Ronaldinho alikuwa zaidi ya Messi Barcelona

Dinho ni mkali zaidi ya Messi, nadhani kwa miaka 20 iliyopita(1992-2012) wa kumlinganisha na Dinho ni Zizzou peke yake na sio huyu mtumia HGH.

Nakubalian na Elizabeth Dominic kwamba LM anabebwa sana na vyombo vya habari.

LM ana mkataba wa udhamini na Adidas, ambao wana mkataba pia na FIFA, kwa hiyo Adidas wanahakikisha wanatoa mchezaji bora ili kukuza biashara yao. Kwa sasa FIFA ya Blatter iko extremely corrupt. Kwa hiyo wachezaji wanaodhaminiwa na Nike, Puma na Reebok kushinda tuzo itakuwa sio rahisi.
 
Ronaldinho WAS the best, Messi IS the best
kwenye dini ya messi wewe ndio utamshikia chetezo.....sasa ubishi wa nini? unakuwa mbishi kama waha bana....wale wanabishana kwenye treni na behewa zima....
 
Thread inasema Ronaldinho ALIKUWA zaidi ya Messi Barrcelona.

nauhakika Gaucho akianzisha Dini basi Companero lazima uwe muumini.

Ronaldinho ni underachiever, kwa kiwango alicho nacho alipaswa kufanya mambo makubwa yanayokaribiana na anayofanya Messi - alipoteza sana muda PSG na baada ya kutoka Barcelona akaanza kuendekeza starehe halafu alivyoanza kuwa fiti tena tukashindwa kumuona kwenye WC 2010 Afrika Kusini, HIS LAST CHANCE TO REDEEM HIMSELF NI MARACANA 2014!
 
kwenye dini ya messi wewe ndio utamshikia chetezo.....sasa ubishi wa nini? unakuwa mbishi kama waha bana....wale wanabishana kwenye treni na behewa zima....

Rejea:

 
kwa kuwa inawezekana inglishi is not richabo nimeomba mkalimani atafsiri maneno hayo hapo aliyoyasema ronaldinho kuhusu messi kama ifuatavyo:

"katika miaka ya hivi karibuni messi amecheza mpira katika kiwango cha juu sana ambacho hatujawahi kukiona kabla kikichezwa na mchezaji yoyote" - ronaldinho

hakuna lugha gongana hapo, ronaldinho anaamanisha kuwa hata yeye hajawahi kucheza mpira katika kiwango cha messi!
 

Da mnabishana hadi na wachezaji wenyewe ambao ndio wanapigia kura mchezaji bora - wamempigia kura mchezaji mwenzao Messi kwa miaka 4 mfululizo na Ronaldinho mwenye kakiri kuwa kiwango cha huyo dogo aliyemkabidhi mikoba Barca hakijawahi kuonekana kabla!
 
Miaka inavyozidi kwenda ndo vipaji vya soka vinazidi kupotea!messi anaonekana mkali kwakuwa yupo katika era ambayo haina wanasoka wenye vipaji ndo maana mbio zao za kushindania yuko yeye na ronaldo tu....angalia ronaldinho gaucho jinsi alivyokuwa anapata ushindani na wenye vipaji vya ukweli!gaucho akiwa dimbani anaweza akajibadilisha akawa pima maji,mkandarasi,feni au mabeki wakijifanya wajanja akajigeuza maji hapo ndo hazuiliki!
 
Tatizo la kuangalia mpira ukubwani ndio hili. Usimdharau baba yako sababu amezeeka. DINHO HAKUNAGA KAMA YEYE.
 
Halafu hata huyo Dinho mwenyewe alishakubali Messi ni NOUUUUMAAAA!!!!!!!!!
Mkuu Kalumbesa, kuna takwimu umewawekea pale juu hakuna hata mmoja wao atakayezikanusha! Wanazipita kama hawazioni huku mioyoni mwao zinawachoma! Haahaaa, HAKUNA KAZI NGUMU KAMA KUPAMBANA NA UKWELI....
 
Dhino ni hana mfano wake, alikuwa na uwezo wa kusimama yeye kama yeye. Haka ka-messi kanabebwa na team tu, hakana lolote. Pale barca hata mimi niwe coach makombe kibao batwaa na sintokosa kama Arsene Wenger..!
 
Amekiri bila yeye binafsi kujijumuisha, huyu ni mtu mzima na busara zake, hawezi sema yeye ni zaidi ya Messi..! Ni juu yetu sisi tunaoijua soka tuchuja bumba na mchele..! Mess bado sana kumfikia Ronaldino Gaucho..! Tofauti ni kwamba Dhino alikaa kwenye peak muda mfupi ukilinganisha na haka ka-messi.! Pili barca ya ka-messi si ya Dhino, hii imekamilika hata wewe upewe team una uhakika wa vikombe na hutoadhirika kama Aserne Wenger
 
Nimeangalia hii video na nimezidi kujihakikishia kuwa Ronadinho alikuwa ni SHOWMAN zaidi kuzidi wenzake. Akiwa uwanjani au popote pale, alifanya watu wafurahi hata kama hakucheza vizuri. Mwenyewe SA nilisikitika kutokumuona kwa sababu kwake yeye lazima huwa anafanya kituko fulani kama vya Zlatan Ibrahimovich ila sema yeye hufanya vingi zaidi.

Ukiangalia hii Video, utagundua kuwa Trick nyingi za Gaucho, ni kama alizisoma kwa Ronaldo ila yeye anazifanya kwa kuziremba zaidi na haraka zaidi. Mpira wa Ronaldo kidogo unafanana na wa Messi kwa sababu yeye anakata chenga si kawaida. Pia Gaucho alikuwa na tatizo la kuwakimbia Mabeki kwa kadri awezavyo labda tu kama hana jinsi wakati Messi na Ronaldo wakiona Mabeki, wao ndiyo wanaona njia. Kwa hili mtu asibishe ila ajikumbushe kwa kuangalia hii video na ya kwanza.

Jambo moja ambalo inabidi nilikubali ni kuwa Ronaldo alikuwa Mzee wa kuvalisha watu chupi, khaaa!!! Yaani anapiga watu matobo hadi wanaanguka. Ila zaidi ya kupiga chenga na kufunga magoli, hakufanya kitu chochote kufurahisha watu uwanjani jambo ambalo Gaucho amewazidi wachezaji karibu wote ukiacha wachache ambao walipofunga magoli, walifurahisha watu hadi wameingia kwenye Historia kama Roger Miller na viuno vyake.

Angalia chenga za maudhi za Ronaldo ambazo nyingi unaziona tena kwa Gaucho. Pia angalia jinsi anavyowavaa mabeki kama Messi anavyofanya. Mario Balotelli angeliweza kumfikia Gaucho kama angelikuwa anacheza vizuri ila yeye naye amebaki vituko tu na mpira hakuna... Mzee wa Bunga Bunga.


Hapa chini, waone wote wawili Ronaldo na Gaucho: Ronaldo and Ronaldinho - Samba | HD - YouTube
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kalumbesa, kuna takwimu umewawekea pale juu hakuna hata mmoja wao atakayezikanusha! Wanazipita kama hawazioni huku mioyoni mwao zinawachoma! Haahaaa, HAKUNA KAZI NGUMU KAMA KUPAMBANA NA UKWELI....

Kweli kabisa ndugu yangu,unafiki kitu kibaya watu wanaujua ukweli halafu wanazuga!Messi ni habari nyingine !!
 


Aaaah Marahaba Myao wa Tunduru....
Nilisema hapo awali mtakatifu Dinho ameshinda tuzo mbele ya akina Kluivert, De Lima, Nedved, Zidane, Maldini, Mendieta, Deco Magic, Rivaldo Victor Borba Fereirra, Del Piero na alama nyingine za Soka.

Lakini hichi kibushuti kinacheza mpira na watu wa mpira wa Darasani na sio vipaji kwa sana...
 
Lakini hichi kibushuti kinacheza mpira na watu wa mpira wa Darasani na sio vipaji kwa sana...

kwa hiyo milan messi atakayoipiga mabao mwezi ujao kwenye uefa cl ni watu wa mpira wa darasani na sio vipaji kwa sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…