiusalama za hapa Afrika mashariki, wakati huo huo unafahamika kwa majina na mawasiliano yako, ni hatari sana lakini kwa sasa unaweza usilione hilo jambo"

Endelea kutupa vitu kimya kimya wakisema unatoa google hio ni nzuri zaidi sababu inamchanganya mtu kubaini vyanzo vyako vya maarifa.

Ahsante.
Hana access yoyote ya taarifa za kiusalama, ameweka huo mstari kuwatisheni...
 
Habibu B. Anga mm nilikua na ushauri tu japo inawezekana umeshashauriwa mara kwa mara, ni hivi, una kipaji Kikubwa sana cha uhandishi na namna ya kupangilia mtiririko wa story na hata kumfanya mtu anayesoma asiruke hata sentensi moja... Ushauri wangu, nadhani kama nia ya kuleta story humu ili ujulikane ishatimia kwa asilimia 100,hakuna asiyekujua humu au ku appreciate kipaji chako. Sasa nilikua nakushauri tumia hii fursa sasa kuanza kutoa vitabu na kuviuza kwa bei itakayokulipa faida, mmoja wa wateja wako wakuu takua mimi, tena kwa bei yoyote isiyozidi Milioni 1 kwa kitabu kimoja. Nimeona kiu ya kila mtu hata kule Insta watu wana kiu kubwa ya kusoma vitabu vyako...itakua jambo jema kama utalifanyia kazi hili.
Tushamshauri sana humu ila anapotezea.Nadhani hilo group la whatsapp linamlipa zaidi.
 
ROMAN ABRAMOVICH: UTAJIRI WA DAMU, RISASI NA UMAFIA

SEHEMU YA NANE

Hakuna kitu kizuri kama kiongozi ambaye anaweza kujitathimini na kukubali mapungufu yake na kukubali kukaa pembeni kupisha wengine. Mtu wa namna hii hata kama kuna madudu aliyafanya unajikuta unapata nafasi ya kumsamehe moyoni.

Licha ya mapungufu yake yote na vituko juu ya vimbwnga alivyovifanya kuidharaulisha Russia, lakini ulipofika wakati na kuelezwa ukweli kwamba ni muda muafaka akae pembeni kupisha mtu mwingine, Boris Yeltsin hakuifanya shingo yake kuwa ngumu.

Roman Abramovich akakutana na ma-oligarch wenzake. Akawapa pendekezo lake la nani anadhani anafaa kuwa rais mpya wa Russia. Akaweka sababu zake mezani… ma-oligarch wakakubaliana naye.

Nilieleza kwamba wale wanaojiita ‘The Family’ ambao ni ma-oligarch na wanafamilia ya Yeltsin kimsingi ndio ambao walikuwa wanaendsha nchi. Na ndani ya The Family kulikuwa na ule ‘Utatu Mtakatifu’… Abramovich, Tatyana na Yumachev. Na katika kipindi hiki Abramovich alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa Yeltsin kuwazidi wote hata ndani ya The Family na Utatu Mtakatifu.

Kwa hiyo ulipofika wakati wa kuzungumza suala hili zito na Yeltsin… ni Abramovich pekee yake… yeye na Yeltsin pekee walijifungia ofisini na ‘kuyajenga’.

Kwanza Abramovich alimueleza Yeltsin kwa nini huu ni muda muafaka yeye kukaa pembeni na kumpisha kiongozi mpya. Baada ya Yeltsin kuukubaliana na hili, Abramovich akamueleza kuhusu pendekezo la mrithi wake. Abramovich akamueleza kwamba anapendekeza Vladimir Vladimirovich Putin, Mkurugenzi Mkuu wa FSB aanze kuandaliwa kurithi kiti hicho cha Urais. Kama ambavyo aliwafafanulia ma-oligarch ndivyo pia ambavyo alimfafanulia Rais Boris Yeltsin.

Tarehe 9 August mwaka 1999 Rais Boris Yeltsin alimteua Vladimir Putin kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu. Yaani kipindi hicho ilikuwa kunakuwa na Waziri Mkuu alafu anakuwa na Manaibu watatu au wawili. Yaani mfano mzuri kama Zanzibar walivyo na ‘Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais’. Kwa hiyo Putin aliteuliwa kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu wa Russia. Nimeeleza kwamba kipindi hiki Russia ilikuwa kwenye mparaganyiko fulani hivi wa kimfumo. Wakati Putin alikuwa anateuliwa kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu lakini nafasi ya Waziri Mkuu ilikuwa wazi. Ndani ya muda wa chini ya miezi kumi na tatu, walikuwa wameteuliwa Mawaziri Wakuu wane tofauti na kufukuzwa. Uteuzi huu wa Putin kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri mkuu ulitangazwa asubuhi ya tarehe hiyo 9… lakini ajabu sana ilipofika majira ya jioni siku hiyo hiyo Putin aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Russia.

Mkakati… Abramovich… Abracadabra…

Uteuzi wa Putin kuwa Waziri Mkuu mwanzoni haukushitua sana watu japokuwa hakuwa na umaarufu kwa wanasiasa wala wananchi kwa sababu kama ambavyo nimeeleza kuwa kwa muda wa kama miezi kumi na tatu tu tayari kulikuwa na Mawaziri Wakuu wane walioteuliwa na kufutwa kazi. Kwa hiyo watu walikuwa wanamuhesabia siku tu Putin kabla yay eye pia ‘kutumbuliwa’… ni kama vile hapa kwetu nchini, ukiteuliwa kuongoza Wizara ya Maliasili na Utalii au Wizara ya Nishati na Madini… watu wanakuhesabia miezi tu.

Lakini siku tatu tu baada ya uteuzi wa Putin, Rais Boris Yeltsin alifanya kitu cha tofauti kulinganisha na Mawaziri Wakuu waliopita ambao aliwahi kuwateua. Katika hotuba yake kwa wananchi alitamka kwamba anatamani Putin awe mrithi wake wa kiti cha Urais siku akiondoka kwenye cheo hicho… wenye kusoma alama za nyakati wakaelewa nini kilikuwa kinaendelea. Hii haikuwa ile ‘teau kisha fukuza’. Putin alikuwa anaandaliwa kuchukua nchi.

Kwa hiyo wapinzania wa Yeltsin au tuseme wapinzani wa ‘The Family’ wakaanza kujipanga kuzuia hicho ambacho kilikuwa kinataka kutokea. Iikuwa wazi kwamba Yeltsin amebakiza muda mchache madarakani, kwa wapinzani wa ma-oligarch hii ilikuwa habari njema kwao kwamba walau sasa na wao watapata zamu yao kufaidi mema ya nchi. Lakini baada ya kauli ya Yeltsin kwamba anatamani kurithiwa kiti cha Urais na Putin walielewa kwamba huu ulikuwa ni mkakati wa kuanza kumnadi Putin kwa wananchi. Kwahiyo nao wakaanza mipango ya kukwamisha suala hilo lisifanikiwe.

Sasa,

nimeeelza kwenye sehemu zilizopita kwamba Yeltsin alikuwa na upinzani mkubwa sana kwa wanasiasa wengine. Upinzani huu ulikuwa na historia ndefu hata kabla hajaanza kuwalimbikizia mali ma-oligarch.

Tutazame kidogo kwa ufupi sana… Shirikisho la Russia lilivunjika December, 1991. Kama mwezi mmoja hivi baadae, yaani January, 1992 Rais Yeltsin alianzisha program mpya kukabiliana na hali ya mbaya ya kiuchumi ambayo ilisababishwa na kuvunjika kwa Shirikisho la Russia. Badala ya program ile kusaidia badala yake ilifanya hali ya kiuchumi kuwa mbaya zaidi. Yeltsin alipingwa vikali mno kwa sera hizo mpya ambazo alizianzisha kiasi kwamba mpaka makamu wake wa Rais alikuwa anazikosoa hadharani kabisa. Likatokea wimbi la wanasiasa wengi hata wa chama chake kujiweka mbali na Yeltsin na kujipambanua kupinga sera hizo mpya za kiuchumi za Yeltsin. Matokeo yake ni kwamba Yeltsin alikuwa akipeleka miswada au mapendekezo Bungeni ili yapitishwe yalikuwa yanakwamishwa makusudi ili kumkata makali ya kutekeleza sera zake za kiuchumi. Kipindi hicho Bunge la Russia lilikuwa linaitwa “Supreme Soviet”. Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Yeltsin na Bunge hatimaye Yeltsin akatangaza kulivunja Bunge. Sasa katiba ya Russia kipindi hicho ilikuwa haimpi mamlaka Rais kulivunja Bunge, kwa hiyo wabunge wakagoma na wakawa wanaendelea na shughuli za kibunge. Yeltsin akaingiza vifaru vya kijeshi kwenye viwanja vya bungeni kutaka kuwatoa wabunge kwa lazima. Wabunge wakagoma… wafuasi wao wakaandamana mitaani pale Moscow… kukatokea mapigano makali kati ya wananchi waliokuwa wanaunga mkono bunge dhidi ya wafuasi wa Yeltsin na jeshi. Inakadiriwa karibia watu 1,500 walipoteza maisha kwenye yale mapigano na kuyafanya kuwa moja ya tukio baya zaidi kwenye historia ya Russia.

Loh.! Nanogewa nichambue zaidi historia hii ya Russia… but let’s cut a long story short. Mapigano yale yalidumu kwa muda wa kama wiki mbili hivi kabla ya Rais Yeltsin na Bunge kufikia muafaka. Bunge walimpa masharti kadhaa ili waendelee kufanya naye kazi ‘smoothly’ na yeye Rais Yeltsin akatoa matakwa yake.

Moja ya makubaliano makuu ilikuwa ni kuunda upya mfumo wa Bunge la ‘Supreme Soviet’. Yeltsin alihisi kwamba Bunge lilikuwa limepewa mamlaka makubwa mno kutokana na mfumo wa kijamaa ambao ulikuwa unatumika kuendesha nchi huko nyuma. Chini ya mfumo huu mpya, kwanza ‘supreme soviet’ litavunjwa na kuundwa ‘Federal assembly’ ambayo itakuwa na ‘chamber’ mbili. Kutakuwa na ‘Lower House’ kwa jina State Duma (au GosDumas kama warusi wenyewe wanavyooita), na pia kutakuwa na ‘Upper House’ kwa jina la Council of the Federation. (Mfumo huu bado ungali unatumika mpaka sasa).

Kwanini nimegusia historia hii? Kuna vitu viwili ambavyo nataka uvione… kwanza ni uhasama wa Bunge na rais Yeltsin kwani hata baada ya mfumo mpya kuwekwa Bunge bado lilikuwa na kinyongo naye kutokana na kile ambacho kilitokea.

Na jambo la pili nataka tufahamu kwamba ile lower house ya Bunge (State Duma) ndiyo ambayo ilikuwa na malamlaka ya kumthibitisha Waziri Mkuu mara baada ya kuteuliwa na Rais.

Sasa,

Bada ya kauli ya Yeltsin kwamba anatamani Putin awe mrithi wake wa kiti cha Urais, wapinzani wa ‘The Family’ wakaanza kampeni ya chini kwa chini kushawishi wabunge wa GosDumas kumpiga chini Putin.

Putin alikuwa anahitaji kura 226 ili kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu.

Kambi ya Yeltsin ikagundua njama hii na mara moja wakaanza kuifanyia kazi. Wanasema pesa sabuni ya roho… haijalishi ni kabila gani au nchi gani… pesa inaweza kubadili moyo wa binadamu. Ma-oligarch wakaingia kazini kumwaga fedha kwa wabunge wa GosDuma.

Siku ya August 16 kura zilipopigwa Putin aliponea chupu chupu kwa kupata kura 233. Kura saba tu zaidi.

Kwa hiyo rasmi sasa Putin alikuwa ni waziri Mkuu wa Russia.

Hatua ambayo ilikuwa inafuata ilikuwa ni kumjenga Putin kwenye mioyo ya wananchi. Kama ambavyo nimeeleza… vyombo vya habari vyote vilikuwa vinamilikiwa na ma-oligarch. Kwa hiyo kila siku vilikuwa vinaandaliwa vipindi malumu vya redio na televisheni… makala kwenye magazeti na makongamano na mikutano ya hadhara… vyote kumuhusu Vladimir Putin.

Lakini moja ya matukio ambayo yalisaidia kumuweka Putin kwenye mioyo ya warusi ilikuwa ni namna ambavyo alishughulikia tafrani ambayo ilitokana na kulipuka kwa mabomu kwenye nyumba za kupanga kwenye miji mitatu nchini urusi… tukio ambalo linajulikana kwa jina maarufu la ‘Russia Appartment Bombings’. Tukio ambalo lilizua hofu kubwa ndani ya Urusi. Putin alionyesha ukakamavu wa hali ya juu na umahiri kulishughulikia suala hilo mpaka mwisho. Lakini pia Putin aliwakosha warusi kwa msimamo wake thabiti juu ya vita waliyokuwa wanaipigana Chechenya.

Miezi mitatu baadae, yaani mwezi December 1999 Rais Boris Yeltsin alijiuzulu ghafla na kwa mujibu wa katiba ya Rusia Waziri Mkuu ndiye anachukua nafasi yake na kuikaimu mpaka uchaguzi mkuu uitishwe.

Yeltisn alijiuzulu tarehe 31 December 1999… siku hiyo hiyo Putin akatangazwa kuwa Kaimu Rais wa Russia. Na siku hiyo hiyo akasaini ‘decree’ ya kwanza na muhimu sana kwenye historia ya Urusi. Decree hii ilikuwa na kichwa kinachosema, “On Guarantees of former President of the Russian federation and members of his family”. Decree hii iikuwa inatoa kinga kwa Rais Yeltsin na wanafamilia wake wote kwamba hawatashtakiwa kwa makosa yoyote yale kama ikionekana labda kulikuwa na makosa yoyote ambayo yalitendeka kipindi cha Urais wa Yeltsin.

Na hii ilikuwa ni moja ya makubaliano kati ya Yeltsin na Abramovich kwa niaba ya ma-oligarch wenzake walipomtaka aachie ngazi… alitaka ahakikishiwe kwamba mali zake hatopokonywa na kamwe asishtakiwe.

Miezi mitatu baadae, Putin aliitisha uchaguzi mkuu ambao alishinda kiulaini kabisa. Tarehe 7 May 2000, Vladimir Vladimirovich Putin alikula kiapo kuwa Rais wa Russia.

Kazi ilikuwa imekamilika…. Abramovich… abracadabra.!!

Swahiba wake ambaye ‘amemfinyanga’ kwa mikono yake na kumtengenezea njia sasa alikuwa amekalia kiti cha urais wa nchi.

Kuna kitabu kitakatifu kinasema “tunakua kutoka utukufu mpaka utukufu”. Na haswaaa, hii ndio hulka yetu binadamu… haijalishi tuko kileleni kiasi gani… siku zote tunataka kuipanda ngazi inayofuata. Hata uwe na kikubwa kiasi gani, nafsini tunaona tulichanacho bado hakitoshi… haijalishi tunacho kingi kiasi gani. Tunatamani, tunatafuta, tunakipata alafu tunataka zaidi… wanadamu tumeumbwa na kiu ya “kukua kutoka utukufu mpaka utukufu”.

Huu sasa ulikuwa ni wakati wa Abramovich kuhamia katika hatua ya pili ya ndoto zake… ndoto kubwa zaidi. Unaweza kudhani kumiliki Sibneft kampuni kubwa zaidi ya kuzalisha mafuta nchini Russia ilikuwa inatosha.. la hasha… Roman Abramovich alikuwa anataka zaidi, na alichikuwa anakitaka safari hii kilikuwa kimono zaidi pale Russia.. Abrfamovich alikuwa anataka kujimilikisha sekta ya Aluminum ndani ya nchi ya Russia. Sekta yenye utajiri mkubwa zaidi nchini Russia lakini pia ikiwa ni sekta hatari zaidi.

Kuingia kwa Abramovich kwenye sekta hii kutakuja kuibua moja ya nyakati za hatari zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Russia na Ulaya mashsriki yote kiasi kwamba mpaka leo hii kipindi hicho kinajulikana kama nyakati za ‘Vita za Aluminum’.

Tutajadili…

Kuhusu ishu ya Vitabu...

Noana kuna jambo nasisitizwa sana, VITABU.

Niliwahi kutangaza kutoa kitabu lakini sijawapa tena update yeyote.

Kuna changamoto imetokea na nilikuwa sitaki kuizungumzia ndio maana kwa mwaka mzima sijasema chochote kuhusu kile kitabu ambacho niliwapostia mpaka picha yake kwamba tayari kinachpwa. Lakini nadhani ni vyema nilisemee mara moja ili walau mnielewe nini kimetokea…

Ni kwamba kwenye kile kitabu kuna hii makala ya ya Ujasusi Sebuleni Kwetu na makala ya The Richest Man. Hizi makala zote zinahusu masuala ya kiusalama hapa Afrika Mashariki.

Nadhani mnaona hali za kiuslama hapa katikati ilikuwa tete kidogo Afrika Mashariki… Kuna mabwana wakubwa wanahisi kwamba hizo makala zina taarifa sensitive na kwamba si vyema zikienda public... so kitabu kikapigwa stop kabla ya kuuza hata nakala moja. Nikafosi kutoa nakala mia moja tu na kuwapa watu waliopo kwenye group langu whatsapp kwa masharti. But sijawahi kumpatia mtu mwingine yeyote nje ya hao na ndio maana hata humu sijawahi kuwaeleza kinapatikanaje.

Taarifa gani hizo sensitive? Wajua, mie humu JF nikionana akiana 'chogo' wanakuja kubeza sijui oooh hii iko google sijui nini nini... huwa nawaangalia nabaki nacheka tu hiiiiiiii... ubaya tumekutana tu hapa JF hakuna anayejua undani wa mwenzake.

Niseme tu kwa haya masuala ya intelijensia Afrika Mashariki nina access ya kupata taarifa kubwa ambazo hata haziko mitandaoni au mtaani. Na kwa kusema hivyo sitaki kumaanisha kwamba labda mie niko pale Oysterbay/K.nyama... hapana, siko huko na sijawahi kuwepo. But nikihitaji intelijensia kuhusu masuala ya Afrika Mashariki najua naipataje… wale mlioko kwenye group nadhani mnafahamu vitu ambavyo mara kadhaa huwa najadili kule kuhusu masuala ya ulinzi na usalama hapa Afrika Mashariki.

Anyways… hiki ndicho kilitokea na sababu kwa nini mpaka sasa nashindwa kutoa kitabu. Ningeweza kutoa kitabu kwa kuondoa makala hizo mbili but nahisi ule ‘umaalumu’ wa kitabu utaondoka. Kwa hiyo bado nakomaa, maana kuna watu wapya pale sasa hivi naamini tutaenda sawa…na mimi mtiifu sana kwa nchi yangu, nawasubiri wao wanipe go ahead ndio nikitoe...

Sikutaka kusema haya muda wote huu maana JF imejaa wajuaji na ungeibuka mjadala ambao hauna maana wala tija… but imebidi niseme maana naona kama hapo juu kuna comment nyingi sana kuhusu kitabu na kwa nini sikitoi wakati nilishatangaza.

Bold - 0718096811

To Infinity and Beyond
Asante kwa kazi nzuri iriyotukuka mkuu,
Wakati mwingine usisahau kunitag na mimi
 
Ushauri kwa mleta story unatakiwa kulisaidia taifa lako hasa kuwajenga kupenda kusoma ili wawe na maarifa Zaid kusud kizazi chako kisijekupata tabu huko mbele kwajinsi dunia inavyokwenda.

Hii story unayondefu tuu lakin kwamakusud baada ya kuona unabembelezwa sana Basi nawe unajidai kuringa hakuna cha muda Wala nn ila unacreate attention kwa watu watu washakujua wewe n Nani na shughuli za hadithi Kama hz n Moja ya shughuli zako na humu jf n maarufu kwa Hilo watu washakwambia Kama n pesa waambie wakutumie naona ukaja juu Kama hutak pesa Sasa ile namba yasimu unaweka Yann?

Watu wanasema huko insta Mara wasp ipo mbele Sasa huku jf maarifa kugawana n bure pili ukileta hapa ikiwa full n rahis nawewe kuongeza tuvitu fulan sababu tunaishi kujifunza kilasiku

Hii story ipo Google Sana tuu unadham watu hawajaitafuta washaitafuta na wengine hata hawakujisumbua sababu wanajua ile lugha ile n shida ndo Mana nitag nnying mno toka unaandika ile siku ya kwanza mpakaleo nitag nitag

Copy lote paste hapa

Naheshimu muda wako uliojipa ukatafsir hi kitu inasaidia kuwapa chakula ya ubongo watanzania waanze kufikiri Sasa dunia ilivyo nasio kulaumulaumu tuu watu.

Hongera kwa kazi ya vidole vyako
Mi nawashangaa watu wanaolalamika story iendelee huwa hawana majukum au kazi zakufanya mpaka wanawaza story?mi huwa nasoma inapoishia ndo hapohapo naisahau kabisa siku nikiingia nikiiona ndo naendelea nayo yani siweki kichwani kwamba kuna story sijaimaliza.
 
Historia tamu sana hii, pia upo sahihi, iyo makala hasa ya richestman itoe. ila.uko vuzuri. ni tag makala ya tisa
 
Mi nawashangaa watu wanaolalamika story iendelee huwa hawana majukum au kazi zakufanya mpaka wanawaza story?mi huwa nasoma inapoishia ndo hapohapo naisahau kabisa siku nikiingia nikiiona ndo naendelea nayo yani siweki kichwani kwamba kuna story sijaimaliza.
mkuu huku kuna mafala lever ya facebook
 
ROMAN ABRAMOVICH: UTAJIRI WA DAMU, RISASI NA UMAFIA

SEHEMU YA NANE

Hakuna kitu kizuri kama kiongozi ambaye anaweza kujitathimini na kukubali mapungufu yake na kukubali kukaa pembeni kupisha wengine. Mtu wa namna hii hata kama kuna madudu aliyafanya unajikuta unapata nafasi ya kumsamehe moyoni.

Licha ya mapungufu yake yote na vituko juu ya vimbwnga alivyovifanya kuidharaulisha Russia, lakini ulipofika wakati na kuelezwa ukweli kwamba ni muda muafaka akae pembeni kupisha mtu mwingine, Boris Yeltsin hakuifanya shingo yake kuwa ngumu.

Roman Abramovich akakutana na ma-oligarch wenzake. Akawapa pendekezo lake la nani anadhani anafaa kuwa rais mpya wa Russia. Akaweka sababu zake mezani… ma-oligarch wakakubaliana naye.

Nilieleza kwamba wale wanaojiita ‘The Family’ ambao ni ma-oligarch na wanafamilia ya Yeltsin kimsingi ndio ambao walikuwa wanaendsha nchi. Na ndani ya The Family kulikuwa na ule ‘Utatu Mtakatifu’… Abramovich, Tatyana na Yumachev. Na katika kipindi hiki Abramovich alikuwa na nguvu ya ushawishi kwa Yeltsin kuwazidi wote hata ndani ya The Family na Utatu Mtakatifu.

Kwa hiyo ulipofika wakati wa kuzungumza suala hili zito na Yeltsin… ni Abramovich pekee yake… yeye na Yeltsin pekee walijifungia ofisini na ‘kuyajenga’.

Kwanza Abramovich alimueleza Yeltsin kwa nini huu ni muda muafaka yeye kukaa pembeni na kumpisha kiongozi mpya. Baada ya Yeltsin kuukubaliana na hili, Abramovich akamueleza kuhusu pendekezo la mrithi wake. Abramovich akamueleza kwamba anapendekeza Vladimir Vladimirovich Putin, Mkurugenzi Mkuu wa FSB aanze kuandaliwa kurithi kiti hicho cha Urais. Kama ambavyo aliwafafanulia ma-oligarch ndivyo pia ambavyo alimfafanulia Rais Boris Yeltsin.

Tarehe 9 August mwaka 1999 Rais Boris Yeltsin alimteua Vladimir Putin kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu. Yaani kipindi hicho ilikuwa kunakuwa na Waziri Mkuu alafu anakuwa na Manaibu watatu au wawili. Yaani mfano mzuri kama Zanzibar walivyo na ‘Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais’. Kwa hiyo Putin aliteuliwa kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu wa Russia. Nimeeleza kwamba kipindi hiki Russia ilikuwa kwenye mparaganyiko fulani hivi wa kimfumo. Wakati Putin alikuwa anateuliwa kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu lakini nafasi ya Waziri Mkuu ilikuwa wazi. Ndani ya muda wa chini ya miezi kumi na tatu, walikuwa wameteuliwa Mawaziri Wakuu wane tofauti na kufukuzwa. Uteuzi huu wa Putin kuwa Naibu wa Kwanza wa Waziri mkuu ulitangazwa asubuhi ya tarehe hiyo 9… lakini ajabu sana ilipofika majira ya jioni siku hiyo hiyo Putin aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Russia.

Mkakati… Abramovich… Abracadabra…

Uteuzi wa Putin kuwa Waziri Mkuu mwanzoni haukushitua sana watu japokuwa hakuwa na umaarufu kwa wanasiasa wala wananchi kwa sababu kama ambavyo nimeeleza kuwa kwa muda wa kama miezi kumi na tatu tu tayari kulikuwa na Mawaziri Wakuu wane walioteuliwa na kufutwa kazi. Kwa hiyo watu walikuwa wanamuhesabia siku tu Putin kabla yay eye pia ‘kutumbuliwa’… ni kama vile hapa kwetu nchini, ukiteuliwa kuongoza Wizara ya Maliasili na Utalii au Wizara ya Nishati na Madini… watu wanakuhesabia miezi tu.

Lakini siku tatu tu baada ya uteuzi wa Putin, Rais Boris Yeltsin alifanya kitu cha tofauti kulinganisha na Mawaziri Wakuu waliopita ambao aliwahi kuwateua. Katika hotuba yake kwa wananchi alitamka kwamba anatamani Putin awe mrithi wake wa kiti cha Urais siku akiondoka kwenye cheo hicho… wenye kusoma alama za nyakati wakaelewa nini kilikuwa kinaendelea. Hii haikuwa ile ‘teau kisha fukuza’. Putin alikuwa anaandaliwa kuchukua nchi.

Kwa hiyo wapinzania wa Yeltsin au tuseme wapinzani wa ‘The Family’ wakaanza kujipanga kuzuia hicho ambacho kilikuwa kinataka kutokea. Iikuwa wazi kwamba Yeltsin amebakiza muda mchache madarakani, kwa wapinzani wa ma-oligarch hii ilikuwa habari njema kwao kwamba walau sasa na wao watapata zamu yao kufaidi mema ya nchi. Lakini baada ya kauli ya Yeltsin kwamba anatamani kurithiwa kiti cha Urais na Putin walielewa kwamba huu ulikuwa ni mkakati wa kuanza kumnadi Putin kwa wananchi. Kwahiyo nao wakaanza mipango ya kukwamisha suala hilo lisifanikiwe.

Sasa,

nimeeelza kwenye sehemu zilizopita kwamba Yeltsin alikuwa na upinzani mkubwa sana kwa wanasiasa wengine. Upinzani huu ulikuwa na historia ndefu hata kabla hajaanza kuwalimbikizia mali ma-oligarch.

Tutazame kidogo kwa ufupi sana… Shirikisho la Russia lilivunjika December, 1991. Kama mwezi mmoja hivi baadae, yaani January, 1992 Rais Yeltsin alianzisha program mpya kukabiliana na hali ya mbaya ya kiuchumi ambayo ilisababishwa na kuvunjika kwa Shirikisho la Russia. Badala ya program ile kusaidia badala yake ilifanya hali ya kiuchumi kuwa mbaya zaidi. Yeltsin alipingwa vikali mno kwa sera hizo mpya ambazo alizianzisha kiasi kwamba mpaka makamu wake wa Rais alikuwa anazikosoa hadharani kabisa. Likatokea wimbi la wanasiasa wengi hata wa chama chake kujiweka mbali na Yeltsin na kujipambanua kupinga sera hizo mpya za kiuchumi za Yeltsin. Matokeo yake ni kwamba Yeltsin alikuwa akipeleka miswada au mapendekezo Bungeni ili yapitishwe yalikuwa yanakwamishwa makusudi ili kumkata makali ya kutekeleza sera zake za kiuchumi. Kipindi hicho Bunge la Russia lilikuwa linaitwa “Supreme Soviet”. Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Yeltsin na Bunge hatimaye Yeltsin akatangaza kulivunja Bunge. Sasa katiba ya Russia kipindi hicho ilikuwa haimpi mamlaka Rais kulivunja Bunge, kwa hiyo wabunge wakagoma na wakawa wanaendelea na shughuli za kibunge. Yeltsin akaingiza vifaru vya kijeshi kwenye viwanja vya bungeni kutaka kuwatoa wabunge kwa lazima. Wabunge wakagoma… wafuasi wao wakaandamana mitaani pale Moscow… kukatokea mapigano makali kati ya wananchi waliokuwa wanaunga mkono bunge dhidi ya wafuasi wa Yeltsin na jeshi. Inakadiriwa karibia watu 1,500 walipoteza maisha kwenye yale mapigano na kuyafanya kuwa moja ya tukio baya zaidi kwenye historia ya Russia.

Loh.! Nanogewa nichambue zaidi historia hii ya Russia… but let’s cut a long story short. Mapigano yale yalidumu kwa muda wa kama wiki mbili hivi kabla ya Rais Yeltsin na Bunge kufikia muafaka. Bunge walimpa masharti kadhaa ili waendelee kufanya naye kazi ‘smoothly’ na yeye Rais Yeltsin akatoa matakwa yake.

Moja ya makubaliano makuu ilikuwa ni kuunda upya mfumo wa Bunge la ‘Supreme Soviet’. Yeltsin alihisi kwamba Bunge lilikuwa limepewa mamlaka makubwa mno kutokana na mfumo wa kijamaa ambao ulikuwa unatumika kuendesha nchi huko nyuma. Chini ya mfumo huu mpya, kwanza ‘supreme soviet’ litavunjwa na kuundwa ‘Federal assembly’ ambayo itakuwa na ‘chamber’ mbili. Kutakuwa na ‘Lower House’ kwa jina State Duma (au GosDumas kama warusi wenyewe wanavyooita), na pia kutakuwa na ‘Upper House’ kwa jina la Council of the Federation. (Mfumo huu bado ungali unatumika mpaka sasa).

Kwanini nimegusia historia hii? Kuna vitu viwili ambavyo nataka uvione… kwanza ni uhasama wa Bunge na rais Yeltsin kwani hata baada ya mfumo mpya kuwekwa Bunge bado lilikuwa na kinyongo naye kutokana na kile ambacho kilitokea.

Na jambo la pili nataka tufahamu kwamba ile lower house ya Bunge (State Duma) ndiyo ambayo ilikuwa na malamlaka ya kumthibitisha Waziri Mkuu mara baada ya kuteuliwa na Rais.

Sasa,

Bada ya kauli ya Yeltsin kwamba anatamani Putin awe mrithi wake wa kiti cha Urais, wapinzani wa ‘The Family’ wakaanza kampeni ya chini kwa chini kushawishi wabunge wa GosDumas kumpiga chini Putin.

Putin alikuwa anahitaji kura 226 ili kuthibitishwa kuwa Waziri Mkuu.

Kambi ya Yeltsin ikagundua njama hii na mara moja wakaanza kuifanyia kazi. Wanasema pesa sabuni ya roho… haijalishi ni kabila gani au nchi gani… pesa inaweza kubadili moyo wa binadamu. Ma-oligarch wakaingia kazini kumwaga fedha kwa wabunge wa GosDuma.

Siku ya August 16 kura zilipopigwa Putin aliponea chupu chupu kwa kupata kura 233. Kura saba tu zaidi.

Kwa hiyo rasmi sasa Putin alikuwa ni waziri Mkuu wa Russia.

Hatua ambayo ilikuwa inafuata ilikuwa ni kumjenga Putin kwenye mioyo ya wananchi. Kama ambavyo nimeeleza… vyombo vya habari vyote vilikuwa vinamilikiwa na ma-oligarch. Kwa hiyo kila siku vilikuwa vinaandaliwa vipindi malumu vya redio na televisheni… makala kwenye magazeti na makongamano na mikutano ya hadhara… vyote kumuhusu Vladimir Putin.

Lakini moja ya matukio ambayo yalisaidia kumuweka Putin kwenye mioyo ya warusi ilikuwa ni namna ambavyo alishughulikia tafrani ambayo ilitokana na kulipuka kwa mabomu kwenye nyumba za kupanga kwenye miji mitatu nchini urusi… tukio ambalo linajulikana kwa jina maarufu la ‘Russia Appartment Bombings’. Tukio ambalo lilizua hofu kubwa ndani ya Urusi. Putin alionyesha ukakamavu wa hali ya juu na umahiri kulishughulikia suala hilo mpaka mwisho. Lakini pia Putin aliwakosha warusi kwa msimamo wake thabiti juu ya vita waliyokuwa wanaipigana Chechenya.

Miezi mitatu baadae, yaani mwezi December 1999 Rais Boris Yeltsin alijiuzulu ghafla na kwa mujibu wa katiba ya Rusia Waziri Mkuu ndiye anachukua nafasi yake na kuikaimu mpaka uchaguzi mkuu uitishwe.

Yeltisn alijiuzulu tarehe 31 December 1999… siku hiyo hiyo Putin akatangazwa kuwa Kaimu Rais wa Russia. Na siku hiyo hiyo akasaini ‘decree’ ya kwanza na muhimu sana kwenye historia ya Urusi. Decree hii ilikuwa na kichwa kinachosema, “On Guarantees of former President of the Russian federation and members of his family”. Decree hii iikuwa inatoa kinga kwa Rais Yeltsin na wanafamilia wake wote kwamba hawatashtakiwa kwa makosa yoyote yale kama ikionekana labda kulikuwa na makosa yoyote ambayo yalitendeka kipindi cha Urais wa Yeltsin.

Na hii ilikuwa ni moja ya makubaliano kati ya Yeltsin na Abramovich kwa niaba ya ma-oligarch wenzake walipomtaka aachie ngazi… alitaka ahakikishiwe kwamba mali zake hatopokonywa na kamwe asishtakiwe.

Miezi mitatu baadae, Putin aliitisha uchaguzi mkuu ambao alishinda kiulaini kabisa. Tarehe 7 May 2000, Vladimir Vladimirovich Putin alikula kiapo kuwa Rais wa Russia.

Kazi ilikuwa imekamilika…. Abramovich… abracadabra.!!

Swahiba wake ambaye ‘amemfinyanga’ kwa mikono yake na kumtengenezea njia sasa alikuwa amekalia kiti cha urais wa nchi.

Kuna kitabu kitakatifu kinasema “tunakua kutoka utukufu mpaka utukufu”. Na haswaaa, hii ndio hulka yetu binadamu… haijalishi tuko kileleni kiasi gani… siku zote tunataka kuipanda ngazi inayofuata. Hata uwe na kikubwa kiasi gani, nafsini tunaona tulichanacho bado hakitoshi… haijalishi tunacho kingi kiasi gani. Tunatamani, tunatafuta, tunakipata alafu tunataka zaidi… wanadamu tumeumbwa na kiu ya “kukua kutoka utukufu mpaka utukufu”.

Huu sasa ulikuwa ni wakati wa Abramovich kuhamia katika hatua ya pili ya ndoto zake… ndoto kubwa zaidi. Unaweza kudhani kumiliki Sibneft kampuni kubwa zaidi ya kuzalisha mafuta nchini Russia ilikuwa inatosha.. la hasha… Roman Abramovich alikuwa anataka zaidi, na alichikuwa anakitaka safari hii kilikuwa kimono zaidi pale Russia.. Abrfamovich alikuwa anataka kujimilikisha sekta ya Aluminum ndani ya nchi ya Russia. Sekta yenye utajiri mkubwa zaidi nchini Russia lakini pia ikiwa ni sekta hatari zaidi.

Kuingia kwa Abramovich kwenye sekta hii kutakuja kuibua moja ya nyakati za hatari zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Russia na Ulaya mashsriki yote kiasi kwamba mpaka leo hii kipindi hicho kinajulikana kama nyakati za ‘Vita za Aluminum’.

Tutajadili…

Kuhusu ishu ya Vitabu...

Noana kuna jambo nasisitizwa sana, VITABU.

Niliwahi kutangaza kutoa kitabu lakini sijawapa tena update yeyote.

Kuna changamoto imetokea na nilikuwa sitaki kuizungumzia ndio maana kwa mwaka mzima sijasema chochote kuhusu kile kitabu ambacho niliwapostia mpaka picha yake kwamba tayari kinachpwa. Lakini nadhani ni vyema nilisemee mara moja ili walau mnielewe nini kimetokea…

Ni kwamba kwenye kile kitabu kuna hii makala ya ya Ujasusi Sebuleni Kwetu na makala ya The Richest Man. Hizi makala zote zinahusu masuala ya kiusalama hapa Afrika Mashariki.

Nadhani mnaona hali za kiuslama hapa katikati ilikuwa tete kidogo Afrika Mashariki… Kuna mabwana wakubwa wanahisi kwamba hizo makala zina taarifa sensitive na kwamba si vyema zikienda public... so kitabu kikapigwa stop kabla ya kuuza hata nakala moja. Nikafosi kutoa nakala mia moja tu na kuwapa watu waliopo kwenye group langu whatsapp kwa masharti. But sijawahi kumpatia mtu mwingine yeyote nje ya hao na ndio maana hata humu sijawahi kuwaeleza kinapatikanaje.

Taarifa gani hizo sensitive? Wajua, mie humu JF nikionana akiana 'chogo' wanakuja kubeza sijui oooh hii iko google sijui nini nini... huwa nawaangalia nabaki nacheka tu hiiiiiiii... ubaya tumekutana tu hapa JF hakuna anayejua undani wa mwenzake.

Niseme tu kwa haya masuala ya intelijensia Afrika Mashariki nina access ya kupata taarifa kubwa ambazo hata haziko mitandaoni au mtaani. Na kwa kusema hivyo sitaki kumaanisha kwamba labda mie niko pale Oysterbay/K.nyama... hapana, siko huko na sijawahi kuwepo. But nikihitaji intelijensia kuhusu masuala ya Afrika Mashariki najua naipataje… wale mlioko kwenye group nadhani mnafahamu vitu ambavyo mara kadhaa huwa najadili kule kuhusu masuala ya ulinzi na usalama hapa Afrika Mashariki.

Anyways… hiki ndicho kilitokea na sababu kwa nini mpaka sasa nashindwa kutoa kitabu. Ningeweza kutoa kitabu kwa kuondoa makala hizo mbili but nahisi ule ‘umaalumu’ wa kitabu utaondoka. Kwa hiyo bado nakomaa, maana kuna watu wapya pale sasa hivi naamini tutaenda sawa…na mimi mtiifu sana kwa nchi yangu, nawasubiri wao wanipe go ahead ndio nikitoe...

Sikutaka kusema haya muda wote huu maana JF imejaa wajuaji na ungeibuka mjadala ambao hauna maana wala tija… but imebidi niseme maana naona kama hapo juu kuna comment nyingi sana kuhusu kitabu na kwa nini sikitoi wakati nilishatangaza.

Bold - 0718096811

To Infinity and Beyond
Naomba nitarg ukitupia Uzi mwingine
 
Back
Top Bottom