Cristiano Ronaldo amemtumia ujumbe wa heshima Lionel Messi baada ya nyota huyo kucheza mechi yake ya mwisho akiwa na timu ya taifa ya Argentina.
Ronaldo amesema Messi ametumia miaka mingi akiitumikia Argentina na ameacha historia itakayodumu milele, huku akimtumia pongezi na heshima kwa mafanikio yote aliyoyapata akiwa na taifa hilo.
βLeo, miaka mingi ya kuitetea nchi yako na historia itakayodumu milele. Heshima yangu yote kwa yale uliyoyafanikisha ukiwa na Argentina.β Ronaldo ameandika.
Ujumbe huo unaendelea kuonyesha heshima iliyopo kati ya mastaa hao wawili ambao kwa miaka mingi wamekuwa wapinzani wakubwa katika soka la dunia, huku wakitawala kizazi kimoja na kuandika historia isiyosahaulika.