Kanye 360
Senior Member
- Nov 8, 2017
- 163
- 236
Gusa wwAlivyo vifanya messi barca mbwa gaucho hagusi hata robo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Gusa wwAlivyo vifanya messi barca mbwa gaucho hagusi hata robo
Usikute hata gaucho hujamuona zaidi ya kuhadithiwa na mama yakoMama yangu anahusikaje hapa ww sindie unaetaka takwimu...nenda uko kwenye source siyo utusumbue tu hapa na stastics stastics
Wewe ni msukuleWe ni mbwa jike
Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na vilabu vya PSG, Barcelona na AC Milan, Ronaldo de Assis Moreira Maarufu kama Ronadinho Gaucho amestaafu soka.
Licha ya Ronadinho kutocheza soka la kiushindani lakini toka mwaka 2015 amekua akicheza michezo ya mabonanza
Kaka na wakala wa mchezaji huyo Roberto de Assis Moreira amethibitisha kuwa umefika mwisho kwa fundi huyo wa kibrazil kucheza soka.
Ronaldinho alianzia soka lake katika klabu ya Gremio ya nchini kwao kabla ya kujiunga na Paris St-Germain mwaka 2001 na baadae kujiunga na Barcelona alikong'ara sana.
Katika msimu wa 2010 -2011 alijiunga na Ac Milan ya Italia kabla ya kurudi kwao na kujiunga na Flamengo mwaka 2011. Kisha alichezea vilabu vya Atletico Mineiro, na Queretaro ya nchini Mexico na kurudi tena kwao Brazil katika klabu ya Fluminense.
Tujikumbushe kidogo aliyokuwa wanafanya uwanjani Ronaldinho
UshapoteaUsikute hata gaucho hujamuona zaidi ya kuhadithiwa na mama yako
Alichokifanya messi barca ni aibu kumlinganisha na wachezea mpira kama gauchoNa alifichwa kwa sababu hakuwa anacheza soka la mashindano tena kma alipokuwa Barca. Sasa hv alikuw anacheza soka starehe tu
Gaucho mbwa tuGusa ww
Lakini wamezika statistics zake zoteAnd in his era, NA WAO WALIFICHWA.
Huyo muandishi ana tofauti gani na eddo kumwembeMwandishi wa LIVESCORE.COM aliandika hivi, nanukuu;
"RONALDINHO WILL BE REMEMBERED AS ONE OF THE MOST TALENTED FOOTBALLERS OF HIS GENERATION, AND NO PLAYER SINCE, HAS BROUGHT THE SAME KIND OF FLAIR TO THE PITCH AS HE DID...!!"
Na yeye muombe statistics...!!!
Wenzako wa Ulaya walimuona na waka-appreciate kiwango chake, WEWE UPO LINDI, ETI UNATAKA STATISTICS....!!!
Sijawahi kuwa challenged na kilaza kama wewe apo dada anguUshapotea
Gaucho kilazaWe fisi tu
Safi sana tumeona statistics kwamba alikuwa kilaza tucopy & paste
MFAHAMU RONALDINHO KWA KINA NA HISTORIA YAKE KWA UNDANI HADI PALE ALIPO KWA SASA
April 26, 2017 - Leo Katika Historia
Porto Alegre, Brazil
Kimo 1.81 m (5 ft 11 1⁄2 in)[1]
Nafasi ya uchezaji Attacking midfielder / Forward
Club information
Senior career*
Years Team Apps† (Gls)†
1998–2001 Grêmio 52 (21)
2001–2003 Paris Saint-Germain 55 (17)
2003–2008 Barcelona 145 (70)
2008–2010 Milan 76 (20)
2011–2012 Flamengo 33 (15)
2012– Atlético Mineiro 9 (3)
National team‡
1996 Brazil U17 6 (2)
1999 Brazil U20 5 (3)
2000–2008 Brazil U23 27 (18)
1999– Brazil 94 (33)
Mchezaji nyota Ronaldinho alikuwa mmojawapo wa wachezaji wa Kombe la Dunia 2002 ambalo Brazil walitwaa ubingwa. Ronaldinho amekuwa mchezaji bora wa FIFA kwa kuchukua tuzo mara mbili
Huu ni msemo aliopenda kuutumia Ronaldinho usemao
“I come from a family where soccer has always been very present.” Ukimaanisha "Nimetoka katika familia ambayo soka limekuwapo toka kitambo"
KWA MUHTASARI
![]()
Ronaldinho akiwa katika mtanange enzi za udogo wake (miaka 7)
Ronaldinho Alizaliwa tarehe 21 Machi, 1980, katika mji wa Porto Alegre, Brazil, Ronaldinho alitoka katika familia ya wachezaji wa soka wa kufikia kilele cha mafanikio katika michezo. Baada ya kucheza klabu mbalimbali akiwa kinda, Ronaldinho alikuja kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu waliounda kikosi cha timu ya Taifa ya Brazili ambayo ilishinda Kombe la Dunia 2002. Ronaldinho alicheza katika vilabu mbalimbali na maarufu katika nchi za Brazil, Ufaransa, Hispania na Italia, na mara mbili ametajwa FIFA Mchezaji bora duniani.
![]()
Ronaldinho akiwa na mama yake mzazi
Maisha ya zamani
Kama nilivyoeleza hapo mwanzo Ronaldinho alizaliwa Ronaldo de Assis Moreira tarehe 21 Machi, 1980, katika mji wa Porto Alegre, Brazil. Baba yake, João Moreira, aliyekuwa mtaalamu na mchezaji wa soka na mama yake, Miguelina de Assis, alikuwa muuza vipodozi ambaye baadaye akaja kuwa muuguzi. Ronaldinho ana Kaka yake mkubwa, aitwaye Roberto Assis, pia alikuwa mtaalamu na mchezaji soka,
![]()
Ronaldinho anapomkumbuka Baba yake hushindwa kuzuia hisia zake
Ronaldinho alikuwa amezungukwa na soka kutoka siku ya kuzaliwa. ",Nimetoka katika familia ambayo soka limekuwapo toka kitambo" anasema. "Wajomba zangu, baba yangu na ndugu yangu walikuwa wachezaji wote kwa hiyo nimeishi katika mazingira hayo toka siku za nyuma., Nilijifunza mengi kutoka kwao" Nilijaribu kwa kujitoa mwenyewe zaidi na zaidi kadri siku zilivyoendelea" Anasema Ronaldinho
Hasa, Ronaldinho anamkumbuka Baba yake na kusema. "Yeye alikuwa mmoja wa watu muhimu sana kwa ajili yangu na kwa kazi yangu, ingawa alikufa nilipokuwa mdogo sana," anasema. (João Moreira alipata mshtuko wa moyo wakati Ronaldinho akiwa na umri wa miaka 8.) "Yeye alinipa ushauri bora ambao nimekua sikuwahi kuupata sehemu yoyote tena katika maisha yangu "Fanya vitu kwa usahihi na kuwa mwaminifu,.nyumbani na uwanjani Kama ni kucheza soka cheza uwezavyo. Yeye daima alisema moja ya mambo muhimu unayoweza kufanya zaidi ni kucheza mpira"
Ronaldinho alianza kucheza na kupangwa soka la vijana akiwa na umri wa miaka 7, na ilikuwa kama kijana wa soka kwanza kupokea jina la utani "Ronaldinho," kutoka jina lake la kuzaliwa Ronaldo. "Mara zote waliniita jina hilo kwa sababu kiukweli nilikuwa mdogo sana" Ronaldinho anaelezea, "Chakushangaza ni kwamba nilicheza na watu ambao walinizidi umri hata kimo. Nilipofika timu kuu ya taifa kulikuwa na Ronaldo mwingine hivyo wakaniita Ronaldinho kwa sababu nilikuwa mdogo"![]()
Ronaldinho akiwa amebebwa na Kaka yake baada ya mechi kumalizika
Ronaldinho anadai ameishi mazingira na maisha ya kimaskini kiasi chake hali anayodai ilizorotesha kiwango chake. "Nyasi tu kwenye uwanja zilikuwa katika kona," Ronaldinho anakumbuka. "Hakukuwa na nyasi katikati! Ilikuwa tu mchanga.
![]()
Ronaldinho akiwa na Kaka yake katika mafunzo ya soka
Ronaldinho ameanza kufahamika Brazili kama kijana mwenye uwezo wa kuzaliwa katika soka alipokuwa na umri wa miaka 13, Ronaldinho katika mechi moja amewahi kufunga magoli 23 katika mchezo mmoja. Wakati akiiongoza timu yake katika michuano michuano ya vijana
Ronaldinho mwenyewe anadai alikuwa na ndoto toka zamani za kuichezea timu yake ya Taifa na kupata heshima katika soka kama walivyopata wachezaji wengine kama vile Pelé, Rivelino na Ronaldo na anadai alijitahidi zana kuzifuata nyayo zao.
![]()
Kisha, mwaka 1997,Ronaldinho aliitwa katika timu ya Taifa ya watu wenye umri mdogo katika timu ya Brazili chini ya miaka 17. Katika kikosi cha Bingwa Duniani michuano iliyofanyika Misri,Ronaldinho alichaguliwa kama mchezaji bora wa mashindano. Muda mfupi baadaye, Ronaldinho alitia saini mkataba wake wa kwanza wa kuichezea Gremio, moja ya timu ambazo zilikuwa katika chat ya klabu bora katika ligi ya Brazili.
![]()
UFANISI WA RONALDINHO KATIKA SOKA
Ronaldinho alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa katika timu ya Gremio mwaka 1998 katika mashindano ya Copa Libertadores.Mwaka uliofuata, alialikwa kujiunga katika kikosi cha Watu wazima timu ya taifa ya Brazil aliposhiriki katika kombe la shirikisho nchini Mexico. Brazili ilishika nafasi ya pili katika michuano hiyo na Ronaldinho alishinda Golden Ball tuzo kama mchezaji bora wa mashindano pamoja na Golden Boot tuzo kama mfungaji bora.
![]()
Ronaldinho akaja kufahamika rasmi katika ngazi za kimataifa, mwaka 2001.Ronaldinho aliondoka Brazili na kutimkia Ulaya,alikotia saini ya mkataba wa kuichezea Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
![]()
Mwaka mmoja baadaye,Ronaldinho kwa mara ya kwanza alishiriki katika fainali za kuwania Kombe la Dunia ambapo Brazili ilifanikiwa kubeba kombe la Dunia kikosi pia ambacho kilikuwa na wachezaji kama Ronaldo na Rivaldo. Ronaldinho alifunga mabao mawili katika mechi tano, ikiwa ni pamoja na mchezo wa mshindi katika robo fainali dhidi ya Uingereza, na Brazil akaendelea na ubabe wake kwa kumpiga mjerumani katika fainali hizo na kuandika historia ya fainali ya tano ya Kombe la Dunia
Mwaka 2003, Ronaldinho alitimiza ndoto ya maisha kwa kujiunga FC Barcelona ya Hispania ligi, moja ya Klabu zilizokuwa tishio kubwa mpaka hivi sasa.
Baada ya kucheza soka la madaha na liliowafurahisha watazamaji wengi wa mpira akiwa katika klabu ya Barcelona Ronaldinho alipata mafaniko makubwa sana katika soka na kiuchumi kupitia matangazo mbalimbali pamoja na animation clip na video za machenga yake ambazo zilikuwa zikipata katika tovuti mbalimbali za kibiashara. Ronaldinho pia Aliweza kuiingizia Barcelona, Ac Milan na timu ya Taifa kiasi kikubwa cha pesa kupitia jezi zake ambazo zilikuwa zikivunja rekodi ya kuuzwa.
Mwanandinga huyo alikuwa na kipaji cha kiwango cha Almasi katika soka.
Nakumbuka kama waliwahi cheza pa1 barca kama sijakosea na alipotoka ndio naona messi kaanza wika,Mimi ni shabiki mkubwa wa messi ni kweli messi tunaweza sema ndiye mchezaji bora kwa sasa kutokana na vitu vyake lakin ukisema umlinganishe na gaucho utakuwa unamuonea sana Gaucho ni habari nyingine anavitu vya kujua yeye tu yule jamaa sijaona kwa kizazi cha leo sijajua wale wa nyuma yangu sijawahi kumuona maladona enzi zake nilikuwa sijapata upeo wa kufatilia mpira watanisaidia wakongwe hapa.
Itakuwa vema ukamuelezea huyo unayempenda siyo kuponda tu Bila kumuelezea unayempenda,chuki haikusaidii chochoteSafi sana tumeona statistics kwamba alikuwa kilaza tu