kwa vigezo vipi? messi kafunga zaidi ya magoli 200 akiwa barca, katoa mapande kedekede yaliyozaa magoli (assists), kafunga goli kama la maradona la wc 1986 kwa kuwapiga chenga mabeki kutoka katikati ya uwanja hadi golini, katwaa makombe 4 kwa mpigo katika msimu mmoja, kama ni kuchekacheka uwanjani na kuwachezesha orchestra mashabiki kweli ronaldinho kamzidi messi; narudia, ronaldinho alifanya mazingaombwe (magic), messi anafanya miujiza (miracles), ronaldinho ni tabasamu la soka, messi ni kicheko cha soka!na kama alivyosema ronaldinho mwenyewe, messi hakunaga!