Ronaldo amwandikia ujumbe wa heshima Messi baada ya kuaga Argentina

Ronaldo amwandikia ujumbe wa heshima Messi baada ya kuaga Argentina

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Cristiano Ronaldo amemtumia ujumbe wa heshima Lionel Messi baada ya nyota huyo kucheza mechi yake ya mwisho akiwa na timu ya taifa ya Argentina.

1791399136269.png

Ronaldo amesema Messi ametumia miaka mingi akiitumikia Argentina na ameacha historia itakayodumu milele, huku akimtumia pongezi na heshima kwa mafanikio yote aliyoyapata akiwa na taifa hilo.

“Leo, miaka mingi ya kuitetea nchi yako na historia itakayodumu milele. Heshima yangu yote kwa yale uliyoyafanikisha ukiwa na Argentina.” Ronaldo ameandika.

Ujumbe huo unaendelea kuonyesha heshima iliyopo kati ya mastaa hao wawili ambao kwa miaka mingi wamekuwa wapinzani wakubwa katika soka la dunia, huku wakitawala kizazi kimoja na kuandika historia isiyosahaulika.

𝐑𝐎𝐍𝐀𝐋𝐃𝐎 𝐌𝐄𝐒𝐒𝐀𝐆𝐄 𝐓𝐎 𝐋𝐈𝐎𝐍𝐄𝐋 𝐌𝐄𝐒𝐒𝐈 🇵🇹🤝🇦🇷.jpg
 
Meanwhile mashabiki wa Argentina

"Ronaldo ni mtu wakati Messi ni Mungu"
Screenshot_20261007-223643.png
 
Ila CR7 ana makusudi si angeandika kihispania aeleweke fasta, anataka mwenzie atafsiriwe na wanae🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom