SI KWELI Ronaldo amesepa Saudia kwenda Hispania kukwepa mabomu ya Iran

SI KWELI Ronaldo amesepa Saudia kwenda Hispania kukwepa mabomu ya Iran

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Ronaldo 1.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikieleza kuwa ndege binafsi inayomilikiwa na nyota wa soka wa Ureno, Cristiano Ronaldo, imeruka kutoka Saudi Arabia usiku wa manane kuelekea Madrid, Hispania, jambo linalohusishwa namshambuliaji huyo kuwa ameondoka nchini humo kufuatia kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi Mashariki ya Kati.


Je, ni kweli Cristiano Ronaldo aliondoka Saudia?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha ndege aina ya Bombardier Global Express XRS inayomilikiwa na Ronaldo kwa mujibu wa Flight Radar24 iliondoka Riyadh na kuwasili Madrid, Hispania Machi 03, 2026 lakini haikuondoka na mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al Arabiya English inaeleza kuwa Cristiano Ronaldo hakuondoka Saudi Arabia licha ya ripoti zilizosambaa sana na vyombo mbalimbali vya habari zikidai kwamba aliondoka nchini humo kutokana na mzozo unaoendelea katika eneo hilo. Tovuti hiyo inabainisha Christiano alionekana katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo siku ya Jumanne.​
4aa54cce-0493-4303-8d6a-b82bfd1c4200_16x9_1200x676.jpg
Aidha mwandishi wa habari za michezo Fabrizo Romano kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X alieleza kuwa ripoti zilizosambaa katika vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu Cristiano Ronaldo kudaiwa kuondoka Saudi Arabia pamoja na familia yake si za kweli kwani Cristiano anaendelea kupatiwa matibabu katika uwanja wa mazoezi wa Al Nassr FC baada ya kupata tatizo katika mchezo uliopita.

"Reports on international media about Cristiano Ronaldo who left Saudi Arabia with his family are wide of mark. It’s a fake news as Cristiano is now doing threatment at Al Nassr training ground after issues in last game. Cristiano has not left Saudi to return to Madrid."​
Back
Top Bottom