Waafrika huwa tunamtetea okocha sababu ni mwenzetu! Ni kweli inawezekana okocha alikuwa na kipaji zaidi ya ronaldinho lakini alikosa vitu basic ambavyo ndio vilimuangusha!
Hata dinho mwenyewe ashawahi kusema okocha ndio namba 10 aliyokuwa anaipenda zaidi!
Sasa tujiulize zaidi ya psg, kwanini alishindwa kucheza timu kubwa akiwa katika ubora wake, madrid,barcelona,Liverpool,man u, ac milan, Juventus, intermilan, arsenal, Bayern Munich basi hata dortmund, valencia, chelsea, roma za kipindi hiko angecheza, ina maana hawa woote hawakuona ubora wake, mwishowe akaangukia bolton, Hull City huko.
Kuna kitu okocha alikosa msingi wa mpira, alikuwa fundi saana, ila wakati mwingine alikuwa anafosi mambo haya majanga naona hata kwa wachezaji wetu kina ajibu huku, kila muda anafosi kupiga outer, au ndemla kujipigia mashuti hovyo sababu ndio mashabiki wanaochomsifia! Anapiga auta hata kama sio ya lazima, wakati mwingine anapiteza mpira bure.
Ndio okocha wakati mwingine sehemu ya kuachia moja, atalazimisha kupiga ile chenga yake maarufu ya kutengua mtu nyonga mienapenda kuiita okocha feint! Sehemu ya kufanya kitu chepesi anafosi kufanya makubwa mwishowe anapoteza mpira ama anauwa move ya kwenda kushamubulia, ama anachelewesha mashambulizi. Na hivi alikuwa na nguvu za kupiga miguu yote ndio wakti mwingine anajipigia pigia tu hovyo. Sisemi alikuwa hapatii sometimes alikuwa anapatia na kufanya mazuri.
Tofauti na gaucho, gaucho alikuwa anafanya burudani zake bila kuharibu mipango ya timu, atapiga no look pasi ambayo ni hatari hata wapinzani hawakutegemea kama pasi itapiga huko! Atapiga vibaiskel kwenye motion, ataachi mali kwa wakati wa hatari zaidi langoni mwa mpinzani. Sisemi alikuwa hakosei ni kawaida kukosea kwa mwanadamu yoyote yule.
Kwangu nitasema ronaldinho gaucho.