Ronald De La Bere Barker 1889-1965. Mzungu aliyeishi kwenye mapori ya mto Rufiji.

Ronald De La Bere Barker 1889-1965. Mzungu aliyeishi kwenye mapori ya mto Rufiji.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Simulizi hizi unaweza kuzisoma Bure ndani ya app ya Maktaba Sauti. Ipo Playstore.

Huyu mzungu alizaliwa huko New Zealand. Baadaye akaja kuishi kwenye mapori ya mto Rufiji akiwa muwindaji. Majina yake mengine ni Mzee Rufiji au Mtawa maporini. Aliandika vitabu vinne vya kuchekesha sana juu ya maisha yake huko Maporini.

Kitabu cha kwanza: Jinsi nilivyofika na Kukaa Afrika.

DIBAJI

MZEE Rufiji au Baka (Barker) ametunga kitabu hiki kwa kutaka kuwafurahisha vijana. Vijana wa kimji na wa mashambani hamkosi mtakipenda sana kitabu hiki. Badala ya kwenda kilabuni ambako pengine upatikane na heka heka zisizo na maana, jisomee kitabu hiki, na vingine katika jamii hii vya huyu mzee ambaye si mwenyeji wa Afrika, lakini jinsi alivyo, tangu mwanzo wa tabia hata katika kuipenda kwake Afrika amekuwa naye Mwafrika mweupe.

Mimi ndiye Mzee Rufiji au Baka nijulikanaye sana karibu na watu wengi wa Afrika ya Mashariki, na pengi ulimwenguni kwa kazi yangu ya uwindaji. Nimepewa majina mengi na wenyeji wa Afrika niliopata kuishi nao katika taabu na raha. Nimepata kuitwa 'Bwana Ziraili' kwa jinsi nilivyozitoa roho za ndovu na wanyama wengi mwituni. Nimepata kuitwa 'Jitu Masoga' kwa masoga yangu, na majina mengi mengine; lakini lile langu la asili limeniselelea.

Vijana na mimi hufurahishana sana katika kila ninakotangatanga. Nawakumbuka wale watoto sita ambao habari zao niliziandika katika kitabu cha 'Masimulizi ya Mtawa Maporini: Kitabu cha Tatu' niliokwenda nao kuwinda hata tukatokewa na simba saba. Watoto hawa wa Kibantu waligeuza silaha kila walichokuwa nacho za kushambuliana na simba wale. Vitu vyenyewe walivyokuwa navyo vilikuwa ni machungwa, darubini, kofia, picha na birika.

Haya basi zisomeni wenyewe hadithi hizi zangu mie; natumaini hakuna atakayeanguka kutoka juu ya pikipiki kama alivyoanguka Mzungu mmoja rafiki yangu aliyezikumbuka hadithi zangu nilizomuhadithia alipokuwa akiendesha pikipiki na kucheka mpaka akaanguka.

MZEE 'RUFIJI'
 
1. NILIVYOSELELEA AFRIKA

VITA kuu ya 1914-1918, jeshi letu lilipofika Mombasa mwaka 1915, nilichaguliwa kwenda kuwaangalia wapagazi wa mizinga ya mahandakini kwa kuwa nilikuwa ni mimi tu niliyejua Kiswahili kuliko Wazungu wengine tuliokuwa nao. Kisha nikapewa kazi ya upelelezi pamoja na kikosi cha maskauti wa kienyeji ambao hapo kwanza walikuwa viongozi wa Wazungu waliokijakija Nairobi kwa kutaka kuwinda au kukagua nchi.

Basi mpaka hivi leo bado nimo katika masikani ya kibantu. Vita kuu hiyo ya kwanza, Afrika ya Mashariki imepoteza maisha ya watu zaidi ya laki kuliko vita ya Boer. Huku Afrika ya Mashariki vita iliendelea zaidi kuliko Ulaya. Mwisho wa vita ulipotangazwa Ulaya, tarehe 11 Novemba 1918, huku kulikuwa bado na kivumbi cha kutosha mpaka maadui walipofukuziwa Northern Rhodesia kutoka Tanganyika. Wakati huo nikawa mkalimani wa Askari wa farasi na baadaye kidogo skauti tena pande za Mozambiki ambako maadui walirudishwa nyuma baada ya kujaribu kuteka zana na chakula katika ngome zetu.

Vita ilipokwisha nikawa Bwana Shauri katika nchi ya Kenya niliyefungua Boma la Kisii. Kisha nikafanya kazi ya Polisi katika baraza za mahakimu kadha wa kadha. Kazi hii ikanifikisha mpaka Ruanda. Kwa kuwa kazi hii ilihusiana na misitu na nyika tu, moyo wangu ukatokea kuipenda sana kazi hii niliyonayo sasa yaani kuwinda, ambayo hata nilipokuwa Bwana Shauri huko Kenya niliwahi kuifanya pengine pengine. Basi kazi hii ya kuwinda ikanipeleka Tanganyika ya kusini ambayo ni pori moja tu kubwa lenye wanyama wengi ajabu. Wawindaji wachache sana wanaolijua pori hili nilihadithialo la Tanganyika ya kusini. Huko nikatanga maporini hovyo. Wanyama, hasa ndovu, walibidi wauawe kwa jitihada zote zinazowezekana na binadamu kwa jinsi walivyokuwa waharibifu wa mengi. Mabwana Nyama na Askari nao walijilazimisha kujitahidi kuwateketeza kama walivyoweza. Nami nikaruhusiwa kupiga ndovu thelathini kwa mwaka mmoja na ndovu watatu kila mwaka kwa cheti cha ushuru wa biashara ya meno au pembe za ndovu.

Miaka hiyo ninayoihadithi nilikuwa na vijana jasiri waliokuwamo katika msafara wangu wa kuwinda. Baadaye nilipokuwa nikifanya kazi ya kuwinda viboko katika nchi ya Rufiji, ambako kazi ilikuwa ya hatari zaidi kuliko ile ya kuwinda ndovu, vijana hao walikuja tena kuandika kazi. Kama tujuavyo, kujitosa mitoni na mabwawani katika nchi ya Rufiji, mwenye mijimamba ya umambani, ni jambo lisilofikiriwa kabisa na Mrufiji wa Rufiji. Walilazimika wajitose kumfuata kiboko aliyekufia katikati ya bwawa ili aletwe maji haba apate kuchanjwa (kupasuliwa au kuchunwa kwa kuitafuta ile faida yake ambayo ni mafuta, ngozi na meno). Jinsi nilivyoungana na wafanya kazi hawa, ilikuwa kama wote ni ndugu kabisa. Wakicheka hucheka, na wakifanya kazi huifanya. Sote tukapendana. Mimi nikawa ni mkubwa wao niliyependwa sana. Maisha haya yakaniongoza katika ukweli wa dunia. Niliyoyaona yatosha kunihakikisha kwamba sisi binadamu wote ni wamoja tu tuliotofautishwa kwa rangi na hali ya nchi mbali mbali.

Kwa mengi vijana hawa walifanana na vijana wengine niliokuwa nao Canada, New Zealand, Amerika, Uingereza, Ufaransa na pengi pengine. Kwa mfano ukatili juu ya wanyama uko katika watoto wa Kizungu na wa Kiafrika. Jambo hili laonyesha jinsi tabia zilivyofanana.

Mtumishi wangu Juma, niliyeandika habari zake katika vitabu vya 'Masimulizi ya Mtawa Maporini', ni mmojawapo katika mia wanaoambatana na wawindaji wa Kizungu kwa kuelekea. Wengi kama Juma wamewatunza mabwana wao wa Kizungu maporini, wamewaokoa katika hatari kubwa hata pengine wamepata kuwaulia ndovu wenye pembe kubwa kubwa na kuwapatia faida nyingi sana.

Juma alikuwa mjanja wa kupendeza. Siku moja nilipiga risasi tano kwa swala watano lakini risasi zote ziliwapitia chini ya kidari na kuwakosa. Tulipofika kambini Jumbe mmoja mroho wa nyama akaja kuuliza kama kuna nyama au hakuna, Juma akamjibu hakuna. "Mbona nimesikia mishindo mitano?" Jumbe akamwuliza. "Ikiwa haja yako ni mishindo mitano," Juma akajibu, "basi chukua." Jumbe akasema, "Wacha utani bwana, niambie kweli." Juma alipoona anataabishwa na yule Jumbe, akasema, "Mishindo mitano uliyoisikia ilikuwa ya furaha ya harusi.” Siku moja nilipokuwa nakwenda kuwinda na wavulana wengine nilimwuliza Juma atafanya nini atakapokuwa anaangalia kambi maana sikutaka akae bure kama jeta. Akageuka na kutazamatazama kibanda changu cha nyasi kilichojaa mashoka ya kuchanjia viboko, kiti changu cha ngozi kilichokuwa chini ya mkuyu uliojaa ninga tele, kisha akasema, "Nafikiri nitapiga deki na kusafisha vioo vya madirisha leo."

Asubuhi moja alinijia na mjusi mdogo mkononi mwake akichekacheka. Kwa kando yetu kidogo kulikuwa na mpilipili hoho mahali palipokuwa kibanda cha jamaa fulani hapo kwanza. Akauendea ule mpilipili, akausafishia na kuujengea uwigo mdogo, kisha akamtia yule mjusi ndani yake. Akaja nilipokuwa akasema, "Je, unaionaje bustani yangu?"

Nilipokuwa Dar es Salaam katika nyumba ya bibi mmoja, watoto wake walinirukia na kunishangalia kama walipata kuniona zamani. Siku ya pili katika ofisi ya bwana mmoja paka akanirukia pia. Yule bwana akasema kwamba mimi nilikuwa mtu wa kwanza aliyenifanyia vile. Katika nchi ya Rufiji kila mara watoto walikuwa wakisukuma basikeli yangu mahali palipoinuka kidogo karibu na kambi yangu. Siku moja walipokuwa wakisukuma hivi, nikaona basikeli yangu inayumba; nilipotazama nyuma, nikamwona mmoja amepanda juu ya kitako cha nyuma. Jinsi nilivyokuwa nikipendwa na kuzoewa kwa upesi na viumbe wenzangu yasangaza sana.

Nakumbuka nilipokuwa mwalimu Sydney, niliona taa zinawaka katika ukumbi wa kulala watoto usiku nilipokuwa natoka sinema. Nikavua viatu vyangu nikawanyatia wale watoto waliovunja amri yaani kuwasha taa saa ile. Nilipofika juu nikawaona watoto wawili wa matajiri wakubwa sana, wengine wawili wa kawaida wamelizunguka beseni lililojaa biskuti, maziwa ya kopo, chokoleti, mikate na samaki wa kopo wakila kwa mikono huku wakifyonza vidole vyao. Nikajikohoza kidogo ili nipate kuwashitua. Wote wakaacha kula na mmoja akageuka taratibu sana. Aliponiona tu, akaendelea kula na kuwaambia wenzie, "Ah, kumbe mwalimu Baka tu huyo, karibu mwalimu ndiyo hivyo tena." Nikawaambia ningelikula kama wasingelichanganya na wale samaki wa kopo. Asubuhi yake wote walikubali maneno yangu.
 
2. NDOVU KISIMANI

MVUA za masika zilikuwa karibu zianze mwaka 1923 nilipokuwa nimekaa katika kiti cha chanja penye meza ya chanja pia, maporini Kilwa ya kati. Kama ilivyo kawaida ya wenyeji, majani yalikuwa yamekwisha chomwa. Ardhi ilikuwa ya moto kwa jua iliyowatia malengelenge wapita njia. Kwa ajili hii wenyeji mara kwa mara hupenda kusafiri usiku. Huonelea heri kukutana na minyama ya hatari usiku kuliko taabu ya jua linaloweza kumtia mtu uwete mara moja.

Kimbunga kikapita na kufanya majivu ya majani na takataka nyingine nguzo ndefu zilizopinda angani. Mtoto aliyekuwa na kisu mkononi kama vile visu vya watoto wa Kirufiji vinavyotengenezwa makusudi kwa kulia embe akanijia taratibu kama siye. Upepo ulipovumia usoni kwake na kumfukiza kwa vumbi, aligeuka na kwenda kinyumenyume mpaka akanifikia.

Akasimama chini ya kibanda changu cha makuti ya miaa akaegemea nguzo mojawapo na kuzidi kuendelea kuchonga kijiti chake. Jinsi alivyoonekana alikuwa kama amekuja kutembea tu wala hakuwa na neno lolote la kusema. Alichokuwa akichonga ilikuwa panda ya manati. Baada ya kitambo kidogo akasema kama yeye siye. Bila ya kujali akasema hadithi yake kwa kuirahisisha na wingi wa dharau. Akanitazama kipembe na kwa chiki kisha akasema,

"Unaitwa."

"Na nani?"

"Wanawake."

"Wanawake gani?"

"Wako kisimani. Uchukue bunduki na risasi mbili.'

"Kwa nini?”

"Ndovu."

Basi ili mradi yule mtoto maneno yake yakawa ya mkato mkato tu. Nilishangazwa kusikia kuwa kuna ndovu kisimani jua kali lote lile. Kwa kawaida ndovu huja usiku kisimani pale kunywa maji na kuondoka alfajiri na mapema wakiacha harufu na mabonge ya vinyesi vyao.

Nikachukua buhamsa yangu pamoja na pakiti mbili za risasi. Nikampa yule mtoto mkongojo wangu ninaoegemezea bunduki kwa kutaka shabaha nzuri anichukulie. Hupunguza hasara ya kupoteza risasi hovyo mkongojo huu; pia waweza kutundika kofia au kitu kingine katika panda zake ulizonazo popote unapotaka kupumzika.

Momadi, yule mtoto aliyekuja kunita, akatangulia na mimi nikamfuata. Nikazifupisha hatua zangu kutaka tuwe sawa na Momadi. Ingawa kweli mtoto yule jina lake lilikuwa Mohamedi, lakini pande za huku hasa maporini kama niliko, wote wenye majina ya Mohamedi huitwa Momadi; kwa hiyo hatuna budi tumwite na sisi Momadi pia. Utawasikia kila mara wakiitwa, "Awe Momadi we!". Kwa mbele yetu katika mionzi ya jua mikali ile iliyotutetemesha, tukaona kama kitu fulani hivi. Tulipokaribia, tukawaona wanawake watano wamekaa chini ya kivuli cha mti mkubwa kando ya barabara. Walikuwa wamezama wenyewe katika soga lao la kike. Hata hawakusikilizana kwa lele lele zilizofudikiza.

"Mzee Baka huyo jamani." Mwanamke mmoja akasema akiondoa kata yake kichwani. Kisha yule mama bila ya kusema lolote kanionyesha kijia kilichoelekea kwenye mianzi. Nilipotazama nikawaona ndovu wawili madume wamesimama kwenye mchanga mweupe uliopasua macho kwa mwanga wa jua. Bonde hili lenye mchanga mweupe, ni mto Ngarambe ambao sasa ulikuwa umekauka kabisa kabisa.

Upepo ulivuma hovyo kabisa; yaani ulitoka kila upande na kuchanganyika. Ulikuwa si wakati wa kuwinda hata kidogo. Ndovu mmoja aliinua mkonga wake juu akitafuta harufu za maadui zake binadamu. Walikuwa tayari kwa kila hali kwani walijua bila shaka binadamu watawatia msukosuko kwa kuja kisimani jua kali lote lile. Masikio yao kama ungo yakapepea huku na huku yakitega sauti yoyote watakayoidhani ni ya hatari. Si misikio hiyo, ilikuwa kama nyungo za kupetea vyakula vya majitu ikipetapeta hewani. Yule mwingine naye alipoinua mkonga wake tu juu wote wawili bila ya kukawia wakaziachia mbio. Walikwisha pata harufu yetu. Hao wakaenda zao mpaka wakajitoma katika pori la miti mibichi iliyokuwa kando ya mto ule mkavu wa Ngarambe. Ingawa mto ulikuwa umekauka kabisa, miti hii ilipata maji kutoka chini sana kwa mizizi yake mirefu iliyokuwa nayo.

Sikuwafuata. Momadi akatumwa kwenda kumwita baba yake na jembe la kuchimbia. Alipofika, yeye na wale wanawake wakachimba tena kile kisima upya. Kisima kilikuwa kimefunikwa na michanga kwa mikanyago ya midudu mizito ile yenye ratili mia tisa. Mavi yao yaliyojaa miba na kokwa za ngongo, peke yake yanaweza kumtoa mtu jasho kuyazoa. Midude hii inayotembea hovyo maporini hadi inachusha kwa jinsi ilivyo.

Jinsi wanavyokula kwa utaratibu, yastaajabisha kuona kinyesi kingi kama kile. Labda usiku wanakula sana na upesi upesi.
 
Lazima aliua, kubaka, na kuwadhalilisha Waafrica wenzetu huko..
Zaidi ya kujifuaisha yeye mwenyewe na Familia yake na Wazungu wenzake, aliwafanyia nn Waafrica wa Rufiji?
 
Lazima aliua, kubaka, na kuwadhalilisha Waafrica wenzetu huko..
Zaidi ya kujifuaisha yeye mwenyewe na Familia yake na Wazungu wenzake, aliwafanyia nn Waafrica wa Rufiji?
Jamaa alikuwa muwindaji wa Tembo na Viboko. Miaka hiyo kuwinda hao wanyama haikuwa ujangili, watu wa Rufiji walimpenda sana. Alikuwa akiwasaidia kuua tembo walioharibu mazao yao. Pia aliwapa ajira kwenye kazi zake za uwindaji.
 
1. NILIVYOSELELEA AFRIKA

VITA kuu ya 1914-1918, jeshi letu lilipofika Mombasa mwaka 1915, nilichaguliwa kwenda kuwaangalia wapagazi wa mizinga ya mahandakini kwa kuwa nilikuwa ni mimi tu niliyejua Kiswahili kuliko Wazungu wengine tuliokuwa nao. Kisha nikapewa kazi ya upelelezi pamoja na kikosi cha maskauti wa kienyeji ambao hapo kwanza walikuwa viongozi wa Wazungu waliokijakija Nairobi kwa kutaka kuwinda au kukagua nchi.

Basi mpaka hivi leo bado nimo katika masikani ya kibantu. Vita kuu hiyo ya kwanza, Afrika ya Mashariki imepoteza maisha ya watu zaidi ya laki kuliko vita ya Boer. Huku Afrika ya Mashariki vita iliendelea zaidi kuliko Ulaya. Mwisho wa vita ulipotangazwa Ulaya, tarehe 11 Novemba 1918, huku kulikuwa bado na kivumbi cha kutosha mpaka maadui walipofukuziwa Northern Rhodesia kutoka Tanganyika. Wakati huo nikawa mkalimani wa Askari wa farasi na baadaye kidogo skauti tena pande za Mozambiki ambako maadui walirudishwa nyuma baada ya kujaribu kuteka zana na chakula katika ngome zetu.

Vita ilipokwisha nikawa Bwana Shauri katika nchi ya Kenya niliyefungua Boma la Kisii. Kisha nikafanya kazi ya Polisi katika baraza za mahakimu kadha wa kadha. Kazi hii ikanifikisha mpaka Ruanda. Kwa kuwa kazi hii ilihusiana na misitu na nyika tu, moyo wangu ukatokea kuipenda sana kazi hii niliyonayo sasa yaani kuwinda, ambayo hata nilipokuwa Bwana Shauri huko Kenya niliwahi kuifanya pengine pengine. Basi kazi hii ya kuwinda ikanipeleka Tanganyika ya kusini ambayo ni pori moja tu kubwa lenye wanyama wengi ajabu. Wawindaji wachache sana wanaolijua pori hili nilihadithialo la Tanganyika ya kusini. Huko nikatanga maporini hovyo. Wanyama, hasa ndovu, walibidi wauawe kwa jitihada zote zinazowezekana na binadamu kwa jinsi walivyokuwa waharibifu wa mengi. Mabwana Nyama na Askari nao walijilazimisha kujitahidi kuwateketeza kama walivyoweza. Nami nikaruhusiwa kupiga ndovu thelathini kwa mwaka mmoja na ndovu watatu kila mwaka kwa cheti cha ushuru wa biashara ya meno au pembe za ndovu.

Miaka hiyo ninayoihadithi nilikuwa na vijana jasiri waliokuwamo katika msafara wangu wa kuwinda. Baadaye nilipokuwa nikifanya kazi ya kuwinda viboko katika nchi ya Rufiji, ambako kazi ilikuwa ya hatari zaidi kuliko ile ya kuwinda ndovu, vijana hao walikuja tena kuandika kazi. Kama tujuavyo, kujitosa mitoni na mabwawani katika nchi ya Rufiji, mwenye mijimamba ya umambani, ni jambo lisilofikiriwa kabisa na Mrufiji wa Rufiji. Walilazimika wajitose kumfuata kiboko aliyekufia katikati ya bwawa ili aletwe maji haba apate kuchanjwa (kupasuliwa au kuchunwa kwa kuitafuta ile faida yake ambayo ni mafuta, ngozi na meno). Jinsi nilivyoungana na wafanya kazi hawa, ilikuwa kama wote ni ndugu kabisa. Wakicheka hucheka, na wakifanya kazi huifanya. Sote tukapendana. Mimi nikawa ni mkubwa wao niliyependwa sana. Maisha haya yakaniongoza katika ukweli wa dunia. Niliyoyaona yatosha kunihakikisha kwamba sisi binadamu wote ni wamoja tu tuliotofautishwa kwa rangi na hali ya nchi mbali mbali.

Kwa mengi vijana hawa walifanana na vijana wengine niliokuwa nao Canada, New Zealand, Amerika, Uingereza, Ufaransa na pengi pengine. Kwa mfano ukatili juu ya wanyama uko katika watoto wa Kizungu na wa Kiafrika. Jambo hili laonyesha jinsi tabia zilivyofanana.

Mtumishi wangu Juma, niliyeandika habari zake katika vitabu vya 'Masimulizi ya Mtawa Maporini', ni mmojawapo katika mia wanaoambatana na wawindaji wa Kizungu kwa kuelekea. Wengi kama Juma wamewatunza mabwana wao wa Kizungu maporini, wamewaokoa katika hatari kubwa hata pengine wamepata kuwaulia ndovu wenye pembe kubwa kubwa na kuwapatia faida nyingi sana.

Juma alikuwa mjanja wa kupendeza. Siku moja nilipiga risasi tano kwa swala watano lakini risasi zote ziliwapitia chini ya kidari na kuwakosa. Tulipofika kambini Jumbe mmoja mroho wa nyama akaja kuuliza kama kuna nyama au hakuna, Juma akamjibu hakuna. "Mbona nimesikia mishindo mitano?" Jumbe akamwuliza. "Ikiwa haja yako ni mishindo mitano," Juma akajibu, "basi chukua." Jumbe akasema, "Wacha utani bwana, niambie kweli." Juma alipoona anataabishwa na yule Jumbe, akasema, "Mishindo mitano uliyoisikia ilikuwa ya furaha ya harusi.” Siku moja nilipokuwa nakwenda kuwinda na wavulana wengine nilimwuliza Juma atafanya nini atakapokuwa anaangalia kambi maana sikutaka akae bure kama jeta. Akageuka na kutazamatazama kibanda changu cha nyasi kilichojaa mashoka ya kuchanjia viboko, kiti changu cha ngozi kilichokuwa chini ya mkuyu uliojaa ninga tele, kisha akasema, "Nafikiri nitapiga deki na kusafisha vioo vya madirisha leo."

Asubuhi moja alinijia na mjusi mdogo mkononi mwake akichekacheka. Kwa kando yetu kidogo kulikuwa na mpilipili hoho mahali palipokuwa kibanda cha jamaa fulani hapo kwanza. Akauendea ule mpilipili, akausafishia na kuujengea uwigo mdogo, kisha akamtia yule mjusi ndani yake. Akaja nilipokuwa akasema, "Je, unaionaje bustani yangu?"

Nilipokuwa Dar es Salaam katika nyumba ya bibi mmoja, watoto wake walinirukia na kunishangalia kama walipata kuniona zamani. Siku ya pili katika ofisi ya bwana mmoja paka akanirukia pia. Yule bwana akasema kwamba mimi nilikuwa mtu wa kwanza aliyenifanyia vile. Katika nchi ya Rufiji kila mara watoto walikuwa wakisukuma basikeli yangu mahali palipoinuka kidogo karibu na kambi yangu. Siku moja walipokuwa wakisukuma hivi, nikaona basikeli yangu inayumba; nilipotazama nyuma, nikamwona mmoja amepanda juu ya kitako cha nyuma. Jinsi nilivyokuwa nikipendwa na kuzoewa kwa upesi na viumbe wenzangu yasangaza sana.

Nakumbuka nilipokuwa mwalimu Sydney, niliona taa zinawaka katika ukumbi wa kulala watoto usiku nilipokuwa natoka sinema. Nikavua viatu vyangu nikawanyatia wale watoto waliovunja amri yaani kuwasha taa saa ile. Nilipofika juu nikawaona watoto wawili wa matajiri wakubwa sana, wengine wawili wa kawaida wamelizunguka beseni lililojaa biskuti, maziwa ya kopo, chokoleti, mikate na samaki wa kopo wakila kwa mikono huku wakifyonza vidole vyao. Nikajikohoza kidogo ili nipate kuwashitua. Wote wakaacha kula na mmoja akageuka taratibu sana. Aliponiona tu, akaendelea kula na kuwaambia wenzie, "Ah, kumbe mwalimu Baka tu huyo, karibu mwalimu ndiyo hivyo tena." Nikawaambia ningelikula kama wasingelichanganya na wale samaki wa kopo. Asubuhi yake wote walikubali maneno yangu.
Mkuu asante sana kwa ku share hii kitu. Nlikuwa sijawahi kumsikia kabisa. Kumbe Tanganyika ina historia ndefu lakini watu wengi hawaijui.
 
Jamaa alikuwa muwindaji wa Tembo na Viboko. Miaka hiyo kuwinda hao wanyama haikuwa ujangili, watu wa Rufiji walimpenda sana.
Ndio yale yale, alikuwa akijilimbikizia nyara, Eti kuwinda wanyama haikuwa Ujangili. Kwa sababu ilitokea Africa ndio maana wanasema hivyo na siyo kwamba hakuwa imepigwa vita nchi zingine kama za Asia.
Alikuwa akiwasaidia kuua tembo walioharibu mazao yao. Pia aliwapa ajira kwenye kazi zake za uwindaji.
I find that hard to believe. Walimpenda kwa ile inatwa "stokholm syndrome" labda.... nadhani, na sio kwa ule upendo wa kibinadamu.

Aliwapa ajira ama aliwalazimisha kufanya kazi? Hivi kuna mzungu aliyekuja wakati huo akaamua tu kuwapatia ajira waafrica na wakapewa mishahara stahiki?

Je, kuna hata familia moja, leo, Rufiji, inaweza kusema 'tulifaidika na ujio wa huyo beberu?'
 
Ndio yale yale, alikuwa akijilimbikizia nyara, Eti kuwinda wanyama haikuwa Ujangili. Kwa sababu ilitokea Africa ndio maana wanasema hivyo na siyo kwamba hakuwa imepigwa vita nchi zingine kama za Asia.

I find that hard to believe. Walimpenda kwa ile inatwa "stokholm syndrome" labda.... nadhani, na sio kwa ule upendo wa kibinadamu.

Aliwapa ajira ama aliwalazimisha kufanya kazi? Hivi kuna mzungu aliyekuja wakati huo akaamua tu kuwapatia ajira waafrica na wakapewa mishahara stahiki?

Je, kuna hata familia moja, leo, Rufiji, inaweza kusema 'tulifaidika na ujio wa huyo beberu?'
Usimjaji mtu kabla ya kumjua. Japo tunaweza kusema vitabu vyake vinaweza kuwa biased, lakini visome na umjue, na uyajue matendo yake kabla hujamhukumu. Msome kama humu, "Maisha haya yakaniongoza katika ukweli wa dunia. Niliyoyaona yatosha kunihakikisha kwamba sisi binadamu wote ni wamoja tu tuliotofautishwa kwa rangi na hali ya nchi mbali mbali."
 
Usimjaji mtu kabla ya kumjua.
Hio ni kweli na ni kanuni ya kidunia, ila historia haidanganyi. Sidhani kama nahitaji muongozo katika hilo. But respectfully, thanks.

Japo tunaweza kusema vitabu vyake vinaweza kuwa biased, lakini visome na umjue, na uyajue matendo yake kabla hujamhukumu.
Ni ngumu, lakini nitajitahidi just for the sake ya huyu Bwana Rufiji
Msome kama humu, ☆ "Maisha haya yakaniongoza katika ukweli wa dunia. Niliyoyaona yatosha kunihakikisha kwamba sisi binadamu wote ni wamoja tu tuliotofautishwa kwa rangi na hali ya nchi mbali mbali."
Nimekuelewa Mkuu...vilvile hayo ☆maneno yake yanatuambia kwamba mtizamo wake wa Mwafrika ulibadilikia, ikiwa ina maana kabla ya hapo alikuwa akituita perhaps "Savages" na alituona kama wanyama tu. Let's call a spade a spade.

===
Nitakisoma kwasabau tu napenda First hand stories(Biographies za 1400-1800) pamoja na Journals zao, barua zao n.k zikienda Ulaya(back n forth)na baadae marekani-very informative especially, kwenye kutujaji-ambazo zinaakisi ukweli kuhusu wao wenyewe na mitizamo yao, na ukweli wa maisha yao wakiwa Ulaya enzi hizo, kabla hawajaanza propaganda. zao za kututawala
 
3. ZIKIRI NA BENI

NILIKUWA taabani niliporudi kutoka maporini kuwinda, kwenye jua kali kama nini sijui chini ya anga kavu za samawi. Nikavua nguo zangu zilizokuwa zimelowa jasho chapa na kujimwagia ndoo ya maji baridi yaliyotoka mvuke kama yakichemshwa kwa joto la mwili wangu. Nikajinyoosha penye kitanda cha chanja mpaka Juma aliporudi kutoka mjini na kunipikia chai nzuri iliyoniburudisha.

Nikajiburudisha chini ya miembe iliyokuwa na kivuli cha kutosha mbele ya kambi yangu mpaka majira ya saa kumi jioni jua lilipozidi kupungua. Upepo mzuri ukanipepea na kuniletea riha nzuri ya majani na mauwa ya maporini pamoja na hewa ya joto iliyotoka mbugani. Videge vikaimba na kurukaruka. Mara nikasikia sauti tamu ya marimba ikija kambini kwangu. Alikuwa Momadi.

Ingawa alionyesha kama anapita wima, aliponiona akasimama na kunisabahi.

"Mwimbo gani uliokuwa ukipiga?" nikamwuliza.

"Mtoto wa Sungura." Akajibu.

"Sasa unakwenda wapi?"

"Mohoro." Mohoro alikokuwa akienda ni mji wa zamani sana kwenye bandari ya majahazi. Bahari ya Hindi iko maili kumi na mbili kutoka Mohoro mjini. Mto Mohoro, ni mkubwa wa kuweza kupitisha majahazi makubwa mpaka forodhani Mohoro. Waarabu na Washerazi walifanya masikani katika mji huu hapo zamani. Kwa hiyo wenyeji wa Mohoro wamekuwa mafundi wa kuunda na kujenga kwa elimu waliyoipata kwa hawa Waarabu na Washerazi. Ni mji wa kutamanisha kwa mengi uliyonayo juu ya udogo wake.

Nikamwuliza kama kuna ngoma Mohoro. Hakunijibu lakini jinsi alivyocheka, nilijua kama kuna ngoma. "Bila shaka kuna ngondo leo huko," nikamwambia, "ningoje tufuatane basi." Nikachukua kurunzi yangu, kibiriti, bunduki na risasi, tukafuatana. Jua likatoweka. Tukayaepaepa mashimo ya nyayo za ndovu yaliyofanywa tangu masika yaliyopita mpaka tukaukaribia mji wa Mohoro.

Tukapita katika mtaa wa vibanda vya udongo na majani mpaka tukafika kwenye kundi la watu waliokuwa wakizikiri. Kijana mmoja katikati yao alikuwa ameshika mwanzi mrefu uliokuwa mwanzi, au tuseme mlingoti kabisa wa bendera ile iliyokuwa na upana na urefu wa futi nane nane. Bendera hiyo iliandikwa kwa nakshi herufi za Kiarabu kwa rangi ya dhahabu iliyochanganyika na rangi ya uwa la waridi jekundu. Sauti zilizotoka vifuani mwao hazihadithiki. Kila mmoja alijitahidi kuvaa kanzu safi nyeupe ya kupendeza. Waliojiweza walivaa kanzu za darizi na wale wenzangu miye walivaa za hivyo hivyo tena. Hao mashehe basi, walikuwa na kila namna ya majoho na vinusukoti. Tangu majoho ya vinyonga mpaka vinusukoti vya hudhurungi.

Kofia za tunga na za baragashi, hazisemekani tena. Wengine walijaza kanzu zao buluu hata zikaonekana kama ni kanzu za kibuluu kabisa.

Tukatazama zikiri mpaka hamu yetu ilipokwisha. Momadi akaonelea heri turudi nyumbani baada ya karamu kwisha. Mohoro kwa sifa za mpunga tu imepasi. Kila karamu huanguka mpunga mpaka watu wakasema hiki nini. Tulipofika kambini nikamkuta mtu amekaa katika baraza ya kibanda changu. Aliponiona akainuka na kuniamkia. "Subalkheri Bwana." "Masalkheri." Nikamjibu.

"Nasikia kuwa unapiga nyama bwana," akasema Juma alipokuwa akiweka bunduki na tochi yangu mahali pake pa kawaida kwa hadhari ya tukio lolote la hatari usiku. Nikaitikia kwa kichwa. "Basi sisi," yule mtu akaendelea kusema, “tumekuja na jeshi letu la zikiri kutoka Mbwera kuja kudhikiri huku wakati huu wa mwaka. Haja yetu hasa kwa kesho asubuhi, ni kitoweo cha nyama ya porini kwa kufanyia karamu yetu kwani huku hakuna hata mbuzi wa kuweza kununua. Kama ukitufanyia msaada huo bwana, tutashukuru sana sana. Angalao wawili watatu tu, tutakuombea dua zuri sana kwa Seyydina Abdulkadir na Sheikh Lila. Hata kama kwa gharama bwana, tafadhali sana kwani mwezi huu ni mwezi mtukufu sana kwetu sisi Waisilamu waaminifu wa haki.”

Shekhe huyu aliyenijia nyumbani kwangu kutaka niwapigie nyama alikuja na kikundi chake cha dhikiri nyuma yangu mimi nilipokwenda Mohoro kutazama dhikiri ingine. Nikakubali kuwapigia nyama asubuhi yake lakini nilikataa kuwauzia. Pia sheria za Walinzi wa wanyama haziruhusu kufanya biashara kwa cheti cha nyama bali kwa matumizi ya mwindaji na wafuasi wake tu. Basi kama nilivyokwisha sema, asubuhi nikawapigia kongoni watano. Nilipompiga kongoni wa kwanza, wale wengine walipigwa na butaa wasijue la kufanya. Hawakupata harufu yangu wala hawakuweza kuniona. Hawakujua upande gani risasi ilikotoka. Basi kwa bahati njema hii nikaweza kuwapiga wengine wanne bila taabu. Mpaka watu walipokwenda kuwachinja wale niliowapiga kwa sheria ya dini, ndipo wengine walipong'amua na kukimbia.

Shekhe alipoona nyama imekuwa tayari akawaamrisha watu wake wafanye kazi ya kukatakata na kuipeleka nyumbani kwao walikofikia. Wakafungafunga na kuondoka na mizigo yao vichwani. Walionekana ni wanaume hodari wa kutosha walipoifanya kazi ile ya nyama katika mavazi ya uwinda. Wanapovaa kanzu zao nyeupe na kuringa mabarabarani kwa mikwaju yao myembamba na laini huonekana kama mizebe ya wapi sijui.

Jua lilipoanza kupunga tu, nikafikiwa na kikosi cha wapiga beni waliongozwa na mtu mmoja aitwaye Simba Karata wa Mohoro mjini ingawa kwao hasa ni Tanga. Ama hadi beni lake lilitia fora. Yeye mwenyewe alikuwa na tarumbeta ndogo hivi iliyopondekapondeka hata alikoiokota anakojua mwenyewe. Wengine walikuwa na filimbi za mianzi na nanda moja kubwa hivi la Kizungu lile la kuvutavuta, vinanda vya midomo, manyanga na matasa yaliyofanywa kwa vipande vya juu vya madebe ya mafuta ulaya kwa kukata vile vishikizo vyake. Mkewe Simba Karata, Mwajuma kwa jina, alitangulia mbele amevaliavalia mwenyewe na rangi za kila namna usoni, akiringa vilivyo huku watu wakimshangilia, na kumwita "Kuini! Kuini!”

Mawingu ya mvua yakatanda na kuzidi kuwapa watu furaha kwani nyakati za mvua zilikuwa karibu sana. Kwanza wakaimba wimbo uliokuwa na maneno haya: "Binti Hasani wee, wacha wivu, una mwana kumgongo kama kenge." Kisha wakaimba, "Wamitemba nakutuma kanitie bibi yangu, Bibi yangu kanambia jina lake silijui." Nyimbo hizi zikanifurahisha sana na vilivyo. Mzee Baka nami nikalamba mdomo wangu kwa utamu nilioletewa na vijana wa vijijini. Sikuweza kuuita Mohoro mji ingawa kweli hapo zama boma la Majerumani lilikuwa Mohoro. Mpaka hivi leo Rufiji nzima hakuna kijiji kama Mohoro. Bado Mohoro haujawa mji.

Mwisho
 
Back
Top Bottom