Rombo, Kilimanjaro: Watoto wawili wa familia moja wafariki katika ajali ya moto

Rombo, Kilimanjaro: Watoto wawili wa familia moja wafariki katika ajali ya moto

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Rombo. Watoto wawili wa familia moja wakazi wa Tarakea wilayani Rombo wamefariki baada ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi kuungua kwa moto.

Akitoa taarifa hiyo leo Ijumaa Agosti 20, 2021 Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Hamis Maiga amesema, tukio hilo limetokea jana usiku uliosababishwa na mshumaa.

Hamisi amesema watoto ambao mmoja ana miaka sita, na mwingine ana mwaka mmoja

"Mwanamke mmoja mwenye watoto wawili aliwasha mshumaa , baada ya kuwasha mshumaa akawa ametoka nje kidogo.

"Mshumaa alikuwa ameweka kwenye meza ya plastiki ndipo mshumaa ulipodondokea kwenye meza na kushika kwenye mabanzi ambayo yalishika moto na nyumba yote kuteketea" alisema Maiga.

Maiga amesema kwa sasa Kamati ya Ulinzi ya wilaya hiyo inaelekea kwenye eneo la tukio.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwanamke mmoja mwenye watoto wawili aliwasha mshumaa "baada ya siku zao kwisha" baada ya kuwasha mshumaa akawa ametoka nje kidogo.

Sijaelewa hapa ulimaanisha nini?
 
"yalishika moto na nyumba yote yenye mashtaka 10 ya kutetea," alisema Maiga

Nyumba yenye Mashtaka 10 ya kutetea ndo nyumba ya namna gani mkuu??
 
Mwanamke mmoja mwenye watoto wawili aliwasha mshumaa "baada ya siku zao kwisha" baada ya kuwasha mshumaa akawa ametoka nje kidogo.

Sijaelewa hapa ulimaanisha nini?
Makosa ya kiuchapaji TU!
 
Back
Top Bottom